Msimu mpya umeanza na haya ndiyo mabadiliko unayotakiwa kuyajua kuhusu msimu huu wa ligi kuu Uingereza msimu wa 2025-2026;
1. Endapo kipa akidaka mpira, kisha akaendelea kuushika bila kuuweka chini au kuanzisha mchezo kwa sekunde 8 basi timu yake itaadhibiwa kwa mpinzani kupewa faida ya kupiga kona.
2. Manahodha pekee ndiyo wanaruhusiwa kumfata mwamuzi kumlalamikia tofauti na hapo mchezaji mwingine akimfata refa bila kuitwa au akaenda kwa kuonyesha utovu wa nidhamu, ataonyeshwa kadi ya njano. Kama nahodha ni kipa basi kabla ya mechi, timu itampendekeza mchezaji mwingine ambaye yeye ndiye ataruhusiwa kufanya mazungumzo na mwamuzi.
3. Kama ikitokea mchezaji anayetakiwa kupiga penati, akaugusa mpira mara mbili wakati wa kupiga basi mchezaji ataruhusiwa kurudia kupiga tena.
4. Kwa baadhi ya mechi, marefa watakuwa wakitumja kamera zao kama ilivyokuwa kwenye FIFA Club World Cup, kwenye baadhi ya matukio tulivyokuwa tunaonyeshwa kupitia kamera zilizopo kwenye sare za marefa.
5. Waamuzi watakuwa na vipaza sauti ili kuelezea baadhi ya maamuzi waliyoyafanya uwanjani.