DOKEZO DAWASA yatoa notisi ya kusitisha usambazaji wa maji ya Visima kwa baadhi ya Maeneo ya Jiji la Dar es salaam

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Apr 18, 2017
2,813
11,991
Mamlaka ya Huduma za Usambazaji wa Maji na Usafi wa Mazingira Dar es Salaam(DAWASA) imetoa agizo la kusitisha biashara ya usambazaji wa maji ya visima katika baadhi ya maeneo ya jiji la Dar es salaam ndani ya siku thelathini (30) kabla hatua kali za kisheria hazijachukuliwa kwa wahusika.

Agizo hili linatokana na kupanuka na kuongezeka kwa wigo wa miundombinu ya DAWASA katika kufikia wateja wengi ambao awali walikuwa hawawezi kupata huduma hii pamoja na ukiukwaji wa sheria ya huduma za usambazaji wa maji ya kisima kinyume cha Sheria ya huduma ya usambazaji maji na usafi wa mazingira Namba 5 ya mwaka 2019 ambapo imepiga marufuku mtu yoyote kujihusisha na usambazji wa maji isipokuwa mamlaka husika tu.

Oktoba 25, 2022, Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Amos Makalla alithibitisha uwepo wa upungufu mkubwa wa maji mto Ruvu, hivyo kuwataka wakazi wa jiji hilo wajiandae na mgao wa maji.

BB8E150B-D931-42E3-BC2A-F38317454899.jpeg



Kuhusu uwepo wa mgao wa maji kwenye jiji la Dar es salaam unaweza kusoma hapa: Rasmi Dar yakumbwa na uhaba wa Maji, RC Makalla athibitisha uwepo wa Mgao
 
Wasambazaji binafsi maji hayakatiki hata siku moja na bill zao rafiki kwa watumiaji

Katika mashirika mabovu nchi hii ni Tanesco, TTCL na Hizo mamlaka za maji

Soko lipo ila ukiritimba na kuvuta miguu

Mfano TTCL ilikuwa ndio kampuni pekee ya Simu

Mimi niliomba kufungiwa nilikaa Miaka mitatu bila kufungiwa zilizokuja simu za mkononi nilienda personally kwenda ku cancel ombi kuwa mizimu yao ya midway sitaki tena.

Dawasa jiji lote soko lilikuwa lao lakini kufungiwa shida na mirushwa kibao ubabaishaji mwingi.

Mimi bomba la Dawasa linapita mlangoni kwangu lakini niligoma kuunga natumia private supplier toka afunge maji hayajawahi kukatika.
 
Sheria za mwendakuzimu hizi. Inabidi bunge lifanye kazi ya ziada kuondoa hizi sheria zilizowekwa na awamu ya 5. Zilikuwa sheria za hovyo za kidikteta. DAWASA hawana makosa... wabunge waliotunga hiyo sheria na Rais aliyeisaini ndo wakulaumiwa.
 
Dah no speech, hata Moro ni hivi hivi kwa wenye bowser wanauza maji ya chumvi laini kwa vile mamlaka inatoa maji kidogo sana watu wananunua maji chumvi.
 
Hao wanataka tuwe kama babu wa Iran tusiwe tunaoga siyo, maji hayatoki wiki mbili mpaka tatu halafu upige marufuku wenye visima eti miundombinu imeimarika
 
Wasambazaji binafsi maji hayakatiki hata siku moja na bill zao rafiki kwa watumiaji

Katika mashirika mabovu nchi hii ni Tanesco,TTCL na Hizo mamlaka za maji

Soko lipo ila ukiritimba na kuvuta miguu

Mfano TTCL ilikuwa ndio kampuni.pekee ya Simu

Mimi.niliomba kufungiwa nilikaa Miaka mitatu bila kufungiwa zilizokuwa simu za mkononi nilienda personally kwenda ku cancel ombi kuwa mizimu yao.ya midway sitaki tena

Dawasa jiji lote soko lilikuwa lao lakini kufungiwa shida na mirushwa kibao ubabaishaji mwingi

Mimi bombs la Dawasa linapita mlangoni kwangu lakini niligoma kuunga natumia private supplier toka afunge.maji hayajawahi katika
Kwa jinsi hii nchi ilivyo na makandokando mengi, huwa nashangaa sana nikiona kiongozi amenenepa na ana tumbo kubwa.

Yani unapata wapi muda wa kunenepa? Watu wanakunywa na maji machafu, taasisi za Serikali zinaongoza kwa rushwa na utendaji mbovu lakini kiongozi ana nenepa? Na kitambi kinatoka? Shida na matatizo ya Wananchi ina maana hayakusumbui kabisa?
 
Coverage ni jambo Moja maana hiyo ni kulaza mabomba tu, ishue ni hayo maji je yatakuwemo kwenye hayo Mabomba ?
 
95% ya wakazi wa Kariakoo wanatumia maji ya visima
Maji ya dawasa hayakidhi hata 5%
 
Back
Top Bottom