Kwa ajili ya kudumisha utulivu wa kiwango cha mchezo, nimegundua kuwa kushuka kwa ubora wa Cole Palmer kulitokana na mgogoro wa kimahusiano kati yake na mchumba wake, Connie Grace. Kwa sasa, kuna taarifa kuwa wamefanyiana block kwenye Instagram, jambo linaloashiria kuwepo kwa mvutano mkubwa. Mwezi Januari, niliandika kwa kubahatisha kwamba huenda Palmer hachezi vizuri kwa sababu ya matatizo ya kifamilia, na baadaye ikathibitika kuwa ni kweli.
Hali kama hiyo iliwahi kumkumba Enzo Fernández, ambaye kiwango chake kilishuka alipokuwa na mgogoro na mke wake. Walipopatana, aliweza kurejea katika ubora wake wa awali. Naam, naamini kwamba Palmer akiyarejesha mahusiano yake katika hali ya amani, utulivu wake wa kiakili utarudi na kiwango chake kitaimarika katika msimu mzima.
Mbali na hilo, usajili wa washambuliaji wawili wenye uwezo mkubwa kuliko Nicolas Jackson wa Liam Delap na Joao Pedro unatarajiwa kuondoa tatizo la ukosefu wa mabao lililoikumba timu msimu uliopita. Safu ya ulinzi pia imeimarika sana, hata kwa wachezaji wa akiba, hivyo Chelsea ina nafasi ya kuwa na moja ya ngome imara zaidi msimu ujao.
Kurejea kwa Andrey Santos pamoja na usajili wa Mahamoud Sar, Jamie Gittens, na Estevão Willian kutatoa mchango mkubwa katika kuongeza ubunifu na hatari katika safu ya kati na ya mbele. Na iwapo tutafanikiwa kumsajili Jorrel Hato, Morgan Rogers au Xavi Simons, bila shaka dirisha hili la usajili litakuwa mojawapo ya madirisha bora kabisa ya hivi karibuni.