Mdau: Baada ya baba kupotea, rafiki yake ametuma watu wenye silaha kuvamia nyumba yetu akitaka tuhame

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Apr 18, 2017
2,813
11,991
Andiko la Mdau wa kutoka Goba kuhusu watu wanaotaka kupora nyumba yao baada ya baba yao kupotea:

Usiku wa kuamkia leo Alhamisi Julai 6, 2023 kuna watu wamevamia katika nyumba yetu iliyopo Goba, Mtaa wa Kiburuni, Dar es Salaam na kuanza kuvunja sehemu ya nyumba, ikiwemo madirisha na milango, baada ya hapo wakamjeruhi ndugu yetu mmoja na kusema kuwa kama hatutahama kwenye nyumba hiyo watarejea kesho yake ambayo ni usiku wa kuamkia Ijumaa Julai 7, 2023.

Wahalifu hao walifika wakiwa makundi, wanne wakaingia ndani na wengine ambao sijui idadi yao walibaki nje, majirani wanasema kuwa walikuwa na silaha za moto ndio maana hata wao walisita kutoa msaada kwa haraka.

Walikuwa wanamtaka kiongozi wa familia ambaye alikuwa katika chumba kingine, wakati akifanya uharibifu huo wakamchukua ndugu yetu mmoja na kuanza kumpiga huku wakimtaka aseme alipo ndugu yetu ambaye ni mtoto wa kwanza wa mzee.

Alikataa kutii kile walichotaka na wakaendelea kumpiga hadi alipopata nafasi ya kuwatoroka na kwenda kuripoti Polisi.

Polisi walikuja baadaye wakakuta wahalifu wale ambao tunaamini wametumwa na aliyekuwa rafiki wa baba yetu kwa kuwa ndiye ambaye tuna mgogoro naye wa nyumba tunayoishi.

Kwa nini rafiki wa baba anahusishwa?
Anahusishwa kwa kuwa mshukiwa anayefahamka kwa jina la Thomas Daniel Kilumile, mzaliwa wa Iringa ambaye kwa sasa anaishi Mwanza, alikuwa ni kama ndugu kwetu wakati baba alipokuwa nasi.

Wawili hao walikuwa marafiki na hata kufikia hatua ya huyo rafiki yake kuwa anakuja kwenye nyumba yetu analala na kwa pamoja walikuwa wakimiliki kampuni.

Walikuwa wafanyabiashara walioshirikiana muda mrefu, ghafla Mwaka 2018 baba akiwa ametoka na gari kwenda kwenye mizunguko yake ya kawaida hakurudi tena mpaka leo.

Hatujui kama ni mzima au ameshakufa na hata gari lake pia halikuwahi kuonekana.

Rafiki wa baba aanza kudai nyumba
Baada ya baba kupotea, ndugu tukaanza kufuatilia madeni na biashara zake alizokuwa anafanya, hapo ndipo sokomoko likaanza, huyo Thimos akaja kudai kuwa nyumba tunayoishi ni mali yake na tunatakiwa kuhama.

Mgogoro ukaanzia hapo, tukamtaka aende Mahakamani ili haki ipatikane, hakufanya hivyo, aliishia kwenda Polisi na suala letu lilifika hadi Serikali za mtaa lakini hakukuwa na utatuzi uliopatikana.

Nyaraka za nyumba zinaonesha zina jina la baba yetu aliyepoteza lakini Kilumile alikuja na nyaraka anazodai ni za kiwanja na kuwa kile ni kiwanja chake.

Kinachoshangaza ni kuwa rafiki huyo wa baba hakuwahi kusema chochote kuhusu umiliki wake wa nyumba hiyo, na kwa kinachoendelea tunapata mashaka kupotea kwa baba na hiki kinachoendelea.

Vitisho
Mzee Kilumile alianza kutupa vitisho yeye na mwanaye ambaye ni Daniel Kilumile wakitutaka tuhame, shauri lilifika Kituo cha Polisi Goba, kwa kuwa alikosa ushahidi akawa ni kama ameshindwa kuendelea.

Nyumba hiyo ilianza kujengwa Mwaka 2011 na ikakamilika Mwaka 2014 ambapo ndipo familia ikahamia.

Mama yetu hayupo hapa anaishi Mwanza, aliwahi kusema rafiki wa baba anataka kutupora nyumba yetu kinyume cha sheria.

Kwa kuwa rafiki huyo wa baba mtoto wake ni mwanajeshi, amekuwa akidai kuwa lazima atatuhamisha na kwa mazingira yanayoonekana sasa inaonekana kuna vitu ambavyo anaweza kuhusika kwa kupotea kwa baba.

Tulitegemea pia baada ya baba kupotea angekuja kutuambia kuhusu biashara aliyokuwa akishirikiana na baba, tulipomuuliza hakuwa na majibu.
 
Nyumba hiyo ilianza kujengwa Mwaka 2011 na ikakamilika Mwaka 2024 ambapo ndipo familia ikahamia.

Hapo kwenye 2024, itakua umekosea kuandika
 
Kwa haya machache huyo kilumila alitakiwa tayari awe mikononi mwa vyombo vya dola akichunguzwa kuhusiana na kupotea kwa baba yenu.
Kama uliyoandika ni ya kweli, basi naamini kabisa kupitia bandiko hili hapa jamiiforums mtapata haki yenu.

Usisite kuleta update hapahapa kwa chochote kitakachoendelea.... Ila kuweni makini sana maana inaonekana huyo kilumila yupo tayari kuondoa uhai wa mtu ili tu apate hiyo nyumba
 
Andiko la Mdau wa kutoka Goba kuhusu watu wanaotaka kupora nyumba yao baada ya baba yao kupotea:

Usiku wa kuamkia leo Alhamisi Julai 6, 2023 kuna watu wamevamia katika nyumba yetu iliyopo Goba, Mtaa wa Kiburuni, Dar es Salaam na kuanza kuvunja sehemu ya nyumba, ikiwemo madirisha na milango, baada ya hapo wakamjeruhi ndugu yetu mmoja na kusema kuwa kama hatutahama kwenye nyumba hiyo watarejea kesho yake ambayo ni usiku wa kuamkia Ijumaa Julai 7, 2023.

Wahalifu hao walifika wakiwa makundi, wanne wakaingia ndani na wengine ambao sijui idadi yao walibaki nje, majirani wanasema kuwa walikuwa na silaha za moto ndio maana hata wao walisita kutoa msaada kwa haraka.

Walikuwa wanamtaka kiongozi wa familia ambaye alikuwa katika chumba kingine, wakati akifanya uharibifu huo wakamchukua ndugu yetu mmoja na kuanza kumpiga huku wakimtaka aseme alipo ndugu yetu ambaye ni mtoto wa kwanza wa mzee.

Alikataa kutii kile walichotaka na wakaendelea kumpiga hadi alipopata nafasi ya kuwatoroka na kwenda kuripoti Polisi.

Polisi walikuja baadaye wakakuta wahalifu wale ambao tunaamini wametumwa na aliyekuwa rafiki wa baba yetu kwa kuwa ndiye ambaye tuna mgogoro naye wa nyumba tunayoishi.

Kwa nini rafiki wa baba anahusishwa?
Anahusishwa kwa kuwa mshukiwa anayefahamka kwa jina la Thomas Daniel Kilumile, mzaliwa wa Iringa ambaye kwa sasa anaishi Mwanza, alikuwa ni kama ndugu kwetu wakati baba alipokuwa nasi.

Wawili hao walikuwa marafiki na hata kufikia hatua ya huyo rafiki yake kuwa anakuja kwenye nyumba yetu analala na kwa pamoja walikuwa wakimiliki kampuni.

Walikuwa wafanyabiashara walioshirikiana muda mrefu, ghafla Mwaka 2018 baba akiwa ametoka na gari kwenda kwenye mizunguko yake ya kawaida hakurudi tena mpaka leo.

Hatujui kama ni mzima au ameshakufa na hata gari lake pia halikuwahi kuonekana.

Rafiki wa baba aanza kudai nyumba
Baada ya baba kupotea, ndugu tukaanza kufuatilia madeni na biashara zake alizokuwa anafanya, hapo ndipo sokomoko likaanza, huyo Thimos akaja kudai kuwa nyumba tunayoishi ni mali yake na tunatakiwa kuhama.

Mgogoro ukaanzia hapo, tukamtaka aende Mahakamani ili haki ipatikane, hakufanya hivyo, aliishia kwenda Polisi na suala letu lilifika hadi Serikali za mtaa lakini hakukuwa na utatuzi uliopatikana.

Nyaraka za nyumba zinaonesha zina jina la baba yetu aliyepoteza lakini Kilumile alikuja na nyaraka anazodai ni za kiwanja na kuwa kile ni kiwanja chake.

Kinachoshangaza ni kuwa rafiki huyo wa baba hakuwahi kusema chochote kuhusu umiliki wake wa nyumba hiyo, na kwa kinachoendelea tunapata mashaka kupotea kwa baba na hiki kinachoendelea.

Vitisho
Mzee Kilumile alianza kutupa vitisho yeye na mwanaye ambaye inadaiwa ni Mwanajeshi wakitutaka tuhame, shauri lilifika Kituo cha Polisi Goba, kwa kuwa alikosa ushahidi akawa ni kama ameshindwa kuendelea.

Nyumba hiyo ilianza kujengwa Mwaka 2011 na ikakamilika Mwaka 2014 ambapo ndipo familia ikahamia.

Mama yetu hayupo hapa anaishi Mwanza, aliwahi kusema rafiki wa baba anataka kutupora nyumba yetu kinyume cha sheria.

Kwa kuwa rafiki huyo wa baba mtoto wake ni mwanajeshi, amekuwa akidai kuwa lazima atatuhamisha na kwa mazingira yanayoonekana sasa inaonekana kuna vitu ambavyo anaweza kuhusika kwa kupotea kwa baba.

Tulitegemea pia baada ya baba kupotea angekuja kutuambia kuhusu biashara aliyokuwa akishirikiana na baba, tulipomuuliza hakuwa na majibu.
Huyo kilumile anahela au ndio njaa imemshika anataka kupora nyumba....iteni tv uchwara waje kuwasikiliza na kuipaisha hewani
 
Sent using Jamii Forums mobile app
 
Yani mtu ukiwashwa kuulizwa maswali magumu na Serikali lazima utafute uchokozi tu.

Huyu mzee ameitia familia yake kwenye matatizo tayali...

MACHOZI YA MKIWA HAYAENAGI BURE.
 
Duuuh huyo jamaa ni kama ameangalia hapo kwa waliobaki ameona hakuna atayemzuia.

Mtu akija na mabunduki hiyo ni ishara hajiamini na anataka akutishe tu.

First off first, kakate RB police

Kisha naskushauri funga CCTV hapo home ziwe hidden, weka vinasa sauti kisha hao wehu wakija wakiwa wanakuuliza uliza maswali na wewe uwe unawajibu najua watajichanganya hapo wataweza kuji expose na utakuwa umeirahisishia kazi mahakama.
 
Andiko la Mdau wa kutoka Goba kuhusu watu wanaotaka kupora nyumba yao baada ya baba yao kupotea:

Usiku wa kuamkia leo Alhamisi Julai 6, 2023 kuna watu wamevamia katika nyumba yetu iliyopo Goba, Mtaa wa Kiburuni, Dar es Salaam na kuanza kuvunja sehemu ya nyumba, ikiwemo madirisha na milango, baada ya hapo wakamjeruhi ndugu yetu mmoja na kusema kuwa kama hatutahama kwenye nyumba hiyo watarejea kesho yake ambayo ni usiku wa kuamkia Ijumaa Julai 7, 2023.

Wahalifu hao walifika wakiwa makundi, wanne wakaingia ndani na wengine ambao sijui idadi yao walibaki nje, majirani wanasema kuwa walikuwa na silaha za moto ndio maana hata wao walisita kutoa msaada kwa haraka.

Walikuwa wanamtaka kiongozi wa familia ambaye alikuwa katika chumba kingine, wakati akifanya uharibifu huo wakamchukua ndugu yetu mmoja na kuanza kumpiga huku wakimtaka aseme alipo ndugu yetu ambaye ni mtoto wa kwanza wa mzee.

Alikataa kutii kile walichotaka na wakaendelea kumpiga hadi alipopata nafasi ya kuwatoroka na kwenda kuripoti Polisi.

Polisi walikuja baadaye wakakuta wahalifu wale ambao tunaamini wametumwa na aliyekuwa rafiki wa baba yetu kwa kuwa ndiye ambaye tuna mgogoro naye wa nyumba tunayoishi.

Kwa nini rafiki wa baba anahusishwa?
Anahusishwa kwa kuwa mshukiwa anayefahamka kwa jina la Thomas Daniel Kilumile, mzaliwa wa Iringa ambaye kwa sasa anaishi Mwanza, alikuwa ni kama ndugu kwetu wakati baba alipokuwa nasi.

Wawili hao walikuwa marafiki na hata kufikia hatua ya huyo rafiki yake kuwa anakuja kwenye nyumba yetu analala na kwa pamoja walikuwa wakimiliki kampuni.

Walikuwa wafanyabiashara walioshirikiana muda mrefu, ghafla Mwaka 2018 baba akiwa ametoka na gari kwenda kwenye mizunguko yake ya kawaida hakurudi tena mpaka leo.

Hatujui kama ni mzima au ameshakufa na hata gari lake pia halikuwahi kuonekana.

Rafiki wa baba aanza kudai nyumba
Baada ya baba kupotea, ndugu tukaanza kufuatilia madeni na biashara zake alizokuwa anafanya, hapo ndipo sokomoko likaanza, huyo Thimos akaja kudai kuwa nyumba tunayoishi ni mali yake na tunatakiwa kuhama.

Mgogoro ukaanzia hapo, tukamtaka aende Mahakamani ili haki ipatikane, hakufanya hivyo, aliishia kwenda Polisi na suala letu lilifika hadi Serikali za mtaa lakini hakukuwa na utatuzi uliopatikana.

Nyaraka za nyumba zinaonesha zina jina la baba yetu aliyepoteza lakini Kilumile alikuja na nyaraka anazodai ni za kiwanja na kuwa kile ni kiwanja chake.

Kinachoshangaza ni kuwa rafiki huyo wa baba hakuwahi kusema chochote kuhusu umiliki wake wa nyumba hiyo, na kwa kinachoendelea tunapata mashaka kupotea kwa baba na hiki kinachoendelea.

Vitisho
Mzee Kilumile alianza kutupa vitisho yeye na mwanaye ambaye inadaiwa ni Mwanajeshi wakitutaka tuhame, shauri lilifika Kituo cha Polisi Goba, kwa kuwa alikosa ushahidi akawa ni kama ameshindwa kuendelea.

Nyumba hiyo ilianza kujengwa Mwaka 2011 na ikakamilika Mwaka 2014 ambapo ndipo familia ikahamia.

Mama yetu hayupo hapa anaishi Mwanza, aliwahi kusema rafiki wa baba anataka kutupora nyumba yetu kinyume cha sheria.

Kwa kuwa rafiki huyo wa baba mtoto wake ni mwanajeshi, amekuwa akidai kuwa lazima atatuhamisha na kwa mazingira yanayoonekana sasa inaonekana kuna vitu ambavyo anaweza kuhusika kwa kupotea kwa baba.

Tulitegemea pia baada ya baba kupotea angekuja kutuambia kuhusu biashara aliyokuwa akishirikiana na baba, tulipomuuliza hakuwa na majibu.
1.Je, huyo unayemwita Kilumile anatoa hoja Zipi hasa za kudai kwamba hiyo nyumba ni mali yake?? Uhalali wa madai yake uko wapi baada ya nyinyi kumsikiliza madai yake??
2.Baba yenu hiyo ardhi aliipataje??Yaani historia ya umiliki wa ardhi kwa baba yenu ikoje??
3.Ina maana mama yenu hajui kitu chochote kuhusiana na upatikanaji wa hicho kiwanja ambacho baba yenu alijenga nyumba??
4.Wakati baba yenu alipopotea, Je, mlifuata hatua zozote zile ktk kushughulikia suala hilo?Je, mliripiti Polisi na kupata nyaraka zozote zile za upotevu wa huyo baba yenu kutoka Polisi au kutoka katika Mamlaka yoyote ile ya Serikali??
5.Baada ya purukushani za huyo Kilumile kudai kwamba nyumba aliyojenga baba yenu ni mali yake, Je, nyinyi kama watoto mlichukua hatua gani za kumhusisha Bw. Kilumile kuwa ni mshukiwa namba moja wa tuhuma za upotevu au kutoweka kwa baba yenu??Je, mmejaribu kuripiti Polisi kwamba Bw. Kilumile ndiye mhusika wa tukio la kupotea kwa baba yenu??
6.Baba yenu alikuwa na hisa kiasi gani kwenye umiliki wa hiyo kampuni ambayo sasa ipo chini ya usimamizi wa Bw. Kilumile??
7.Je, nyinyi kama watoto mlichukua hatua gani ktk kujihusisha na kampuni hiyo aliyoiacha baba yenu mara tu baada ya baba yenu kutoweka ktk mazingira ya kutatanisha??

Bado Nina maswali mengi sana kuhusu hili suala lenu, isipokuwa muda wa kuandika hapa sina wa kutosha ili kuweza ku-deal ipasavyo na hili tukio.
 
Poleni sana jirani,binafsi namfaham mzee(aliyepotea).Pia n jirani yenu.Natanguliza pole.

Si nilisikia baba alikua n mmoja wa watu waliokua wanadai sirikali! Au ulikua ni uzushi tu?

Na inasemekana ndo chanzo cha kupotea kwake maana kwa hali ya kawaida labda uwe mafia yani umpoteze mtu na gari yake pia isije kuonekana milele na huyo mtu unayempoteza sio mtu ww mchezo mchezo.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom