Chelsea FC (The Blues) | Special Thread

Chelsea FC (The Blues) | Special Thread

Wewe labda huangalii mpira, kamfatilie kuanzia Bundesliga ana goli 10+ ,

Anajua ku dribble na kukaa na mpira na anajua kufunga

Katika mpira ogopa Sana mchezaji anayeweza kukaa na mpira ,

Naomba huyu jamaa msimpate na asije EPL , huyo Ni balaa jingine
Mimi nilimfuatilia na un ayosema yote ni kweli kabisa. Anayo pace na nguvu na ndio advantage yake inayomfanya akae na mpira kwenye final third. Asingeweza kucheza kila mara kwa sababu hizo nafai ya no. 10, CAM wanashika Mbape na Griezman na no. 9 ambayo pia anacheza kashika kipenzi cha kocha Giroud. Ana miaka 25 tu na kwa bei ya mil 10 ni sawa na bure. Hiyo bei haimaanishi ni mchezaji wa hovyo ni kwa sababu asipouzwa january July 23 ataondoka bure. Na baada ya dirisha kuisha anayo uhuru wa kupatania mkataba na timu yeyote bure
Stats zake
Mechi 15 za ligi magoli 10 na 3 assist
Katika mechi 15 ya ligi kajihusisha na magoli 13
Katika hizo mechi ana jumla ya mashuti 55
DFB Pokal mechi 2 goli 3 na assist 1
Katika mechi 2 za DFB Pokal kajihusisha na magoli 4
Jumla ya mashindano yote Mechi 17, goli 13, assists 4
Katika mechi 17 ya mashindano yote kajihusisha na magoli 17

Kwenye kushoot anazo shots 55 zinazomfanya kuwa wa kwanza Bundesliga na goal attepmts wa pili. Ana urefu wa 1.92M na hivyo kumfanya kuwa mzuri sana kwenye kuwania mipira ya juu
 
Wachezaji wanahisi maamuzi ya kufanya mabadiliko kwenye idara ya matibabu kwa wachezaji yaliyofanywa msimu uliopita wa kiangazi umeleta madhara makubwa kwenye majeruhi ya wachezaji.

Chelsea players are reportedly concerned that the club's decision to overhaul their medical department last summer has backfired - with the Blues said to be launching a review into their injury crisis.

66551873-11632769-image-m-2_1673630282936.jpg

1244437541.0.jpg

newFile.jpg

0_GettyImages-1243750982.jpg
 
Tarajia kutoona tetesi ovyo ,Chelsea wamekuwa wahuni Sana kwenye usajili

Walimfanyia Hivi hivi city kwa Cucurela , kwa Barca ndio walishindwa

Ila dili nyingi Toddy hafanyi negotiation ,anakuja anauliza Bei anaweka mezani,.
Tulieni jamani bado tunaunda timu ambayo mtaiogopa sana

1673844551876.png
 
Sasa hivi tarajia ukimya ,halafu klabu zitawaundia zengwe tu ,wewe subiri uone , hawawezi kubali kila target zao mnaingilia

City kwa Cucurela mlimfanyia uhuni

Liverpool alijifanya anamtajataja Enzo , Hadi Sasa pale Hana chake

Gakpo ilikuwa Gafla ,nadhani angekuwa Chelsea muda huu
Wiki hii tutadeal na Noni Madueke na Thuram + kiungo mmoja
 
Haaland alikuwa na mapenzi na City na kwa sababu yeye alikuwa na maamuzi ya RC yake aliweza kubebwa na city very cheap

Makhailo Mudryk alikuwa na RC ya Eur 50M ila muda wa kutumia hiyo clause ilikuwa haijafika na hivyo hakuwa na maamuzi ya uuzwaji wake. Naamini angekuwa na uhuru kama Haaland angeenda Arsenal na Arsenal wangembeba kwa Eur mil 50 tu by cash bila addons
 
Telegraph wanaripoti kuwa Chelsea wanamuania RB wa Real Valladolid anaitwa Ivan Fresneda 18yrs. Huyu ni Tunda la Real Madrid academy na ni mzaliwa wa Madrid
Ivan anawaniwa na Newcastle na Arsenal na amefanyiwa tathmini ya kuwa na dhamani ya paundi mil 15

p564899_t192_2022_0_002_000.jpg
 
Wapendwa mashabiki wa Chelsea
Amani iwe nanyi
As-salaam 'alykum

Kwa nini matokeo kwa sasa ni mabaya sana kwa Chelsea?

Sababu yake kubwa ni mbili ambazo ni mabadiliko ya umiliki na uongozi iliyosababisha mabadiliko haya:
  1. Mabadiliko ya Maono na
  2. Mabadiliko ya Approach
HOW?
Wakati wa Roman Abramovich lengo ilikuwa angalau kila mwaka kushinda makombe na hiyo ilitimia ila hapa kuanzia 2018 hadi leo ukiacha 2021 iliyumba sana
Jinsi au apprach ya kufikia hayo maono yalikuwa hayana uendelevu ndani yake
Alimradi mbinu mbinu na ujanja ujanja utumike ili kufikia maono
Mbinu mojawapo ilikuwa kuajiri wachezaji walioiva na kubadilisha makocha kila mara
Approach kubwa ilikuwa ni kuwasikiliza zaidi wachezaji kuliko kocha. Hii haina uendelevu kwa sababu kocha anafanya kazi kwenye mazingira ya woga na kutokuwa na jitihada zozote za kujenga timu kwa sababu wakati huo "PROCEES" ilikuwa haiaminiki kabisa. MOU aliletwa darajani mzee wa mbinu mbinu na kweli mbinu zake za kupaki mabasi na kushambulia kwa kushtukiza iliua kabisa ufalme wa Mwanitesa United na Arsenal kila mwaka wao ndio title contenders.
Alipotoka MOU wakaja wengine kwa staili hiyo hiyo na ndio maana makocha wengine walishindwa kuleta makombe walifukuzwa haraka sana. KOcha wa Chelsea wakati huo kama huna mbinu na ujanjuaujanja ulikuwa hufai kuwa kocha wa Chelsea. Wale makocha wenzangu wa kujenga timu na kujali sana process walikuwa hawafai kuwa makocha wa Chelsea.

Nakumbuka ile 2016 akina Fabregas, Costa na Hazard walivyomgomea MOU akatimuliwa ili kambi itulie na Conte alipokuaj na mbinu zake pup tukabeba EPL tena

Sasa wamekuja Wamarekani
Maono yao ni kuwa na timu imara iliyojengwa kutokea kwenye mizizi. Yaani timu ambayo haitegemei tena kuwanunua wachezaji walioiva badala yake kuwepo na pool ya academy ambao wataingizwa kwenye first team bila kutumia ghrama kubwa. Na ndio maana usajili mkubwa wa akina Boehly ni wa vijana chini ya miaka 21

Hawa tunaowaona zaidi ya miaka 21 ni kwa ajili ya kutatua tatizo la muda mfupi ambalo wamelirithi kutoka kwa utawal uliopita

Wao wanaamini ukishakuwa na timu iliyojengwa imara kuanzia kwenye mizizi pia kutakuwa na uendelevu wa kubeba makombe

Juhudi ya kuhakikisha hili linatimia limeonekana pia kwa kuboresha idara ya scouting kwa kuingia mkataba na digital scouting system inayoitwa AiScouting kwa miaka mitano na ikionyesha manufaa nadhani huu ndio utakuwa mtindo wa maisha pale darajani.

"London, UK – Chelsea FC has today announced the signing of AiSCOUT – the world’s first fully automated talent analysis and development platform.

The six-times Premier League and two-times Champions League winners negotiated a deal to secure AiSCOUT as their Official Academy Research Partner, with the platform set to become an integral part of the club’s recruitment and scouting process for academy players over the next five years."

Approach ya wamiliki wa sasa ni kuwa upande wa kocha, wachezaji wasioperform aidha kwa kushuka form au kumgomea kocha kama akina Fab, costa na Hazard, watatimuliwa kama Arteta alivyomtimua Auba
Mimi naona hiii approach ni nzuri kwani itarudisha heshima kwa kocha na wachezaji watamsikiliza kocha na kufanyia kazi maelekezo yake bila mgomo baridi.
Hakutakuwepo na mchezaji aliyemkubwa kuliko kocha au timu. Conte alipogundua hiyo tabia ya kumgomea kocha kwa Costa alimtimua kwa sms kitu ambacho iligharimu ajira yake. Natamani Conte ndie huyo wa 2017 angekuwepo sasa Chelsea ya akina Boehly. Wangeendana ile mbaya. Na Chelsea ingetisha ile mbaya. Ndio maana mimi bado naomba Mungu Boehly na wenzake wangetumia tu busara kukatisha mkataba wa GP na kumchukua Conte pale Spurs kwa sababu hajaridhika kabisa. Spurs hawana jeurii ya kuingia sokoni na kwa hiyo Conte kabakia na matakataka yanamchefua sana pale Hotspurs.

Hii aproach ya kujenga kuanzia kwenye mizizi na kuwa upande wa kocha itakuja kuonekana dhahiri baada ya misimu mitatu hadi minne ambapo utamaduni wa timu nzima itakuwa kila mtu atimize wajibu wake. wachezaji kumheshimu kocha na kocha kufanya kazi kwenye mazingira ya uhuru bila woga. Pia overhead ya timu kwenye manunuzi yatakuwa yamepungua sana na akina Boehly watapiga pesa nyingi za faida ile mbaya. Kwa wakati huo pia Chelsea itakuwa imenunua vilabu mbalimbali duniani kama ilivyo kwenye plan kwa ajili ya kuzifanya hizo vilabu kuwa ni pool ya kuwapata wachezaji ambao ni talented kwa bei rahisi

Ikifika wakati huo kama vilabu vingine havijafanya mabadiliko kama haya watakuwa wanaisikia Chelsea kwenye bomba tu. Kwa sababu kama timu inapata faida na ina wachezaji wanaoweza kufanya lolote uwanjani kwanini UEFA isiwe ya kwetu kila mwaka?
Kwa nini EPL isiwe ya kwetu kila mwaka?

Mashabiki wenzangu wa Chelsea tusiwe na shaka na uongozi kwa mwaka huu. Hata tukimaliza nafasi ya 17 no problems

Tukishalima sangari na kupanda, wakati wa mavuno tutachekelea juu kwa juu

YAJAYO YANAFURAHISHA ZAIDI
 
[emoji23][emoji23][emoji23] Hii akili yako haitofautiani na wale jamaa wa fursa za kilimo cha matikiti.
Screenshot_20230116_114825.jpg
 
Hawa wachezaji nane (8) ni lazima watoke July 2023 aidha kwa bure kama Jorginho, kwa mkopo au kuuzwa kabisa
  1. Jorginho
  2. Ziyech
  3. Auba
  4. Havertz
  5. Pulisic
  6. Azpilicueta
  7. Koulibally
  8. Reuben Loftas Cheek
Mkuu hebu moeni Havertz heshima yake bhana. Jiulizeni ile performance yake timu ya taifa iko wapi? Chelsea kuna kitu hakipo sawa naamini Havertz yuko sawa.

Hii pia kwa wale wanaomsema Mount kwamba hatufai wakumbuke yule Mount wa msimu uliopita.
 
Sawa mkuu, naona maombi yako yamefika kwa matajiri kwa sababu kiangazi kuna sangari zinang'olewa hapo darajani.

Ila hawa hawatakwepa
  1. Jorginho
  2. Ziyech
  3. Auba
  4. Pulisic
  5. Azpilicueta
  6. Reuben Loftas Cheek
Bahati mbaya sana Pulisic na Cheek wana umri mdogo ila watafyekwa tu
Cheek Leicester city wamehsamwekea radar zao
Pulisic Juve wanamtaka swapa deal na Denis Zakaria
 
Hiyo ofa imekataliwa na PSV wanataka ofa karibu na mil 40
Huyu mchezaji alipendekezwa na Christopher Vivell na bado nasikia anasukuma uongozi umsajili haraka

1673881246339.png
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom