Mohamed Said
JF-Expert Member
- Nov 2, 2008
- 20,912
- 30,254
UBISHI MKUBWA: DUKA LA MAFUTA YA TAA LA MAMA MARIA LILIUZA MAFUTA YA TAA AU MAFUTA YA TAA NA COCA-COLA?
Pamekuwa na ubishi mkubwa kuhusu duka la mafuta ya taa la Mama Maria Nyerere katika moja ya mitandao ya kijamii kuhusu duka la mafuta ya taa la Mama Maria Nyerere.
Ubishi uko katika bidhaa.
Mama Maria duka lake aliuza mafuta ya taa peke yake au na bidhaa nyingine?
Chanzo ni makala ya Mama Maria kufikisha miaka 93.
Katika makala hiyo mwandishi aliandika kuwa Mama Maria alikuwa na duka la kuuza mafuta ya taa Magomeni.
Mimi nikaandika kueleza kuwa duka hili lilianza Mtaa wa Mchikichi na Livingstone mwaka wa 1955 wakati huo Mwalimu Nyerere akiishi na Abdul Sykes.
Nikaendelea na kueleza kuwa hilio duka likahamia nyumbani kwa Ali Msham Mtaa wa Jaribu, Magomeni ambae alifungua tawi la TANU nyumbani kwake na akampatia sehemu Mama Maria kuweka duka lake la mafuta ya taa baada ya Mwalimu kuhamia Maduka Sita Magomeni.
Inaelekea wasomaji wengi hawakupoendezwa na historia hii na hapo ndipo mashambulizi dhidi yangu yakaanza.
Duka lilikuwa linauza mafuta ya taa peke yake au na Coca-Cola?
Sababu ya watu hawa kusema hivyo ni kuwa kuwa kulikuwa na bango linalotangaza soda hiyo katika picha niliyoweka.
Ubishi wa kuuza soda ulimalizika kiasi kwa mmoja wa jamaa zangu kuniletea taarifa kuwa duka la Mama Maria lilikuwa linauza pia na Coca-Cola na mtu aliyekuwa anapeleka soda hiyo hapo dukani anaitwa Amal Bafadhil.
Mashambulizi hayakuacha wako walioniita muongo nk. nk.
Nami nikawajibu kwa kusema kuwa mbona hili la soda na mafuta ya taa ni jambo dogo kwa nini hamuulizi Ali Msham alikuwa nani katika kupigania uhuru wa Tanganyika kiasi kwanza atoe nyumba yake kuwa tawi la TANU na kisha kutoa nafasi kwa Mama Maria kuweka duka lake la mafuta ya taa hapo kwake?
Nikawauliza kama wangependa kujua jina la kijana wa Ali Msham ambae yeye kila siku alikuwa akimsindikiza Mama Maria nyumbani kwake baada ya kufunga duka jioni Maghrib na kiza kishaingia?
Wakati huo kutoka Mtaa wa Jaribu kwenda Maduka Sita sehemu kubwa ilikuwa miembe na mikorosho hapakuwa na nyuma nyingi na taa za mtaani hakuna.
Niliuliza kama wangependa hata kujua historia ya mtoto huyu wa Ali Msham.
Wako kimya hadi leo.
Huyu mtoto wa Ali Msham jina lake ni Abdallah Omar Likonda sasa ni mzee lakini yu hai anaishi Mvuti, Chanika.
Abdallah Omar Likonda ana historia nzima ya nyakati zile.
Leo ni nimepita nyumbani kwa marehemu Ali Msham na kuangalia lilipokuwa duka la Mama Maria.
Nimepiga picha nyumba ambayo nimeelezwa imebadilka sana lakini walinionesha lilipokuwa duka la Mama Maria na wakanionyesha pia sehemu upande wa kulia wa nyumba ilipokuwa shule ya TAPA aliyofungua Ali Msham na upande wa kushoto kulipokuwa na nafasi kubwa ambayo ndipo TANU ilipokuwa ikifanya mikutano yake ya ndani.
Katikati ya hii nyumba mpaka leo bado iko fremu na ndipo lilipokuwa duka la mafuta ya taa la Mama Maria Nyerere.