juan david
JF-Expert Member
- Jan 23, 2013
- 3,952
- 5,438
Hapo kwa Petrovic ni ngumu mkuu, ingekuwa hivyo makocha wangekuwa wanawafundisha, ndio maana sio kila mchezaji anaendana na style flan ya uchezaji,Ndg umejibu kwa kuchambua vizuri
Pochettino alisaini mkataba wa miaka miwili tu
Pochettino alikatiziwa mkataba wake kwa sababu alianzisha ubishi na uongozi, wamiliki wakaona hayuko tayari kufanya nao kazi kama teammate, alitaka mamalaka zaidi kwenye usajili na uuzwaji wa wachezaji, hili likapingana na maono na muelekeo wa uongozi kwenye hii project
Changamoto kubwa iliyoko kwenye uongozi kwa sasa ni kutosajili kwa kuchanganya wachezaji wenye umri mkubwa na uzoefu, wanaosajiliwa wote ni watoto wanaohitaji muda
Ila kwa upande wa usajili mimi sina shutuma juu yao, wachezaji tulionao ni wazuri na chini ya uongozi muafaka tutavuna tunachokipanda
Kinachowachanganya wengine wasiojua dynamics za soka humu ni kwamba walidhani ubora wa timu mwisho wa ligi utaendela mwanzoni bila kutilia maanani kuwa kocha ni mpya, mfumo ni mpya na wachezaji bado ni wale wale wachanga a,mbao wanajitahidi kuzoea ligi na consitency.
Mimi naamini wachezaji wote wakiwa fit, na kocha akajua naman ya kuwapanga, kuwatumia na mazoezi, timu itashindania top 4, hilo sina shaka nalo
Petrovic na Jorgensen hawalingani
Petrovic anaweza kuwa anamzidi Sanchez kwenye shot stopping
nadhani kwa lavia nahisi ni kwa sababu ya kuwa nje mda mrefu ,Niliangalia mpira dk 90 zote nilichogundua ni haya:
1. Sanchez siyo kipa wa kutegemewa, long ball zote alizipiga nje.
2. Sanchez alichelewa kutoa maamuzi ya kuanzisha mashambulizi na pindi akianzisha mashambulizi lazima apeleke mpira kwenye uelekeo usiyo sahihi.
3. Levia na Chukuemeka hawawezi kusimama sehemu ya kiungo, Levia ni mzito sana...kila mara alikuwa nyuma ya adui pale timu ikipoteza mpira kitu kilichosababisha walinzi kupata shida sana kwasababu hawakuwa na usaidizi.
4. Levi Colwil hqwezi upande wa left back, sijui shida ni nini asiwekwe katikati.
5. Badiashile ile style yake ya kusimama juu ya mpira sijui alijifunzia wapi...anapoza mpira alafu anakuwa mzito kuanzisha mashambulizi, either apigwe benchi au abadilishe namna ya uchezaji, hakuna timu ya kumchukuwa kwa mkopo.
6. James hajakaa sawa, Jana alikuwa anachelewa sana kurudi kufanya recovery pindi timu ikiwa inashambuliwa.
7. Modrik amebadilisha nywele ila hajabadilika.
8. Madueke akiongeza umakini ni mchezaji mzuri.
9. Marc Geui ni mchezaji mzuri sana, kila wakati alikuwa sehemu sahihi.