CNN Report: UAE yapewa ardhi Afrika kufanya uwekezaji chechefu, watachuma mabilioni ya dola kutunza misitu ya nchi tano ikiwemo Tanzania

Taso

JF-Expert Member
Jun 12, 2010
2,463
2,289
Chanzo

Kuelekea mkutano wa mazingira wa dunia, COP28, utakaofanyika mwezi December 2023 huko Dubai, CNN imetoa ripoti maalum inayoilaumu UAE kwa kuendesha miradi chechefu ya kimazingira ikiwemo kukwapua ardhi ya Afrika ikijifanya kutunza mazingira wakati nia halisi ni kujikingia kifua wakati inaendelea na biashara ya mafuta kisukuku, fossil fuel, ambayo yanapigwa vita na dunia. Dunia maana yake makubaliano ya COP, ambayo ni mikutano ya UN mahususi kwa mazingira ya dunia.

UAE ni nchi ya sita kwa kuzalisha mafuta duniani, na inakabiliwa na deadline ya katazo la matumizi ya mafuta kisukuku kwa sababu za kimazingira na pia nguvu ya soko la nishati m-badala. Hivyo UAE wanakimbizana na muda kufaidika na mafuta na gesi yao na pia wanafanya harakati kubwa kuishawishi dunia iendelee kuvumilia matumizi ya mafuta kisukuku.

Mafuta hayo, ikiwemo gesi asilia, makaa ya mawe na petroleum yanaharibu mazingira kwa sababu yanatengeneza gesi ya CO₂
. Mwaka 2050 ndio mwaka ambao dunia imejiwekea iwe mwisho wa kuzalisha CO₂ kwa utaratibu kwamba hewa inayotengenezwa iwe sawa na inayoondolewa hewani, NET ZERO EMISSION. Misitu, ambayo hupumua CO₂ ni njia muhimu inayotegemewa katika kusafisha mazingira, Na misitu imejaa Afrika. Sasa dunia imekubaliana kwamba misitu inahitaji hela kuitunza kwa kuzuia kukatwa kwa miti, na Waarabu wameonyesha kwamba wana hela ya kuwekeza kwenye kutunza misitu.

Lakini kumbe pia ni biashara nzito. Mkutano wa COP28 wa December 2023 unaenda kuweka taratibu za kuuziana kitu kinaitwa carbon credits, ambazo ni kama points utakazopata kwa kusafisha mazingira, na zitauzwa kwenye soko la dunia kama zinavyouzwa forex, bitcoints, commodities au hisa.

Waarabu wa UAE wameingia mikataba kutunza misitu katika nchi tano za Afrika ikiwemo Tanzania. Wa-Emirati watatumia umiliki wa misitu hiyo kuuza hizo Carbon Credits. Dunia imekubaliana kwamba nchi na makampuni yanayoendelea kuharibu mazingira kwa biashara ya mafuta kisukuku zinapaswa kuonyesha kwamba wakati zinaharibu pia zinatengeneza, yani zinafanya carbon offset, na juhudi hizo zitapimwa kwa carbon credits. Na biashara ya kuuziana carbon credits CNN inasema itakuwa ni ya mabilioni ya dola, na Waemirati watavuna mabilioni. Ripoti pia imesema uwekezaji kwenye ardhi za Afrika husababisha wenyeji kupokwa ardhi na kuhamishwa kinguvu. Na pia hakuna uhakika wa kisayansi kama kweli kutunza misitu Afrika kutaboresha mazingira yatakaoendelea kuchafuliwa na nchi za mafuta, petrostates.

Katika biashara hiyo dunia haijali nani anamiliki carbon credits, amezipatia wapi, anachimba mafuta wapi, amesafisha mazingira wapi. Inachotaka dunia ni kwamba CO₂ kwenye hewa ya dunia ipungue. Ukiwa na msitu, au namna yoyote ya kuonyesha unatunza mazingira, ni hela. Waarabu na viongozi wa nchi hizi tano za Afrika wameona fursa.

My take:
Sasa hebu niambie, mwekezaji wa kutunza misitu! Mwarabu! Hivi ni taasisi gani hapa duniani ina nguvu kuliko TANAPA katika ku control mapande ya ardhi ya nchi ? Kwa nini tusiuze hizo carbon credits sisi wenyewe ? Kusema hatuwezi ni dhahiri serikali imesema uongo! Wanaweza. Na wanafanya, tena kwa mkono wa chuma. Haiyumkini waliposema tuwape wawekezaji control ya mali nyeti za nchi kwa sababu computer za TRA na TPA hazisomani pia ilikuwa uongo. Hii ni miradi ya viongozi wanaofaidika na nchi kuendelea kuuzwa kama pimpu anavyofaidika kuuza changudoa kwa bei sawa na bure.
 
Kuna taasisi moja huwa ina dili na Land Grabing in Afruca, ukisoma report zao unaweza usipate usingizi. Hata Tanzanua kuna Aridhi isha uzwa kuna nchi zinamilik Aridhi Tanzania sema haiwekwi wazi.
 
Back
Top Bottom