Chelsea FC (The Blues) | Special Thread

Chelsea FC (The Blues) | Special Thread

Ngoja tupeane muda maana hilo la kwamba owners wamebadili malengo waliyokuwa nayo awali wakati wanamleta Potter na Pochetinho na wakati wanasajili nayasikia leo kwako. Sikujua kama walikurupuka hapo awali na sasa hivi wamebadili gia angani. Na kama hiyo kweli maswali yanabaki kuwa mengi kuliko majibu
Sijasema wamebadili amlengo, maono yameboreshwa
 
Gary Neville’s Top 5:
  1. Arsenal
  2. Man City
  3. Man United
  4. Chelsea
  5. Liverpool
@SkySportsPL

Wameanza baada ya jana kuona mechi ya Chelsea na leo wameona Spurs walivyoboronga na hawana squad depth sasa wamekiri Chelsea itamaliza top 4 tena mbele ya Liverpool

Sasa wasodoaji kazi kwenu
 
Atacheza namba ngapi sasa? Na Felix namba ngapi na Palmer namba ngapi?

Ndo haya ninayoyasema kwamba usajiri unafanyika kwa kuangalia nani atatupa faida baadae na siyo kuunda timu.

The same happened with Petrovic ishu ya kwamba hawezi kucheza mpira ni uongo. Ukweli ni kwamba kwenye makipa wetu ni Petrovic pekee ndo anaweza kuuzwa kwa faida maana ameonyesha kiwango kizuri msimu uliopita.
Nikisema TB ni Mfanyabiashara kuna Mapimbi hunijia resi kuwa ninamchukia, kiaje?

Ubinadamu ni kazi/The humanity is a work.
 
Gary Neville’s Top 5:
  1. Arsenal
  2. Man City
  3. Man United
  4. Chelsea
  5. Liverpool
@SkySportsPL

Wameanza baada ya jana kuona mechi ya Chelsea na leo wameona Spurs walivyoboronga na hawana squad depth sasa wamekiri Chelsea itamaliza top 4 tena mbele ya Liverpool

Sasa wasodoaji kazi kwenu
Waandishi wa habari wa sky ni wanafiki sana na wana chuki ya waziwazi na Chelsea
 
Fagia fagia anayofanya Maresca haina tofauti kabisa na alichokifanya Arteta Arsenal na alichokifanya Kipara baba yao Man city.

Waliingia na kuwaondoa wachezaji wasiofaa, wakiwemo wenye majina makubwa kwenye chumba cha kubadilishia nguo.

Kama meneja, unahitaji kuwa na mamlaka kama hayo na yakiungwa mkono na uongozi kufanya kazi na kuheshimiwa na kikosi. Yeyote anayeona kocha anakandamiza na ana tatizo na hilo anapaswa kuondoka, ili kukuruhusu kujenga kikosi cha uaminifu, kinachofaa kwa soka la kocha.

Arteta alipofanya hivyo, vyombo vya habari vilidai kuwa alikuwa akipoteza chumba cha kubadilishia nguo lakini alikuwa akifanya chumba cha kubadilishia kuwa chake, chini ya udhibiti wake. Ilifanya kazi.

Natumaini baada ya muda mfupi hii fagifagia italeta matunda na furaha darajani
 
Man city ameshindwa kimkeep Alvarez kwa sababu good players can not accept to start on the bench. Palmer ni mfano mwingine. Hivyo wale madogo akina Santos, Paez na Estavao wanaweza kuishia kutuharibikia kwa sababu they are almost on the same age range.

Nikiona mtu anasifia transfer strategy ya sasa nabaki kumwangalia na kushangaa sana.

Hivi umemnunua Sanchez kwa 30+M alafu umuuze kwa 3M baada ya miaka 3 utegemee kuwa na timu bora baadae yenye uwezo kifedha? Au utajikuta kwenye madeni na matajiri wataacha kutoa mkwanja kwa sababu ya hasara. Hapo ndo kifo cha timu huwa kinaanzia.

Nikikuuliza maswali Dewsburry amesajiliwa kwa sababu gani pale Chelsea? Kwa nn hela yake na ya Felix usimnunue Olmo?

Atacheza namba ngapi sasa? Na Felix namba ngapi na Palmer namba ngapi?

Ndo haya ninayoyasema kwamba usajiri unafanyika kwa kuangalia nani atatupa faida baadae na siyo kuunda timu.

The same happened with Petrovic ishu ya kwamba hawezi kucheza mpira ni uongo. Ukweli ni kwamba kwenye makipa wetu ni Petrovic pekee ndo anaweza kuuzwa kwa faida maana ameonyesha kiwango kizuri msimu uliopita.
Unahisi kwa petrovic kunq team inaweza toa 20-30 saizi????

Tukubaliane tu Nkunku hatakiwi kucheza LW hana hiyo threat, hii sio mara ya kwqnza tangu pre season watu washaliona

Nkunku probably atacheza 10 o Akitumiwa kama False no 9

Ndio maana tangu mwanzo nasema usajili wa felix haukufaaa kuhitajika nafas yake kuna 2 player wanaicheza hiyo vizuri.
 
Pia angalia usajiri wetu ni kama unafanywa na watu wasio na akili, una Palmer, Neto (kwangu huyo ni the best and natural winger kwenye wingers wetu wote), Mudueke, Nkunku na madogo wengine kwenye mkopo hivi unamsajili Felix ili aje kuongeza nini kwenye timu?
Mi sijui kwa nini watu wanalalamika, kwani hao wachezaji ni lazima wacheze siku moja??
Mnataka mbaki na akina madueke peke yake, atacheza mechi zote peke yake? Hivi madueke huwa mnaona nini kwake ambacho mm sikioni!!
 
Fagia fagia anayofanya Maresca haina tofauti kabisa na alichokifanya Arteta Arsenal na alichokifanya Kipara baba yao Man city.

Waliingia na kuwaondoa wachezaji wasiofaa, wakiwemo wenye majina makubwa kwenye chumba cha kubadilishia nguo.

Kama meneja, unahitaji mamlaka hayo, yakiungwa mkono na uongozi kufanya kazi na kuheshimiwa na kikosi. Ni kukandamiza mamlaka yako, yeyote ambaye ana tatizo na hilo anapaswa kuondoka, na kukuruhusu kujenga kikosi cha uaminifu, kinachofaa kwa soka lako.

Arteta alipofanya hivyo, vyombo vya habari vilidai kuwa alikuwa akipoteza chumba cha kubadilishia nguo lakini alikuwa akifanya chumba cha kubadilishia kuwa chake, chini ya udhibiti wake. Ilifanya kazi.

Natumaini baada ya muda mfupi hii fagifagia italeta matunda na furaha darajani
Miaka mitatu Arteta amepata trophy ngapi? Kwanini CFC imuige Arteta? mpaka leo anasaka wachezaji wenye uzoefu.
 
Mi sijui kwa nini watu wanalalamika, kwani hao wachezaji ni lazima wacheze siku moja??
Mnataka mbaki na akina madueke peke yake, atacheza mechi zote peke yake? Hivi madueke huwa mnaona nini kwake ambacho mm sikioni!!
Labda uulize wew mkuu, Kuna wadau humu wanaona potential kwa noni.
 
Labda uulize wew mkuu, Kuna wadau humu wanaona potential kwa noni.
Noni anayo potential lakini swali zuri kwani anahitajika acheze peke yake? Timu kubwa inahitaji wachewzaji wazuri wengi washindanie nafasi, na mabosi pale Chelsea wanachokitengeneza ni hicho
 
Hii timu haina scorer.

Inapigwa 2

Inaenda kumleta Felix
Ikipigwa 3 jumapili tunaenda kumleta Sacho
Tukipigwa 6 ndio akili inafunguka na kukubali kumsajilli Osimhen na itakuwa too late
Wamarekani siwatambuagi wanavyotenegneza faida kwenye maamuzi ya kichizi kama hizi
Sio tu Striker hata kwenye defense haijakaa vizuri, kule kulikokaa vizuri ndio tunawekeza nguvu
 
Noni anayo potential lakini swali zuri kwani anahitajika acheze peke yake, timu kubwa inahitaji wachewzaji wazuri washindanie nafasi, na mabosi pale Chelsea wanachokitengeneza ni hicho
Noni watano twanga na sterling wawili weka na mchuuzi wa mykalo ndipo Joao mmoja mkuu.
Noni ni wa kucheza team kama crystal palace au Everton lakn sio Chelsea, nikimuangalia noni anacheza najisemea pengine ningekua Ulaya saiv yawezekana ningekua mchezaji wa premier kwa sababu akili ya mpira yangu ya kucheza mpira ilikua ni mara 5 ya akili ya noni.
 
Mi sijui kwa nini watu wanalalamika, kwani hao wachezaji ni lazima wacheze siku moja??
Mnataka mbaki na akina madueke peke yake, atacheza mechi zote peke yake? Hivi madueke huwa mnaona nini kwake ambacho mm sikioni!!
Kumekuchaaaa.... Mkohoti Vs Madueke mtifuano uko pale pale 😆

Ubinadamu ni kazi/The humanity is a work.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom