DART Special Thread: Tunaomba Maoni Ushauri, Malalamiko, Pongezi na Mapendekezo kuhusu Mabasi ya Mwendokasi

wewe bongo yoyo yaan utoke kibaha mpaka gerezani kwa 750 iyo mwendokasi ya wapi au ya china, nauli ya kibaha mpaka kimara ni 700 utoke kimara mpaka gerezan ni 750 jumla 1450
Ndio ilivyo unalipa 750/- pale Kibaha na tiketi haichanwi unakuja kimara unaendelea na safari ama kwenda gerezani au kivukoni!!! Swali kwani huwezi safiri kwa bei hiyo kutoka kivukoni/gerezani kwenda kibaha? Fanya utafiti kabla ya kuropoka!!!
 
Ivi mna utaratibu wa mteja kununu tiketi kupitia simu yake ?
Utaratibu upo tena tunautangaza na kuusisitiza kila siku, ukiwa na simu janja (smart phone) iwe ya android ama ya mfumo wa IOS unaweza kupakua Mwendokasi app kisha ukishakuwa nayo kwenye simu yako ni rahisi kuitumia kwa kufuata maelekezo machache, kwa namna programu hiyo ionavyofanya kazi angalia matangazo kwenye tovuti yetu www.dart.go.tz pia kupitia katika tovuti hiyo unaweza kuingia katika mitandao yetu ya kijamii ambayo pia ina maelezo ya Mwendokasi app.
 
Hakuna mtu aliyekimbia tupo humu kwa saa 24 , ndiomaana tumeanzisha huu uzi kwa ajili ya kupata feedback ya namna mambo yetu yanavyokwenda.

Kama mko humu saa 24 kwa nini baadhi ya maswali hujibu?
Kuna maswali yapo kwenye comments zilizopita lakini hakuna majibu!
Vingine vinahitaji ufafanuzi lakini umekwepa why???
Na ulivyo hewa hata hii comment na ulichoulizwa utajifanya huoni!
Rudi nyuma pitia comment moja moja jibu kila inayohitaji majibu!!!
 
Asante kwa kuja.
Ni lini hayo mabasi mtayapeleka Mwanza pia ili wananchi wapate huduma ya usafiri..??
Sababu jiji la Mwanza limekua na tayari limechangamka na mkituletea hizo Bus zikaanzia route ya Kisesa, Igoma, Neshno, Buzuruga, Mabatini, Nata, Pepsi, Mkuyuni, Nyegezi, Buhongwa, Nyashishi hadi Usagara and Return.
Mwanza ipi unayoongelea wewe na zitapita wapi izo basi?Ngosha ukishashiba Sato ulale sio kuandika pumba
 
Hatutaki mkandarasi anayejenga mwendo kasi ya mbagala aje kujenga ya Tegeta, kwa sababu sipendezwi na spidi yake. Ni hilo tu.
 
Wekeni hayo mabasi yenu AIC maana madirisha Huwa madogo na watu wanakuwa wengi sana jambo ambalo ni hatari.
Hafu kingine kwanini mabasi yenu mengine hupita vituoni matupu bila kusimama au kuchukua abiria hamuoni mnafanya biashara kichaa
Aisee kweli kabisa,niliwahi shuka njiani kabla ya kufika nakoenda,nilikuwa nakosa hewa,nikaona Cha kufika nn, nikashuka!

Yanni mtu umesimama muda mrefu kituoni unaona gari hiloo linapita tupu,inakera sn
 
Kwa mujibu wa design tunatakiwa tuwe na basi kila baada ya dakika tano ,kwa sasa kwakua tuna upungufu wa mabasi ndiomaana hali haiko kama inavyotakiwa kuwa , lakini juhudi zinafanyika usiku na mchana na serikali yenu sikivu ya awamu ya tano kuhakikisha mabasi ya kutosha yanapatikana kwa awamu ya kwanza na awamu ya pili kule Mbagala ambayo iko katika hatua za mwisho za umalishaji.
Hili suala la upungufu wa mabasi siwaelewi kabisaaa, mabasi yamejaa yanrpaki tu getezani,kimara, kwanini?
 
Mkiwa active mtapata mengi sana. Ila msije mkaja na mambo ya wenzenu TANESCO ya kupewa changamoto walizonazo, wao badala ya kuhangaika na changamoto hizo, wanaanza mambo ya kutaka mtu aandike namba yake ya simu, anakoishi na jina lake kamili..!!!
Hahahaaa! Kumbe unaikumbuka hii ishu, yule mtanesco kakomaa kweli kutaka namba watu tunamueleza vingine ye hataki
 
Back
Top Bottom