Wazee, imekuja kama surprise kwangu hadi sijaamini masikio yangu na nikabaki na maswali kibao.
Asubuhi nilikuwa nasikiliza Power Breakfast so ikafika point hawa kina Masoud wakawa wanajadili ishu za Fiesta hasa viingilio. Kusema kweli imeniacha na mshtuko mkubwa sana hadi nimebaki najiuliza sababu ya kufanya Fiesta iwe cheap hivyo nini. Wanaogopa au wamefeli au wanawajali watanzania??
Imagine mtu atapata ticket hadi kwa buku 3. Very cheap, ndiyo. Lakini naamini sio bei walioweka kwa kupenda kwao, itakuwa ni tathmini walioifanya wakahisi wanavyojua wao. Hio sababu ya kuwa ni kura na mapendekezo ya watu naona ni porojo tu. Yaani wabongo tungepewa nafasi ya kuamua kiingilio, si wengi tungesema iwe bure.
Btw, V.I.P ni 20k. Ukilipia getini kwa kawaida ni 5k na kwa Tigo Pesa ni 3k tu. Levoz beibiii!