Mimi kwa sababu zangu binafsi na za kimpira nilipenda Pochetino aendelee kubaki kwa sababu kuna mambo mengi alionyesha kuyamudu.
Nina uhakika wengi hamjasahau mechi ya kwanza ya ligi ilikuwa ni Liverpool vs Chelsea. Mpira ulitembea na mechi iliisha kwa sare, tulipata point kwa city na kumchapa Man U na tangu Januari tulipata matokeo mazuri mpaka msimu unaisha tulikuwa nafasi ya sita.
Wachezaji waliimpove mfan Palmer, Jackson, Caisedo, Mudueke, Galagher, Chalobah, Cucurella, Gusto nk.
Timu ilicheza mpira direct
Tulimaliza nafasi ya 6 huku tukiwa na injuries za James, Fofana, Nkunku, Chilwel, Levi Colwil na hata wachezaji waliokuwa wanacheza wengi walikuwa wamenunuliwa kutoka Belgium, Spain, Portugal etc . Hivyo hawakuwa na uzoefu wa ligi kuu wala kucheza pamoja kama timu.
Lakini lazima tukubali kuwa Poch siyo sehemu ya Chelsea ya sasa. Kocha ni Maresca na inabidi tumback up kwa kumpa muda angalau hata mechi 10.
Pamoja na kuwa hana uzoefu ktk kazi ya ukocha ila anaonyesha uwezo na authority ya kufanya hivyo.
Tumpe muda ili tumhukumu kwa haki. Ila kumhumu baada ya mechi 2 siyo fair.