We jamaa umetoa lecture kama Prof wa Chuo kikuu. Mi napenda members wanauona mpira kwa Angel nyingine.
Nakuunga mkono tofauti kati ya Enzo na Makocha wengine mfano Thomas Tuchel, Klop, Conte n.k makocha hao hawakuonyeshi madhaifu ya wachezaji kwenye timu zao, mifumo yao na style zao za uchezaji zinabeba madhaifu ya wachezaji.
Enzo mifumo na style zake unakuonyesha ubora na udhaifu wa mchezaji mmoja mmoja, eneo moja moja (Ulinzi, Kiungo na Ushambuliaji).
Kiufupi kwenye mifumo ya kocha Enzo, eneo linakuwa bora kutokana na ubora wa wachezaji kwenye eneo husika. Ndio maana tunamuona Jackson na Madueke wanazingua, Utawaona Caicedo, Cucurela, Sancho, Palmer na wengine wanakiwasha kwenye maeneo yao kwa sababu wanaonyesha ubora wao.
Madueke sio mchezaji mbaya ila mapungufu madogo madogo ndio yanamuumbua kwenye ubora mkubwa wa mbinu na style za Kocha. Madueke anatakiwa aende sambamba na details za ubora kocha anazotaka kutoka kwake kama mchezaji na sio Madueke kujichezea ilimradi anajiona ana kipaji na uwezo