Roving Journalist
JF Roving Journalist
- Apr 18, 2017
- 2,814
- 11,991
Mamlaka ya Huduma za Usambazaji wa Maji na Usafi wa Mazingira Dar es Salaam(DAWASA) imetoa agizo la kusitisha biashara ya usambazaji wa maji ya visima katika baadhi ya maeneo ya jiji la Dar es salaam ndani ya siku thelathini (30) kabla hatua kali za kisheria hazijachukuliwa kwa wahusika.
Agizo hili linatokana na kupanuka na kuongezeka kwa wigo wa miundombinu ya DAWASA katika kufikia wateja wengi ambao awali walikuwa hawawezi kupata huduma hii pamoja na ukiukwaji wa sheria ya huduma za usambazaji wa maji ya kisima kinyume cha Sheria ya huduma ya usambazaji maji na usafi wa mazingira Namba 5 ya mwaka 2019 ambapo imepiga marufuku mtu yoyote kujihusisha na usambazji wa maji isipokuwa mamlaka husika tu.
Oktoba 25, 2022, Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Amos Makalla alithibitisha uwepo wa upungufu mkubwa wa maji mto Ruvu, hivyo kuwataka wakazi wa jiji hilo wajiandae na mgao wa maji.
Kuhusu uwepo wa mgao wa maji kwenye jiji la Dar es salaam unaweza kusoma hapa: Rasmi Dar yakumbwa na uhaba wa Maji, RC Makalla athibitisha uwepo wa Mgao