Changamoto 17 za Uwekezaji kwenye Ardhi na Majengo hapa Tanzania

Aliko Musa

Senior Member
Aug 25, 2018
156
240
Zipo changamoto nyingi za uwekezaji kwenye ardhi na majengo. Leo ninakushirikisha baadhi ya changamoto ambazo nimeziona zinaweza kukuzuia kutoka hapo ulipo kwenda hatua nyingine ya mafanikio.

MOJA.

Upatikanaji wa hati ya umiliki wa ardhi.

Hii ni sababu kubwa ya wawekezaji wengi kukosa sifa za kupata mitaji fedha kutoka kwenye vyanzo mbalimbali vya mitaji fedha.

Kwa mazingira yetu ya Tanzania, kupewa hati ya hakimiliki ya ardhi imekuwa ni changamoto kubwa mno. Changamoto hii inatakiwa kutafutiwa suluhisho na serikali yetu.

Ingawa kuna baadhi ya wananchi wanachangia kutopata hati ya hakimiliki ya ardhi kutokana na uelewa wa mwekezaji husika.

Suluhisho; kuwepo na ongezeko kubwa la makampuni ya kufuatilia utolewaji wa hati ya ardhi kutoka wizarani. Pili, serikali iweke mkazo kwenye kupunguza wanaohitaji rushwa kwenye mchakato wa kufuatilia hati ya viwanja au mashamba yao.

MBILI.

Upatikanaji wa mikopo ya majengo.

Mpaka sasa sijawahi kukutana na benki ambayo hutoa mikopo ya majengo. Bali hutoa mikopo ambayo huambatanishwa na huduma za utumishi wa umma na biashara halali za waombaji wa mikopo.

Kwa maana hiyo, ili uweze kupewa mkopo majengo ni lazima uwe na sifa mbili;-

✓ Uwe mtumishi wa umma au sekta binafsi.

✓ Uwe na biashara iliyosajiliwa na imeonyesha historia ya kutengeneza faida kwa kipindi elekezi.

Pia, inawezekana kupewa mkopo kwa watu wasio na sifa kama za hapo juu endapo wanataka kununua nyumba za kupangisha ambazo zipo kwenye soko imara la nyumba za kupangisha. Hii ndiyo huitwa mikopo ya majengo.

Hati miliki ya kimila ina nguvu sawa kisheria sawa na ile ya hati miliki ya kiserikali. Lakini hakuna mpango maalumu wa kutofautisha ardhi inayoruhusiwa kumilikiwa na wananchi kwa shughuli mbalimbali.

Mfano; unaweza kununua ardhi na ukapewa hati ya mkataba wa mauziano, wakati huohuo ardhi hiyo haina sifa ya kumilikiwa na raia.

Changamoto hii huwafanya watoa mikopo ya majengo kuweka ugumu sana kukubali matumizi ya hati ya mkataba wa mauziano.

Hii huwafanya wawekezaji kwenye viwanja na nyumba kukosa sifa za kutumia viwanja na nyumba zao ipasavyo.

Hii huathiri moja kwa moja jinsi mtaji fedha unavyopatikana. Wawekezaji wengi hujikuta kwenye shimo la kina kirefu mno baada ya kumiliki nyumba ambayo haina cheti cha hati miliki kutoka wizarani.

Wawekezaji wangeweza kutumia mikopo ya majengo kunasua mtaji fedha unaoshikiliwa na viwanja na nyumba wanazomiliki. Hivyo huishia kukusanya kiasi kidogo cha kodi kutoka katika nyumba moja au mbili za kupangisha.

Hatimaye hushindwa kabisa kufikia uhuru wa kifedha au huchelewa kufikia uhuru wa kifedha.

Kutokuwepo kwa kampuni nyingi za kutoa mikopo ya ardhi na majengo hupelekea kupungua kwa ushindani kati ya kampuni za mikopo na kampuni nyingine.

TATU.

Uwepo wa chombo cha nyumba na makazi.

Tanzania hatuna chombo kimoja ambacho kinashughulikia changamoto za ardhi na nyumba hasa majengo ya kupangisha.

Hivyo kumekuwepo na mnyororo wa changamoto za wapangaji, wenye nyumba na wasimamizi wa nyumba bila kuisha.

Suluhisho; Tungeunda chombo kimoja kwa ajili ya kushughulikia mambo ya umiliki wa ardhi na majengo kama vyombo vingine vya umeme (TANESCO), rushwa (TAKUKURU), na kadhalika.

NNE.

Maarifa sahihi ya kuwekeza kwenye ardhi na majengo.

Kundi kubwa sana la wamiliki wa ardhi na majengo hawafahamu kipi kinatakiwa kufanywa kwa wakati gani na kwa namna gani.

Wawekezaji wengi hawawezi kutambua mizunguko ya masoko ya bei za ardhi na majengo katika halmshauri wanapowekeza. Hii hupelekea kuwekeza kwa kubahatisha tu.

Pia, wapo wamiliki ambao wanamiliki nyumba za kupangisha ambazo haziwezi kutengeneza faida au kipato endelevu cha kuwafanya wawe matajiri.

Wamiliki hao wa nyumba hushindwa kutengeneza fedha kutoka kwenye nyumba zao za kupangisha kwa sababu mbalimbali.

Lakini sababu kuu ya kushindwa kwao ni kukosa maarifa sahihi ya jinsi ya kuwekeza kwenye majengo ya kupangisha kwa manufaa makubwa ya kifedha.

Mimi Aliko Musa ni mshauri mbobezi kwenye uwekezaji wa ardhi na majengo. Ukiwa na mimi tutashirikiana na wewe kuhakikisha unamiliki nyumba za kupangisha zenye kuingiza kiasi kikubwa cha kodi ya upangishaji kila mwezi.

Nimeanzisha programu iitwayo DISTRICT REAL ESTATE WORKSHOP. Hii ni programu ambayo inahusu uchambuzi wa kina katika wilaya moja tu. Ni programu ambayo ninakushirikisha fursa moja kwa undani zaidi na ni wapi panafaa kutengeneza fedha katika wilaya husika.

Programu inafanyika kwenye makundi yangu yote ya whatsapp kwa kila siku za jumapili. Jumapili hii (03-Disemba-2023) tuna programu inahusu kumiliki majengo ya chekechea (Daycare Centers) katika wilaya ya Morogoro Mjini.

TANO.

Chama cha wamiliki wa ardhi na majengo.

Kwanini tusiwe na chama cha wamiliki wa nyumba hasa nyumba za kupangisha. Chama hiki ambacho kitakuwa ni msaada kwa wamiliki wengi wa nyumba kuhusu changamoto ndogondogo za uwekezaji kwenye ardhi na majengo.

Chama ambacho wamiliki watakutana kubadilishana uzoefu, maarifa, hamasa na taarifa sahihi kuhusu mambo ya msingi ya uwekezaji kwenye majengo.

Pia, chama hiki kitakuwa ni daraja zuri kupitishia taarifa sahihi na maarifa sahihi kutoka vyombo mbalimbali ikiwemo serikali za mitaa na wizara mbalimbali.

SITA.

Kukosa sehemu ya kutunza taarifa za madalali wa ardhi na majengo.

Kwa kawaida taarifa za madalali wote waliosajiliwa zinatakiwa kutunzwa kwenye tovuti moja ambayo itakuwa ni sababu mojawapo ya kuongeza ubora huduma za udalali kwenye ardhi na majengo.

Kutokuwepo kwa tovuti au mfumo maalumu wa kutunza taarifa za madalali wote ambazo zitakuwa zinaonekana na umma imekuwa ni sababu mojawapo ya kuwa na madalali wanaotoa huduma za hovyo sana.

SABA.

Kukosa sehemu ya kutunza na kupata taarifa za wakaguzi na wathaminishaji wa ardhi na majengo.

Moja ya ubobezi muhimu sana kwenye uwekezaji wa ardhi na majengo ni ukaguzi wa ardhi na majengo. Ukaguzi wa ardhi na majengo ni hatua muhimu sana kabla ya kununua na kuuza nyumba au ardhi yako.

Ingesaidia sana endapo tungetengeneza sehemu ya kuweka taarifa za wakaguzi wa nyumba. Bila kuandaa taarifa/ripoti bora za ukaguzi majengo ni vigumu sana kuwa na picha kamili ya hali ya uwekezaji wako.

NANE.

Kuwa na kampuni chache za huduma za mikopo migumu.

Mikopo migumu ni moja ya mikopo inayosaidia sana kwenye baadhi ya mbinu za kuwekeza kama vile kununua na kuuza majengo ndani ya miaka miwili, kununua nyumba kwa njia ya minada ya hadhara na kadhalika.

TISA.

Kukosa kampuni za washauri wabobezi kwenye ardhi na majengo.

Hivyo wawekezaji kwenye ardhi na majengo kukosa sehemu ambapo wanaweza kupata huduma za ukocha na ushauri wa uwekezaji wao.

Washauri wengi kwenye eneo hili wameweka nguvu kwenye kumiliki viwanja au nyumba za kuishi. Na huishia kuwaambia wateja wao kuwa hapa itakuwa ni fursa kubwa sana kwa baadaye.

Kuna washauri wachache sana ambao wamejikita kwenye kutengeneza au kutunza utajiri kupitia ardhi na majengo.

KUMI.

Kukosa chombo cha kuandika ripoti na taarifa zote zinazohusu ardhi na majengo.

Taarifa muenendo wa masoko ya ardhi na majengo katika mikoa tofauti tofauti, taarifa za upatikanaji wa ardhi katika mikoa tofauti tofauti na taarifa nyingenezo.

KUMI NA MOJA.

Mgogoro kati ya mwekezaji na serikali.

Wawekezaji kwenye majengo ya kupangisha huweza kuingia kwenye mgogoro mkubwa kati ya serikali na wao wenyewe. Hii inaweza kusababisha na sababu tofauti tofauti za umiliki wa ardhi.

Mfano wa kwanza.

Mwekezaji anaweza kununua kiwanja kutoka kwenye serikali za mtaa akapewa hati ya mkataba wa mauziano tu.

Baada ya hapo akaenda kuihakiki kwa wakili au mwanasheria wa wilaya. Lakini mwisho wa siku wanakuja kumwambia nyumba uliyojenga ipo ndani ya hifadhi ya serikali.

Mwekezaji anaambiwa wananchi wa mwanzo kuishi hapa walikaidi agizo la serikali la kuondoka eneo hili ili lisitumike kama makazi ya watu.

Mfano wa pili.

Mwekezaji ananunua kiwanja na kujenga nyumba za kupangisha. Baada ya miaka miwili unakuja wito wa kumuondoa na kumuambia abomoe nyumba yake kwa sababu amejenga nyumba kwenye viwanja vya matumizi ya majengo ya viwanda.

Mwekezaji huyu, pia, anaambiwa wananchi wa mwanzo kuanza kuishi eneo hilo walihimizwa kutojenga eneo hilo lakini wakakaidi. Na taarifa hiyo wanapewa wananchi baada ya miaka kumi kumi au pengine zaidi ya miaka hiyo.

Mwekezaji anajenga nyumba karibu na barabara. Kiukweli ni makosa kujenga nyumba kwenye hifadhi ya barabara. Lakini mamlaka husika wanaweza kukaa kimya bila kuandika alama ya bomoa kabla nyumba haijakamilika.

Hivyo mwekezaji huumia kwa sababu ya kukosa maarifa sahihi ya uwekezaji kwenye ardhi na nyumba kuhusu umiliki wa ardhi na nyumba.

KUMI NA MBILI.

Kulipwa fidia.

Mwekezaji anaweza kuendeleza nyumba ambayo imeandikwa taarifa ya kulipwa fidia. Hii inaweza kutokana na kushindwa kuwa na subira kwa mwekezaji husika.

Lakini hii ya kufanya maendelezo kwenye nyumba ambayo imethaminishwa kwa ajili ya fidia ni kosa. Inaweza kupelekea mwekezaji kukosa sifa ya kulipwa fidia ya nyumba yake.

Mambo yote haya huhusiana na umiliki wa ardhi. Kupoteza sifa ya kupata fidia kwa sababu za kisheria ambazo zingeweza kuepukika ni jambo linalo mfanya mwekezaji ashindwe kufikia malengo yake.

KUMI NA TATU.

Kodi ya majengo.

Wawekezaji hawafahamu uwiano sahihi ya kulipia kodi ya majengo serikalini na thamani za majengo yao.

Hii hupelekea kutopata manufaa ya kifedha kwa wawekezaji husika. Badala ya kupangisha nyumba kwa kufanya tathmini ya jumla ya kodi ya majengo serikalini. Mwekezaji hufanya yote haya pasipokuwa na utaratibu wowote.

Kwa hivi karibuni kodi ya jengo imeongezeka hadi asilimia 50 ya kodi ya mwanzo. Majengo ya kulipia 1,000 kila za
Kama wawekezaji wangejifunza kuhusu sheAAZiria za umiliki wa ardhi kabla ya №wazee nyumba za kupangisha migogoro mingi ingepungua.

KUMI NA TANO.

Kukosa nguvu ya kisiasa yenye matokeo chanya kwenye uwekezaji huu.

Historia ya uongozi kwenye majimbo ya ubunge inaonyesha kubwa majimbo ambayo walishikiliwa na wabunge kutoka upinzani yalipata huduma muhimu kwa tabu mno. Mfano ni jimbo la Ubunge la Mbeya Jiji ambayo ilikuwa chini ya chama kisichotawala ngazi ya uraisi.

Kwenye uwekezaji wa ardhi na majengo, nguvu ya kisiasa ina matokeo ya moja kwa moja.

Kumi Na Sita.

Kukosa nguvu ya kiuchumi yenye matokeo chanya.

Moja ya kitu kingine ambacho kinakwamisha wawekezaji kwenye ardhi na majengo ni;-

✓ Kuchelewa kutekelezwa kwa miradi mikubwa yenye kuleta mageuzi ya kiuchumi katika wilaya husika. Mfano; ujenzi wa bwawa la umeme.

✓ Kufa kwa viwanda vyenye matokeo chanya kwenye thamani ya ardhi katika wilaya husika. Mfano; ni kiwanda cha ngozi cha mkoani Morogoro kiitwacho Tanzania Leather Goods Ltd hakifanyi kazi mpaka sasa.

Kumi na saba.

Kukosa usanifu kwa kiutaalam wa miji mbalimbali hapa Tanzania.

Miji mingi imejengwa bila mpangilio maalumu. Miji isiyo na mpangilio mzuri inakuwa haina thamani kubwa ukilinganisha na miji ambayo ina mpangilio mzuri wa majengo yake na miundombinu yake.

Miji ambayo haina mvuto hupelekea ardhi yake na majengo yake kutokuwa na thamani. Hii hupelekea ardhi hiyo kukosa soko kwenye taasisi mbalimbali ikiwemo vyanzo vya mitaji fedha. Lakini wasomi tunao na wanahitamu kila mwaka. Na wengine wameajiriwa katika halmshauri zetu bila kuonyesha matokeo ya ajira zao japo kwa sehemu ndogo.

Rafiki yako,

Aliko Musa.

Mbobezi majengo.

MUHIMU; Jiunge BURE na kundi la whatsapp liitwalo TZ REAL ESTATE TEAM. Ukiwa hapa utapata masomo na mijadala kuhusu uwekezaji kwenye ardhi na majengo (real estate investment).

Whatsapp; +255 752 413 711
 
Back
Top Bottom