Chelsea FC (The Blues) | Special Thread

Chelsea FC (The Blues) | Special Thread

Acha negativity mkuu itakuua wewe mwenyewe, huu ni ushabiki tu wa mpira lengo kuu ni kufurahi, Timu inafanya vizuri na kocha anaenda vizuri. Hakuna kocha asiye na mapungufu na huyu ni mchanga. Anaweza kuja kuwa bonge la kocha kupitia hii timu akiwa na chemistry nzuri nayo
Wewe mwenyewe umeridhia kuwa Kocha ni mchanga kwa sasa ila inawezekana baadaye akawa mzuri, mi ni nani hata nikupinge Mkuu?

Namtakia sana Kocha Maresca mafanikio ila si dhambi kuchambua madhaifu yake inapobidi.

Ubinadamu ni kazi/The humanity is work.
 
Hongereni THE BLUES kwa kufuzu Fainali.

Jana nimengalia mechi bora sana, jana tumecheza kama mabingwa wa UCL 2 Mkononi.

Wachezaji wote 1st eleven walikuwa wa moto kupambania kutinga fainali.

Tunahitaji kusajili msaidizi wa Cucurela, anatumika sana kitakachofuata ni injury. Jamaa yupo fire sana kwa sasa. Kocha asituaminishe Gusto ni mbadala wake.

Kwa muda mrefu tulikosa mchezaji wa kupiga mawe, kuachia bullet, Kutumia nafasi chache kufunga magoli. Jana Jao Pedro amenibubujisha machozi.

Jao Pedro 1 = 10 Jackson

Jao Pedro shikamoo boss
Tuombe Mungu Jao Pedro asipate majeruhi, pia aendelee na consistency kiubora maana isijekuwa ni nguvu ya soda japo kiukweli anastahili kupongezwa.

Ubinadamu ni kazi/The humanity is work.
 
Mosses Caisedo yukoje kiafya kwa mechi zingine kama fainali ya world club cup 2025 wakuu?

Ubinadamu ni kazi/The humanity is work.
 
Kuna baadhi ya mashabiki wa Chelsea ambao tayari wana makocha wao mioyoni, na hawatampenda Maresca kamwe. Kuna wanaompenda sana Pochettino, wengine Enrique, Hans Flick, Tuchel, Conte, Xabi Alonso, na wengine Simone Inzaghi. Orodha inaendelea — kila mtu ana chaguo lake. Hii ndiyo sababu ni vigumu sana kuafikiana kuhusu nani hasa ni kocha bora.
 
Wewe mwenyewe umeridhia kuwa Kocha ni mchanga kwa sasa ila inawezekana baadaye akawa mzuri, mi ni nani hata nikupinge Mkuu?

Namtakia sana Kocha Maresca mafanikio ila si dhambi kuchambua madhaifu yake inapobidi.

Ubinadamu ni kazi/The humanity is work.
Timu nyingi sasa hivi wanwageukia makocha wachanga kwa sababu wanakuwa naflexibility kuliko wale wakongwe. Huyu Maresca atakuja kupata popularity hapa hapa Chelsea. Mbona Pep alipata poipularity Barselona akiwa ni mchanga kabisa na hadi leo hiyo popularity ya Barc elona imembeba hadi kupata heshima kubwa duniani?
Kuna baadhi ya mashabiki wa Chelsea ambao tayari wana makocha wao mioyoni, na hawatampenda Maresca kamwe. Kuna wanaompenda sana Pochettino, wengine Enrique, Hans Flick, Tuchel, Conte, Xabi Alonso, na wengine Simone Inzaghi. Orodha inaendelea — kila mtu ana chaguo lake. Hii ndiyo sababu ni vigumu sana kuafikiana kuhusu nani hasa ni kocha bora.
 
Ila wazee sina imani kabisa na pazia la Ngorika bus. Sijajua kwanini mpaka sasa hivi tumekwama kupata replacement ya Sanchez.
Mike Penders ni mzuri kocha ana hofu tu
Hata Filip Jorgensen ame improve ila bado kocha hamuamini

Uzuri wa Robert Sanchez uko kwenye foot work na kudaka mipira ya juu
Tatizo lake kubwa ni mbili

Yuko slow kureact kwenye mikwaju
Pili saa nyingine anakurupuka na maamuzi ya ajabu ajabu

Beki wetu wameimarika sana na ndio wanaomfichia madhaifu yake
 
Chelkenge nasikia eti msimu huu mmebadili mpaka nicknamed yenu, sasa hivi nimesikia mnajiita "The Black"
01jvpjde2gec7kew1e5h.jpg
 
Wewe mwenyewe umeridhia kuwa Kocha ni mchanga kwa sasa ila inawezekana baadaye akawa mzuri, mi ni nani hata nikupinge Mkuu?

Namtakia sana Kocha Maresca mafanikio ila si dhambi kuchambua madhaifu yake inapobidi.

Ubinadamu ni kazi/The humanity is work.
Sasa unapimtakia mafanikio kocha maresca huku comment zako zingine za fire maresca...mara hajafukuzwa tu tukueleweje mkuu😂...unakuwa kama yule shabiki wa nyumbu Enzi za ole Gunnar anakujaga na comment za Bado hajafukuzwa? Au ndo ww na i.d nyingine?
 
Enzo & Caicedo hizi mashine zipewe maua yao. Work rate yao ni kubwa sana uwanjani.

Tungepata mbadala wa Lavia wakina Enzo na Caicedo wakawa huru kutembea uwanjani aisee eneo la kiungo lingekuwa moto sana.

Lavia majeruhi ndio changamoto.

Labda Santos anaweza kufanya jambo, japokuwa kwa sasa ni mzito sana.
Essugo sijui kwanini hapewi nafasi
 
Kocha wetu tunaweza kumsema vibaya but kiukweli wakati mwingine anafanya vizuri tumsifie, Jana tumepiga mpira mkubwa kuliko mechi zote za michuano hii.Mimi napenda namna tunavyofika mbali kiasi hiki faida yake inasaidia Nini? Tunajenga mentality wachezaji kuwa na uchu ya ubingwa na pia kwa kocha uzoefu wake kuongezeka baadae tutakuwa tishio sana team imejipata mapema kuliko namna wapinzani wetu wanavyofikiri
 
Mnaenda kudhalilika fainali,,, tena Ombeni walau mkutane na Madrid., mkikutana na watoto wa Paris hakuna rangi mtaacha kuona
 
Kitu nilichokiona mechi ya jana

Mbinu za kocha bila wachezaji kujituma uwanjani ni kazi bure

Mbinu za kocha bila selection nzuri ya Wachezaji ni kazi bure

Jana wachezaji walionza 1st eleven walijituma sana kuna muda nilisema moyo wa Enzo utapasuka. Caicedo kapiga kazi chafu sana.

Mabeki ndio usiseme utulivu wa hali ya juu na kujituma kukaba.

Mkanda ulianza kusokota pale sub zilizoanza kufinyika, kule mbele wakaingia makirikiri.
Hii inachangia na kushinda conference cup hii imeleta chachu kwa wachezaji kuwa wapambanaji na kutamani kushinda zaidi makombe
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom