Sweta la baba yangu lenye historia ya maisha yangu

Ivan Stepanov

JF-Expert Member
Apr 22, 2023
4,894
15,962
Nimejiskia ku share hii sehemu ndogo ya maisha yangu ambayo sikua naijua kiundani mpaka hivi juzi kati.

Twende pamoja.

Nilifiwa na mama angu mzazi nikiwa darasa la kwanza 1997.

Sikua naishi nae maana mama alikua mchepuko tu kwa mzee hivyo walishindwana mapema baada ya mimi kuzaliwa.

Siku moja walipotofautiana, (mzee alinisimulia) mama kwa hasira akamwambia mzee "chukua kitoto chako sitaki kukiona" 😂😂😂 halaf mama akasepa ndani. Mzee akangojaaa mpaka usiku sana mama hakurudi.

Nilikua na miezi mi 3 tu muda huo na tulikua tunaishi mkoa mmoja hapo nyanda za juu kusini magharibi.
Baba akanibeba (sikua na nguo mwilini) akanitia ndani ya sweta alilokua amevaa, akasepa na mimi (hili sweta lake analitunzaga mpaka leo for that memory na ndio lili trigger hii story yotee akanisimulia).

Kituo cha kwanza ilikua ni police station central. Akafika akatoa taarifa kuwa amesusiwa mtoto na mama mtoto hivyo amemchukua kwakua hajui mama yake kaenda wapi na hawaishi pamoja maana yeye mzee ameoa na anaishi na mkewe.Akaandika maelezo na polisi wakauliza mtoto yuko wapi?, mzee akabinjua sweta akanitoa kuwaonyesha.Walishtuka na kushangaa sana ila wakampa go ahead akaondoka na mimi.

Mzee alitumia akil sana maana alikua anajua maza lazima angekuja kutoa taarifa polisi (mama angu alikua wa enzi hizo, a banker, mtata sana mtu wa bukoba na mzee wangu yeye darasa la 7 tu sema akil mtu wangu za maisha na kujiamin bas).

Na kwel usiku sana, baada ya hasira kupungua (nahis), mama akili zikamrudia na hatua aliyochukua ilikua ni kufika polisi akatoa taarifa ya kupotelewa na mtoto, askari kwakua tayar walikua na taarifa ya mzee wakaunga dots wakajua huyo mama mzazi ndio huyu, wakampa vipande vyakee wakamsema sana kuwa ni mzaz gan mwanamke anakua katili kias hicho kisha wakamtimua bila msaada.(hapa polisi walimuonea sana)

Mzee wangu alikua ameoa na mke wa mzee pia alikua ana mtoto mchanga wa umri wangu ambaye tumetofautiana mwezi mmoja tu kuzaliwa.Yaani wakat mimi nazaliwa, mke wa mzee alikua amejifungua mwezi mmoja uliopita.

Mzee alipofika nyumbani, ikamlazimu kuniacha kwanza kwenye gari, akaingia ndani na kumueleza kila kitu mama mkubwa(mke wake),

Mama (mkubwa) akauliza "yuko wapi mtoto sasa?" Mzee akasema yuko kwenye gari.
Usisahau hapo nilikua na miezi mitatu (3) tuuuu.

Kwa mujibu wa maelezo ya mzee, huyu mama alinionea huruma sana (ofcz hakunieleza kuhusu alimalizana vipi na kesi yake ya kuzaa nje).

Basi huo ukawa mwanzo wa maisha yangu mapya kwenye makazi mapya na mzazi mpya ambaye akachukua jukumu la kunilea na kuninyonyesha mimi na mwenzagu(wa kiume pia). Akatulea watoto wachanga wawili pamoja na wengi wasitujua family yetu kiundani mpaka leo hii wanajuaga sisi tulizaliwa mapacha.
kwakua mzee financially alikua vizur tuu bas haikua kaz nzito ku provide in compensation to changes occured both kwangu na mama zaid ambaye jukumu la malez lime shift overnight toka kuwa na mtoto mmoja mchanga mpaka kuwa na mapacha

Kwa upande wa mama mzazi mgogoro ulikua mkubwa sana, lakin mwisho wa siku mzee alifanya fitna sana kias kwamba mama mzazi hakuweza kunichukua.Mzee kidogo alikuwa alwatani mjini na alikua akifahamiana sana na wakuu wa vyombo vya usalama hivyo mama alikua at disadvantage na issue ikamshinda na mahusiano yao yakafia hapo na mzee.

Mzee wangu ni type zile za akina baba wa zamani ambaye kwake mwanamke hapaswi kumleta dharau so akasema kitendo mama kumuachia mtoto mchanga usiku alikitafsiri kama dharau iliyopitiliza na akajipa 2 hours kusubiri kabla haja amua uamuzi mgumu.2 hours alizongoja na mama angu hajarudi basi akapitisha azimio kuwa hatakaa anipate tena (mimi) maishani.

Mama nae aka susa kabisaaa kwa habar ya ishu zinazonihusi mimi na akahama kikazi kuja jijin dar ambako aliolewa na mwanaume mwingine.Mama angu naye alikua mtata sana plus usomi hakutaka kuleta unyonge akapiga chini mtoto na baba yake 😂😂😂

The vulnerable being there nikabaki kuwa mimi.Anyways ndio maisha

Mpaka nafunga mwaka mmoja ndio angalau uvumilivu ukamshinda ikabidi aanze kuwa anakuja nyumbani kwa mama angu mpya sasa mara moja moja akipata nafasi kuja kunijulia hali.

Mama pamoja na mama angu mzazi kama wanawake walitokea kuelewana sana ofcz ikiwa kama mama kuonyesha gratitude na shukrani kwa namna ambavyo mama (mpya) alibeba jukumu ambalo haku stahili.

So akawa anakuja kutu visit mara moja moja akipata likizo na ikafikia hatua akawa anatuchukua (mimi na pcha wangu) kuja dar tukiwa tumefikisha about 4 years..Tutakaa kisha ataturudisha..ikawa hivyo yan na maisha yakaendelea.

Infact, malezi ya mama angu(mpya) ndio yaliteka na kuujenga mfumo mzima wa mtazamo kias kwamba linapotajwa neno mama basi anaye kuja akilin mwangu wa kwanza ni huyu mama angu.Na sio mama mzazi.
Na hii ni mpaka leo nikiwa na utu uzima huu.

Sijawah ku experience ile concept ya MAMA WA KAMBO kabisaaa maisha yangu yote.Nampenda sana na mzee wangu huwa linampa raha sana hilo mpaka kesho.

Mama mzaz akiwa kwenye ndoa yake akazaa mtoto wake wa kike (mdogo angu). Lakin alikuja kufariki kwaajil ya uzazi akijifungua mtoto mwingine.

Na hiki kipindi sasa nilikia na 6 years nkkiwa Darasa la kwanza.

Sikuwahi kuhis pengo lolote kwenye maisha yangu kwa kuondokea naye mama mzazi.Ukichanganya na ile hali ya utoto, sikumbuki kujiskia uchungu ila nakumbuka nililia sanaa msibani kwakua nilimuona baba angu analia.

Halafu ile kati kat ya watu wengi na sikua najua kuhusu misiba basi kumuona mzee analia niliogopa sana nikamkubatia mzee huku nalia sana namwambia "baba turud nyumbani, baba turudi nyumbani".(hii image mpaka leo haijawahi kunitoka).
Tulipomaliza nikarud mkoa kuendelea na maisha.

Nilipoteza kabisaa connection na family upande wa mama angu, hata mdogo angu wa kike tuliye share tumbo moja aliyeachwa akiwa na 1 years hatukuwah onana tena from 1997 kakiwa katoto sana.

Kaka zangu na dada zangu upande wa baba na mama angu (mpya) hao ndio kwangu ndugu zangu mpaka kesho. Ni kama wao ndio tumezaliwa tumbo moja.But ofcz they are my blood.

2009 nikiwa kidato cha sita ndio kwa mara ya kwanza napokea simu namba ngeni toka kwa mdogo angu ambaye muda huo walkua wameshaondoka jijin miaka mingi kurudi kanda ya ziwa.Alikua kidato cha pil kipindi hicho yeye.

Ndio muunganiko wetu ukarudi tena hapo ila hatukuwah kuonana still.Mpaka anamaliza sekondary akaamua kutoendelea na shule akaolewa mkoa mmoja hapo kanda ya kaskazini.

2015 kwa mara ya kwanza nikafika kumtafuta nimuone baada ya miaka mingi kupita tokea 1997.
NIkamkuta ana mtoto mmoja wa kike na siku nafika ndio siku huyu mwanaa anaanza kutembea, yani ile kuniona tu na hakanijui, ile furaha kakaanza kuoiga hatua na kutembea rasmi( odcz alikua kwenye hatua za kuanza kutembea ila ikawa coisedense siku nafika ndio sasa rasmi na yeye anatembea bila kujishikilia mahala).

Dada yangu( mdogo angu) akashangaa sana na akafurahi sana pia kwa wakat mmoja what is happening.

Honestly nilimkuta yuko kwenye hali mbaya sana ..kachoka!! Maisha duni, dah niliumia sana nikachukua hatua.

IKAWA MWANZO MPYA.
Lakin yote haya nilipata kusimuliwa baada ya kumuuliza mzee kuhusu sweta lake ambalo mpaka juz kati bado analo analitunza chumbani kwake.Nilimuuliza kuhusu sweta hili kwakua kwenye picha nyingi za ujana wake nililiona amelivaa kwenye occassion mbali mbali lakin katika vyooote vya ujana wake kwanini amelitunza sana sweta hilo na hali halimtoshi wala halitumii???

BASI NDIO CHANZO CHA MZEE KUNIPA HABAR HII YOTE YA YEYE NA MCHEPUKO WAKE (mama yangu mzazi).

Mwisho
 
Hongera kwa huyo mama aliekulea kiasi aujihisi Kama ni mama wako wakambo, wanawake wa dizaini hiyo hakuna katika kizazi Cha Sasa ni kumi kwa moja.
Uko sahihi ingawa hili nahisi lilitegemea zaid nafas za wanaume kwenye family zao.Ujue zaman wazee wetu walikua completely provider when it comes to home affairs so ni rahis mwanamke kuwa submissive na maamuz yako kama mwanaume yanakua powerful.

Ila kwasasa tuna share sana majukumu na hawa wanawale wetu ndani ya nyumba kias kwamba u find urslef limited when it come to final says
 
Kabisaa madingi wa kitambo walikua vyuma "kweri kweri".
hata sijui tulifeli wapi sisi kuweza kudindishiwa na wanawake katika kizazi chetu. Sikumbuki kumuona mama yangu ama mwanamke yeyote yule akithubutu kubishana na mzee wangu mpaka kufa kwake.

Anyways jichukulie ni mwenyewe bahati mno kupata mama aliekukubali na kukulea kama mwanae. Kama ulivyosema kuwa unamchukulia kama mama yako na hivyo ndivyo ilivyo, huyo ndio mama yako hasa.

Kwa uandishi wako ni dhahiri mzee na mama yako mlezi walifanya kazi nzuri mno katika kukulea. Be blessed.
 
hata sijui tulifeli wapi sisi kuweza kudindishiwa na wanawake katika kizazi chetu. Sikumbuki kumuona mama yangu ama mwanamke yeyote yule akithubutu kubishana na mzee wangu mpaka kufa kwake.

Anyways jichukulie ni mwenyewe bahati mno kupata mama aliekukubali na kukulea kama mwanae. Kama ulivyosema kuwa unamchukulia kama mama yako na hivyo ndivyo ilivyo, huyo ndio mama yako hasa.

Kwa uandishi wako ni dhahiri mzee na mama yako mlezi walifanya kazi nzuri mno katika kukulea. Be blessed.
Thanks chief.Pamoja sana
 
Wanaume wa sasa tumepoteza ujasiri kwa kushea majukumu ya familia n wake zetu na utandawazi huu kwa wanawake wanautumia vibaya katika familia.
Angalia cku hz kuna siku ya single mothers na vikoba na bank za wanawake. Yooote haya ndio yanayo mpatia options nyingine.
Leo hii TV na maredioni kuna vipindi vingi vya kike kama WANAWAKE LIVE,Dadaz na n.k ukisikiliza shekh wangu unaona kabisa wanatiana ujinga mwingi kuhusu wanaume na familia kwa ujumla.
Achana na magroup ya whats up kuhusu kujipatia maamuzi
 
Wazee wetu walikua na misimamo na wakina mama pia walipata malezi Bora ya ndoa,ndoa ilikua kitu Cha thamani sio Sasa ndoa fashion uliemuoa tayari ashapitiwa na wazee umri wa babako mwanamke dizaini hiyo awezi kukuheshimu.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom