Chelsea FC (The Blues) | Special Thread

Chelsea FC (The Blues) | Special Thread

Ili kikosi kiwe kizuri zaidi
1. Jackson akiondoka, msaidizi wa Palmer atafutwe.
2. Jackson akibaki, hivyo kocha amfanye acheze nyuma ya mshambuliaji ili awe mgawa mipira make hapo yupo vizuri sana.
3. Msaidizi wa Cucurella atafutwe.
Mawinga wetu...Netopia, Gittens, Estavao, George pia Joao Pedro anaweza kucheza nafasi hizo. Sasa ni wakati wa timu kutulia

Palmer yuko na covers nyingi tu:
  • Enzo Fernandez,
  • Andrey Santos
  • Estevão Willian
  • Iwapo Xavi Simons au Morgan Rogers atasajiliwa
Msaidizi wa Cucurella ndie hayupo ila Chelsea sasa wanaamini kuwa wanayo wachezaji wazuri na wakutosha kwenye kikosi cha sasa. Wanaamini Reece James na Malo Gusto wanaweza kucheza kama beki wa kushoto ingawa asili yao ni mabeki wa kulia. Aidha, klabu inaweka imani kwa chipukizi wa miaka 19, Ishe Samuels-Smith, aliyesaini mkataba wa muda mrefu hadi 2031 na kuonekana kama chaguo la baadaye—ingawa bado hajawa tayari kwa kucheza mara kwa mara katika kikosi cha kwanza. Kwa sasa klabu inampango wa kumuuzia Strasbourg ili akapate uzoefu wa kwa kucheza mechi nyingi. Chelsea itaweka kipengele cha kumnunua baadaye kama maendeleo yake ni mazuri. Chelsea wanamuuza kwa ajili ya kukidhi vigezo vya UEFA zinaitaka Chelsea kuuza wachezaji ili ikubaliwe kuwasajili wachezaji wapya waliosajiliwa msimu huu kuweza kucheza UCL. Wachezaji hao ni:
  • Joao Pedro
  • Jamie Gittens
  • Mahamoud Sar
  • Dario Esugo
  • Estevao Willian
Kumekuwa na taarifa za kuhusishwa na Jorrel Hato wa Ajax, mchezaji wa miaka 19 mwenye uwezo wa kucheza kama beki wa kushoto au beki wa kati, lakini hakuna hatua madhubuti zilizochukuliwa. Kwa sasa, Chelsea inaonekana kuzingatia kutumia wachezaji waliopo na kukuza vipaji vya vijana badala ya kufanya usajili mpya.
 
Unajua kwanini nasema THE BLUES ni nzuri kwenye mishandano ya mitoano kuliko mbio ndefu EPL?

Kuna kitu kinaitwa ARI ya wachezaji. Huwa nasema wachezaji wetu wakiamua kucheza angalau 70% - 80% ya Nguvu + uwezo tunashinda mechi kirahisi.

Ili kufikia hiyo % lazima wachezaji wawe na ARI YA JUU. Unaweza kuangalia ARI ya wachezaji walioyoonyesha mechi 14 za mwisho EPL na FIFA CWC.

Hiyo ARI ndio waliyokuwa nayo Liverpool msimu ulioisha hata ukiwatangulia goal walikuwa wana uwezo wa kurudisha na kukubamiza.

THE BLUES kabla ya mechi 14 za mwisho ilikuwa ikipata bao unaona ARI za wachezaji zinashuka kila mchezaji anatuambia good nyt, kupelekea adui kukaza, kusawazisha na kuongeza goli.

Hata msimu ulioisha still tulikuwa na wachezaji wazuri wengi wasiokuwa na ARI ya kutumia nguvj+ uwezo wao kila mechi.

Msimu huu wachezaji wakiingia na ARI ya juu ya kutaka ushindi hata umpange mchezaji gani tutashinda mechi.

Mkuu, hali unayoizungumzia ilikuwepo baada ya mechi dhidi ya Everton tarehe 22 Desemba 2024 na kabla ya Machi 2025. Tangu Machi, hadi Aprili na Mei hadi leo, ari ya wachezaji imebadilika sana, mentality yao sasa ni moja tu: kufunga mabao na kushinda mechi hata kama ni PSG au Liverpool au Mancityu au Arsenal.

Hata katika miezi ya Desemba hadi Machi, Maresca alijipoteza kidogo, akitoa matamko ya kushangaza kwenye mikutano ya waandishi wa habari, jambo lililopelekea wachezaji nao kupoteza mwelekeo. Alidai mara hajapewa majukumu ya kufuzu Top 4, mara hajapewa jukumu la kufuzu UCL, mara timu haiwezi kucheza mashindano manne, mara haiwezi kushinda EPL, au kufunga bila straika—hasa baada ya Jackson kuumia.

Lakini kuanzia Machi, Maresca alibadilika ghafla—akaanza kutangaza malengo ya kumaliza katika Top 4 na kushinda Kombe la Conference League. Na kweli, kuanzia kipindi hicho Chelsea ilicheza mechi 26: imeshinda 20, imetoa sare 2, imepoteza mechi nne tu.

Ninaamini Maresca amejifunza na hatarudia tena kuyumbisha hali ya kifikra ya wachezaji. Ari ya ushindi imejengeka na naamini itaendelea msimu mzima. Na hata kama hatutachukua kombe, Chelsea itamaliza juu ya Arsenal.

1753030574014.png
 
Takataka hii, madueke mweupe.
Wewe ungekuwa mmiliki wa Chelsea ungehama hii dun ia kwenda kuwatafuta aliens waje duniani kucheza mpira. Kila mchezaji kwako ni takataka
Xavi Simons ana miaka 22 tu na kwa achievement aliyokwisha ifikia tim,u yeyote kubwa ingependa kumsajili. Itakayomzuia tu ni kama ataendana na mfumo wa kocha. Chelsea ikifanikiwa kuuza wachezaji na hasa kama kati ya Nkunku an Jackson wakiuzwa, Chelsea inaweza kumsajili Xavi Simons au Morgan Roders. Kwa Moirgan Roders Chelsea inaweza kubadilishana na Nicoals Jackson kwa ajili ya kutimiza masharti ya UEFA. Aston Vila watatakiwa kuuza wachezaji. Sis nuuzwaji wa Noni Madueke→ Arsenal for €55.4M, Djordje Petrovic → Bournemouth for €28.88M, Bashir Humphreys → Burnley for €14M, Kepa Arrizabalaga → Arsenal for €5.8M na Marcus Bettinelli → Man City for €2.4M umetatua hitaji la UEFA.
 
Duh mbona unatutisha. Katika usajili staki kuusikia ni wa Ganacho kutoka Serengeti.
Garnancho ni LW mzuri sana na ana miaka 20 tu, usiwapime Nyumbu wakiwa Serengeti ila wapime wakiwa London 😀 😀😀😀
Wewe sikiliza mziki wa Bryan Mbeumo na Matheus Cunha, wametoka kwenye timu zao wakiwa watakatifu sasa wanaenda kuchafukwa kule Serengeti
 
Wewe ungekuwa mmiliki wa Chelsea ungehama hii dun ia kwenda kuwatafuta aliens waje duniani kucheza mpira. Kila mchezaji kwako ni takataka
Xavi Simons ana miaka 22 tu na kwa achievement aliyokwisha ifikia tim,u yeyote kubwa ingependa kumsajili. Itakayomzuia tu ni kama ataendana na mfumo wa kocha. Chelsea ikifanikiwa kuuza wachezaji na hasa kama kati ya Nkunku an Jackson wakiuzwa, Chelsea inaweza kumsajili Xavi Simons au Morgan Roders. Kwa Moirgan Roders Chelsea inaweza kubadilishana na Nicoals Jackson kwa ajili ya kutimiza masharti ya UEFA. Aston Vila watatakiwa kuuza wachezaji. Sis nuuzwaji wa Noni Madueke→ Arsenal for €55.4M, Djordje Petrovic → Bournemouth for €28.88M, Bashir Humphreys → Burnley for €14M, Kepa Arrizabalaga → Arsenal for €5.8M na Marcus Bettinelli → Man City for €2.4M umetatua hitaji la UEFA.
Shida huwa mnaangalia chelsea pekee ndio mana utaona hivyo, huyo mtoto kwa muda mchache niliofanikiwa kumuona, ni mchoyo sana. Yaan tumeuza madueke mwenye kitambaa cheusi kichwan tunanunua madueke mweupe asie na kitambaa cheusi.
 
Cole Palmer na mpenzi wake, Connie Grace, waliacha kufuatana kwenye Instagram baada ya Cole Palmer kukataa ombi lake la ndoa. Connie amekuwa akimlazimisha Cole Palmer kufunga ndoa ya kimkataba kwa zaidi ya mwaka mmoja sasa, lakini nyota huyo wa Chelsea amekuwa akisitasita na kusema kuwa yeye ni bado ni mdogo sana kwa ndoa na anataka kuzingatia taaluma yake ya mpira kwanza.
1753041475422.png
 
Kama unamaanisha hiyo hata mimi niliona hiyo kwenye comparizon na Morgan Rodgers. Hata hivyo bado Simons amemuach mbali sana Madueke na kama kocha atamuona anafaa ni kwa vile unyimi wake hauna madhara yadhahiri kwenmye kuisaidia timu ishinde. Madueke kwa uchoyo alikuwa too much
 
Mamaqdou Sar anarudi Starsbourg kwa mkopo baada ya kusani mkatab wa miaka nane na Chelsea
1753041783580.png
 
Cole Palmer na mpenzi wake, Connie Grace, waliacha kufuatana kwenye Instagram baada ya Cole Palmer kukataa ombi lake la ndoa. Connie amekuwa akimlazimisha Cole Palmer kufunga ndoa ya kimkataba kwa zaidi ya mwaka mmoja sasa, lakini nyota huyo wa Chelsea amekuwa akisitasita na kusema kuwa yeye ni bado ni mdogo sana kwa ndoa na anataka kuzingatia taaluma yake ya mpira kwanza.
View attachment 3412454
Huu uamuzi wa Palmer unaweza kuisaida sana Chelsea kuliko kuishi na mchumba mgomvi bora aishi peke yake kwanza ainue kiwango chanke cha soka
 
Huu uamuzi wa Palmer unaweza kuisaida sana Chelsea kuliko kuishi na mchumba mgomvi bora aishi peke yake kwanza ainue kiwango chanke cha soka
Amefanya maamuzi sahihi kbs, kwanza mwanamke mwnyew anaonekana yupo kimkakati zaidi, anataka ndoa akijua dogo mali ipo. Amwache dogo ale maisha kwanza ndoa badaeee sana.
 
Hivi mfano ikatokea hii team imeingia UEFA pamoja na Chelsea haiwezi ikawa na shida
Ilikuwa iwe hivyo msimu uliopita na wamiliki walifanya yafuatayo:
Kuanzisha ‘blind trust’:
Hisa za Strasbourg zinaweza kuhamishiwa kwa mdhamini huru (blind trust) ili kuhakikisha BlueCo haina ushawishi wowote wa kiutendaji au kisoka kwa klabu hiyo wakati wa mashindano ya UEFA
Hata msimu ujao ikitokea hivyo naamini ndivyo watakavyofanya

Option nyingine ila sidhani kama wamiliki watafanya ni kuuza share kwa kupunguza ili kuondoa ushawishi wa maamuzi kwenye timu mojawapo wakati wa mashindano hayo
 
Sheria ya UEFA hairuhusu timu mbili au zaidi za mmiliki mmoja kushiriki mashindano, managament inachagua timu moja ya kushiriki. Nadhani ndio sheria hiyo sijui kama imeshabadilika.
Hapana ndg. Hii option ni too extreme na haijawahi kutokea hivyo tangu hiyo sheria itungwe. Crystal Palace wao walifanyiwa demotion kutoka Europa League kwenda Confrenece league kwa sababu wamili hawakufanya yaliyotakiwa kufanywa kabla ya tarehe 1, March ambayo ndio deadline ya kufanya hayo marekebishao ya umiliki
Option ni mbili zenye tija
Punguza share kwenye timu moja ili kuondoa ushawishi wa maamuzi wakati wa mashindano - hii option bado hakuna mmiliki anayekubali kuuza share zake hivi hivi
Option ya pili ni kuhamisha hisa (Share) kwenda kwenye mdahmini huru (Blind trust) ambaye ndie atakuwa na maamuzi ya kiutendaji kwenye hiyo timu wakati wote wa mashindano ambapo yakiisha udhamini wake unaisha pia. Hii ndio safe option kwa wamiliki wengi.
 
Mashabiki wa Chelsea nchini Ghana ni wa kipekee kabisa. Hadi kanisani wako na Chelsea kwa furaha kubwa.
Nguvu na ari yao vinaakisi kwa uzuri shauku na furaha ambayo klabu yetu inaleta kwa watu duniani kote.

Huu uamuzi wa Palmer unaweza kuisaida sana Chelsea kuliko kuishi na mchumba mgomvi bora aishi peke yake kwanza ainue kiwango chanke cha soka
Hii situation ya aina hiyo iliwahi kumuharibia sana Antony Martial akiwa Man Utd lakini pia iliwahi kumuharibia sana Kepa Arrizabalaga akawa anachomesha vibaya mno.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom