Todd Boehly na TT hawakuwa wanaelewana kwenye mambo mengi
Suala la shared vision kama sababu ya kuachana ilikuwa ni kisingizio tu
Baadhi ya tofauti zenyewe ni
- Boehly alimtaka Ronaldo, TT hakumtaka tena alisema waziwazi kwenye media - Boehly hakulipenda hilo
- TT alimtaka Fofana afanyiwe medical test London ili ajumuishwe kwenye timu haraka, Boehly alikuwa na plan tofauti ya kumpeleka Fofana Marekani - TT hakulipenda hilo na alikasirika waziwazi
- TT alimsifia Marina na kumuita ni Director mzuri kwenye media - Boehly alichukia kuona Manager wake yuko upande wa Marina ambaye hakutakiwa tena kwenye bodi ya Chelsea
- Boehly alisema kule Marekani, unapochukua biashara lazima uwe na uhakika kwamba uko pamoja na watu wanaoendesha hiyo biashara
- Lengo letu ni kumtafuta kocha ambaye yuko tayari kushirikiana na sisi
- Kuna KUTA nyingi zinazotakiwa kuvunjwa pale Chelsea
- Kabla ya hapa timu kuu na academy hawakuwa wana mfumo wa taarifa shirikishi yenye kueleza wachezaji muhimu wanatokea wapi
- Ukweli ni kwamba hatukuwa na uhakika kama Tuchel aliona kile tunachokiona sisi
Kwa maoni yangu
Boehly akiendelea kuwa dikteta kwa viongozi technical wa timu kama sporting director ajaye, kocha na wengineo, Chelsea itaharibiwa na itaishia kuwa mid table timu.
Nasema hivi kwa sababu Mmiliki anayeingilia kati maamuzi ya technical people itafanya Chelsea ikataliwe na very important staff and players
Dalili hizo zimeshaanza kuonekana
Fuatlilia Saga la Sporting Director wa RB Salzburg, huyo bwana ameoan mbali, akafikiri akawaza kuwa akikubali ofa ya Boehly hata kama ni nzuri atakuja kumfanywa boya wa kutekeleza matakwa yake na hivyo kumharibia jina
So akaona better kubaki huko Salzburg ambako anapewa uhuru wa kufanya kazi yake
Wekeni haya maoni yangu vizuri, Kocha kama PEP hata akipewa mshahara mara 2 ya pale City hatakubali kufanya kazi na Boehly.
So huko tunakokwenda tutaishia kuwapata watendaji na makocha wa kawaida tu ambao wao lengo lao ni mshara na wala sio kutenda kazi yao professionally
Wengine humu tulishangilia kwa TT kuondolewa lakini nimefikiri nikawaza nikagundua hili nililolisema
Na staili ya wamarekani wengi wanajiona wao wanajua kuliko wengine na ndio maana katika soka la Uingereza wamarekani wengi wanafeli kwa sababu wanajifanya wanajua biashara hii ya soka kumbe hawajui