Roving Journalist
JF Roving Journalist
- Apr 18, 2017
- 2,812
- 11,989
Waziri wa Maliasili na Utalii, Angellah Kairuki amesema hayo wakati akitoa Hotuba katika Uzinduzi wa Mkakati wa Kitaifa wa Mianzi (Bambos) kwenye Ukumbi wa Mikutano wa Chuo Cha Utalii Dar es Salaam, leo Februari 19, 2024.
Amesema “Natambua kwa takwimu za sasa, Tanzania tunapoteza takribani eneo la misitu lenye ukubwa wa hekta 469,000 kila Mwaka.
“Hali hii si nzuri kwani kama juhudi za pamoja hazitachukuliwa basi kasi ya kuenea kwa jangwa zitaathiri Nchi yetu na hatimaye kuchangia kwenye kuathiri dunia katika siku za usoni. Hivyo, juhudi hizi za kuendeleza miti ya mianzi ni jambo la muhimu na la kila Mtanzania kuhakikisha kuwa misitu inaendelezwa na kuhifadhiwa kwa ajili ya manufaa ya kizazi cha sasa na kijacho.”
Ameongeza “Napenda kuwahimiza wadau wote wa Misitu kusoma kwa umakini Mkakati na Mpango Kazi wa Kitaifa wa Mianzi ili kupata picha ya tulipo sasa na kuhakikisha kuwa unatekelezwa ipasavyo ili kuendeleza misitu hapa Nchini.”
Aidha, ameto maelekezo kwa Chuo Cha Viwanda vya Misitu Moshi kwa kushirikiana na SIDO na wadau wengine washirikishwe kutafuta teknolojia za kisasa za kuchakata mazao ya mianzi ili kuyaongezea mnyororo wa thamani na kupata fedha nyingi kwa kuuza mazao hayo ndani na nje ya nchi.
Amesisitiza “Ninaielekeza Taasisi ya Utafiti wa Misitu kufanya tafiti za kutambua maeneo sahihi ya kupanda aina mbalimbali za mianzi pamoja na kuiagiza Idara ya Misitu na Nyuki ifanye tafsiri ya nyaraka hizi mbili kwa lugha ya Kiswahili na kuzisambaza. Serikali itaweka mazingira wezeshi kwa wadau wote wa zao la mianzi ili kuhakikisha linaleta tija kwa Watanzania na Taifa kwa ujumla.”