Chenge ajiuzulu!

Chenge ajiuzulu!

It is easy to criticise. Nauliza je ni nani angefaa kwa mawazo yako?

...........wagombea wote wawili walioingia tatu bora na msanii kikwete walikuwa maili mia far much better kuliko kikwete..sema basi tu wananchi wote walikuwa as if wamefuniikwa tambara la kaniki machoni na huyu kinyamkera...ndio wanazinduka leo...lakini wachunguzi wa mambo ya kisiasa tangu mwanzo na hadi leo tunasema kama tulivyosema hata kabla ya haya!!!
 
Mimi nampongeza kwa hatua aliyochukua.Pia nitampa hongera zaidi kama ataamua kuwatumikia wananchi wa jimbo lake kwa heshima na kuwarudishia heshima kubwa waliyompa na kumchagua kuwa mbunge.Namaanisha AJIUZULU NA UBUNGE.Hakuna heshima kubwa kwa wananchi wako kama hiyo.Umeonyuesha dhamira ya dhati kabisa kwa kuanza na uwaziri ambapo ulikua ni tunda la ubunge.

Ukikaidi kujiuzulu ubunge ni sawa na kuwadhalilisha wapiga kura wako kana kwamba wao wanaufurahia ufisadi
 
Game Theory hebu njoo utueleze habari za Dola milioni 15 na sio 1.
manake sasa hiyo inaweza kuitwa hatari kubwa!

wazungu watatizama na accounts za mkewe na watoto.

chenge hali imemkalia vibaya kwa vile tu umepita mkono wa mzungu ila kwa JK tu alikuwa yupo tayari kumkumbatia na kutudanganya kuwa ni mti safi
 
...........wagombea wote wawili walioingia tatu bora na msanii kikwete walikuwa maili mia far much better kuliko kikwete..sema basi tu wananchi wote walikuwa as if wamefuniikwa tambara la kaniki machoni na huyu kinyamkera...ndio wanazinduka leo...lakini wachunguzi wa mambo ya kisiasa tangu mwanzo na hadi leo tunasema kama tulivyosema hata kabla ya haya!!!

Ama kweli kakuboa kupita kiasi! Mimi pia JK ananichefua lakini hii mzee ni zaidi ya kipimo!
 
Hapo si ajabu Kikwete na genge lake la mafisadi wanawalaani kimoyomoyo hao SFO kwa kuwaharibia mlo, maana wananchi wamepiga kelele weee lakini wapi...mzungu kuibuka kuulizia tu akaunti vipi ndio wanatapatapa... kwa mwendo huu Dr. Watson tutakuwa tunamlaumu bure!
 
...........wagombea wote wawili walioingia tatu bora na msanii kikwete walikuwa maili mia far much better kuliko kikwete..sema basi tu wananchi wote walikuwa as if wamefuniikwa tambara la kaniki machoni na huyu kinyamkera...ndio wanazinduka leo...lakini wachunguzi wa mambo ya kisiasa tangu mwanzo na hadi leo tunasema kama tulivyosema hata kabla ya haya!!!

..kwa hili la haya yanayofumuka,nadhani bora hata huyu JK!

..kimsingi,hata angekuwa nani kuti la mwaka 2005 lilikuwa lishakauka linangoja kuanguka tu. na waliolikausha tunawafahamu!

..sasa hawa wengine wangetuletea tafrani tu. wangekataa na kufanya mbinu nyingi mambo yaonekane sawa wakati ni mabovu.

..in any way one sees it,JK has been the best thing for tanzania!

..na bado! mwaka haujaisha huu!
 
Jamani hatuna Rais yaani haoni kama Mawaziri wake ni mafisadi na hawezi kuwaondoa katika nyadhifa hadi wajiuzulu wenyewe.Hichi ni kipimo cha kuwa serikali yake ni bomu kuliko serikali zote zilizopita kwa idadi ya Mawaziri waliojiuzulu kwa kipindi cha miaka yake miwili madarakani nafikiri ikifika 2010 atabaki na Mawaziri wachache aloanza nao.
 
Game Theory hebu njoo utueleze habari za Dola milioni 15 na sio 1.
manake sasa hiyo inaweza kuitwa hatari kubwa!

wazungu watatizama na accounts za mkewe na watoto.

chenge hali imemkalia vibaya kwa vile tu umepita mkono wa mzungu ila kwa JK tu alikuwa yupo tayari kumkumbatia na kutudanganya kuwa ni mti safi

Siyo DOLA ni PAUNDI..BRITISH STERLING POUNDS!
 
Msimao wangu uko pale pale kuwa mh achukue hatua za kishujaa na kizalendo!Licha ya kwamba yeye anafikiri kila kitu ni siri..apo naona atakuwa amekosea.Ila wana jf..jambo moja naona pia nigusie wakati huu ambao tunatoa maoni yetu kwa mh rais.Kwasasa wananchi wa kawaida hawajui msimamo binafsi wa mh rais kuhusu Zimbabwe!Inawezekana wazungu wanambana ili kumfanya atekeleze matakwa yao dhidi ya Mugabe huko Zimbabwe kwa kutumia cheo chake cha uenyekiti wa AU!Ni wazungu hao hao waliomtayarisha JK ili atumikie matakwa yao kwa kuhakikisha anapata uenyekiti wa AU kwa kusaidiwa na UK pamoja na USA..chonde chonde wavuja jasho wasisahauliwe!!Na ndio maana nasema awe shujaa tu!Aombe msamaha..afanye mabadilko ya kikatiba na kiuongozi!Tutamsamehe tu..ni ubinadamu..cha muhimu ni kwamba hatakuwa na haja ya kuwa puppet wa maslahi ya mabepari bali ya taifa na wananchi wake!Atakuwa mzalendo wa kweli na historia a Tanzania itamtukuza!Awapige bao mafisadi na makaburu..awe upande wa haki..na wananchi watakuwa upande wake!
 
aidha baada ya kujiuzuru kwake awe muungwana zaidi
kwa kueleza chanzo cha vijisenti vyake.

kama alishindwa kuwa muungwana wakati anatuibia atakuwaje muungwana wakati wa kuiuzulu?
 
Msimao wangu uko pale pale kuwa mh achukue hatua za kishujaa na kizalendo!

Hivi watanzania tumeishiwa sifa za ushujaa au ndiyo kumpaka mtu mafuta kwa mgongo wa chupa? Hivi nani amesahau uzalendo wa kina Nyerere, kawawa na wengineo. hivi kweli Kikwete si mwanajeshi unafikiri na yeye alikuwa mstari wa mbele wakati wa vita vya kagera? Mashujaa na Wazalendo hawaogopi kufa!
 
...........wagombea wote wawili walioingia tatu bora na msanii kikwete walikuwa maili mia far much better kuliko kikwete..sema basi tu wananchi wote walikuwa as if wamefuniikwa tambara la kaniki machoni na huyu kinyamkera...ndio wanazinduka leo...lakini wachunguzi wa mambo ya kisiasa tangu mwanzo na hadi leo tunasema kama tulivyosema hata kabla ya haya!!!

Mikael,

Mimi siku zote nitakumbuka nilivyokuwa namuua kikwete siyo 2005 tu, bali toka 1995.Nilijua Kikwete mtupu, nikajua pia Mkapa naye mtupu.
 
At last kimeeleweka.

Kilichobakia ni kuwaachia wachunguzi wa Uingereza ambao ninawaamini kufanza kazi yao. Andrew Chenge sasa ajiandae kwa maswali hata kama ana mwanasheria kutoka Cleveland.

Idumu JF!
 
Mikael,

Mimi siku zote nitakumbuka nilivyokuwa namuua kikwete siyo 2005 tu, bali toka 1995.Nilijua Kikwete mtupu, nikajua pia Mkapa naye mtupu.

Mkapa sio mtupu... fikiria vizuri jamaa ni kichwa!! amepotoka kimaadili uzeeni tu na baada ya kulewa madaraka!!! ndio maana alitangaza mali zake akiwa anaiongia madarakani lakini wakati wa kutoka katoka kimyakimya. Yeye mwenyewe anajua mpaka anachukua hakuwa na dhambi, makosa na dhambi nyingi ametenda pale magogoni.
 
Maadili is everything, ukipotoka kimaadili hata kama ulikuwa genius wa PR na international relations na msemaji wa kiingereza mzuri zaidi serikali ya Tanzania nzima bado unakuwa mtupu.

Ukiwa na maadili, hata kama umepungukiwa uwezo katika vikorombwezo vingine watu watakusaidia.

Sasa kama Mkapa siyo Mtupu katusaidia nini miaka kumi aliyokaa urais kama siyo kutuibia tu na kustawisha wezi wenzake kama kina Balali na Chenge?

Mkapa unayemsema wewe si mtupu ni yupi? Ni yule diplomat aliyeenda Australia na kumchamba Tony Blair huku akimtetea mwizi mwenzake Mugabe? Achana na huyo, mimi naongelea Mkapa mlevi mbwa aliyelewa whiskey na kulala fofofo pale Sea View wakati rais Mwinyi anamsubiri airport kwenda state visit.

Naongelea yule Mkapa ambaye mwanae, in a truly prophetic statement, alivyopata habari kuwa baba kawa rais alisema "Mama yangu waTanzania tumekwisha".

Naongelea Benjamin William Mkapa aliyempokea Kissinger na kumu impress Nyerere kwa karama yake mpaka akam promote kumfanya foreign policy technocrat number one, only kulewa madaraka.
naongelea Benjamin Mkapa mjivuni aliyekuwa haendi kanisani (kanisani kwake kulikuwa Hellenic Club na Palm Beach Hotel na rafiki zake wa foreign) Mpaka alipoukwaa urais ndiyo akaanza kwenda St Immaculate, only to stop after finishing his two terms.

Hapo hata sijaingia kwenye Kiwira na connections za kina Andy Chande!

Huyo mtu unamuona ana akili?

Noblesse Oblige ina demand, to whom much is given much shall be exacted.For this precise reason, in the final analysis Mkapa may emerge lower than Kikwete, kwa sababu, unlike Kikwete who is genuinely of feeble mind and malnuorished perception, Mkapa is supposed to be a giant, then how come he left us where he left us?
 
Mimi Ngabu mpaka leo hii siamini kuna watu (tena ambao hujigamba eti wana akili na walipataga divisheni wani fomu foo na fomu six) ambao walimwona Kikwete anafaa. Sijui walichokiona ni nini ambacho mimi Ngabu sikukiona. Kuna kipindi hadi walinifanya nianze kujishuku labda mimi hamnazo...na ndio maana nilikuwa nashindwa kung'amua walichokuwa wanakiona
 
Nyani, nadhani umechanganya kufaulu mtihani na kuelimika.

No..no..no! Sijachanganya kaka. Wao ndio yalikuwa majigambo yao kwamba kwa vile walifaulugu hivyo vidato kwa divisheni wani (kwa kukariri vitu I must say) basi wanajiona kwamba wana akili, uelewa, na wameelimika kuliko akina sisi tuliopataga madaraja ya tatu yanayokaribia daraja la nne. Naelewa kabisa tofauti ya kufaulu mitihani na kuelimika.
 
Nyani,
Naomba kuelewa zaidi. Una maana Kikwete alikuwa anafaulu vizuri mitihani, au unawazungumzia watu wa pembeni waliokuwa wanamshabikia? I am interested to know about his academic performance and background, huko nyuma na hata hapo Chuo Kikuu Dar. Hii inaweza labda kidogo kusaidia kumfahamu vizuri kiongozi wetu huyu.

Nimetafuta mambo muhimu na ya kipekee aliyoweza kuyafanya akiwa waziri katika wizara alizowahi kuziongoza nimetoka patupu. Sijaona hotuba wala uamzi uliojitokeza kumjengea sifa hadi waTanzania tukaona anafaa kuwa Rais. Bado ninaendelea kujiuliza, ni sifa zipi hasa zilizotuvutia?

Watanzania inabidi tuwe na utamaduni na utaratibu wa kumchambua mtu anayetaka kuwa kiongozi. Tusiwe tunaongozwa tu kama ng'ombe kuwakubali viongozi tunaoletewa na vyama bila ya kuhoji.
 
Back
Top Bottom