Chelsea FC (The Blues) | Special Thread

Chelsea FC (The Blues) | Special Thread

343/4222 hybrid

Siumesema kocha hana formation , kama unafatilia utajua tuchel anatumia mfumo gan kuanzia huko alipotoka n utajua kocha huwa anademand nini kutoka kwa wachezaj wak
Mifumo sio formation hapa ndio sasa footbal come to the mix
Formation ni mpangilio tu ya wachezaji uwanjani ili uweze kuachive mfumo wako kama kocha
Hapa ndio tunapoteana kwenye lugha

Tunaposema system au style au mfumo kwa kiswahili tuna maanisha philosofia au falsafa ya mpira kocha anayotumia kupata matokeo,
Mfano PEP anatumia possesive footbal akiamini kuwa wachezaji wakiwa na mpira wanaweza kuufanyia kazi yeyote wanayotaka hadi kupata matokeo wanayotaka
Klopp anatumia Direct football, mpira wa kuupeleka mbele haraka haraka kufanya mashabulizi, akiamini kuwa mpira unaopelekwa mbele unaoverload final third na kuzaa matunda

Conte anatumia falsafa ya kushambulia kwa kushtukiza au counter akiamini hivyo hivyo kuwa mpira wa kushtukiza unaleta matokeo haraka kwa sababu nafasi zitakuwa zimeachwa wazi na hivi kuzitumia kabla timu pinzani haijarudi nyuma kucover

Niamb ieni TT anatumia style ipi, na usije na formation hata Karubanzila leo akipewa timu hatashindwa kuwapanga wachezaji wake uwanjani hata kwa 2-2-2-2-2

Goodnight
 
Style ya uchezaj wa tuchel tangu amekuja katika build up huwa anatumia 3-2 base (5 man base)

Wakat huo kuna kuwa rotational ya nafasi kwa wale wa tatu wa mbele huku wakirudi juu kidogo kupokea mpira na huwafanya tim pinzan kwenda kupress ile base yetu na kucreate nafasi kwa wale no 10 wawili

Hiyo kwa kifupi,

Njia nyinginge ni jinsi anavyocreat overload upande mmoja na kucreat nafas upande wapili, refer msim uliopita wakat reec n chilwel walivyokuwa katika form before injury + game ya juzi ya spurs goal la 2

Hii ni summary tu.
20220827_000539.jpg
20220827_000719.jpg
20220827_000723.jpg
20220827_000821.jpg
 
Style ya uchezaj wa tuchel tangu amekuja katika build up huwa anatumia 3-2 base (5 man base)

Wakat huo kuna kuwa rotational ya nafasi kwa wale wa tatu wa mbele huku wakirudi juu kidogo kupokea mpira na huwafanya tim pinzan kwenda kupress ile base yetu na kucreate nafasi kwa wale no 10 wawili

Hiyo kwa kifupi,

Njia nyinginge ni jinsi anavyocreat overload upande mmoja na kucreat nafas upande wapili, refer msim uliopita wakat reec n chilwel walivyokuwa katika form before injury + game ya juzi ya spurs goal la 2

Hii ni summary tu.View attachment 2335915View attachment 2335918View attachment 2335919View attachment 2335922
Arrangement sio style, rudia hilo darasa Tena. Baadae nitafafanua styles za football au mifumo in relation to formation.

Style now falsafa na haihusiani na mpangilio wa wachezaji uwanjani. These are two different phenomena

Arrangement au formation ni kuwapanga wachezaji kulingana na uwezo na talkents zao ili wakuletee matokeo.
mfano unaweza ukatumia counter attack style ukitumia 433 kama alivyofanya MOU akiwa Chelsea au ukatumia 343 kama alivyo fanya Conte akiwa Chelsea nk.
 
Ukitaka kujua TT ana shida, wee fuatilia, Sterling atasota sana kufunga hadi atawekwa benchi, narudia tena kusema haiwezekani wachezaji wengi wala sio wachache walikuwa wanafanya vizuri kwenye timu zao wamekuja Chelsea na kuflop
Nampenda sana TT ila asipobadilika mimi nitaacha kumsema vizuri
Hafai hata kufundisha academy
 
Matokeo yakiwa mabovu ndio huwa tunatafuta sababu ila katika kitu nachoamini mimi wachezaj ndio wanaomuangusha kwa nafas wanazokosa tho na yeye anamapungufu yake.

Game nyingi tu tunapoteza/tunadraw coz ya uzembe wa wachezaj wetu kwa either wakose chance o kufanya mistake. (Chance wanazokosa wakina mount/havertz/werner etc huwezi mlaumu kocha, mistake anazofanya mendy,chalobah etc huwez mlaum).

Ni game chache sana unakuta tuchel ankuwa complicated
 
Sergi Milonkovic Savic wa lazio sijui kwa nini tim kubwa hazimuoni huyu mwamba
Jana aliiwezesha Lazio kuwaziba Inter na Lukaku akirangaranga tu 3-1 ikiwemo pasi murua ya huyo mwamba aliyompasia Felipe Andertson
 
Dili la Auba linaelekea kufeli kwa sababu ya mkataba
Auba anataka mkataba wa miaka miwili, sisi Chelsea tukasema miwili haifai kwa veteran wa miaka 33
 
Dili la Auba linaelekea kufeli kwa sababu ya mkataba
Auba anataka mkataba wa miaka miwili, sisi Chelsea tukasema miwili haifai kwa veteran wa miaka 33
TT is desperate alichelewa kufanya maamuzi sokoni yani uuze Lukaku 26 na Warner 24 ununue Auba 33, sawa wote wana kasoro ila hapo tofauti kubwa ni ipi? Ni sawasawa kuuza filinji na kununua coolerbox
 
343/4222 hybrid

Siumesema kocha hana formation , kama unafatilia utajua tuchel anatumia mfumo gan kuanzia huko alipotoka n utajua kocha huwa anademand nini kutoka kwa wachezaj wak
Nitaelezea systems au styles au philosophies au falsafa maarufu za Football zinazotumika kwa sasa,
Hii mifumo inaweza tumiwa na formation yeyote ile, formation itabadilika tu kuendana na aina ya wachezaji ambao kocha anao chini ya umiliki wake

Tafsiri ya football system au mfumo
Mfumo ni maelekezo ya kimbinu wanayopewa wachezaji inayohusiana na kujilinda ili kuzia kufungwa magoli na kushambulia ili kufunga magoli.

Timu moja kwa mechi moja inaweza ikatumia mifumo zaidi ya moja ili kutekeleza lengo la hiyo mechi husika

Kocha anyebadilibadili mifumo kwenye uchezaji anaweza kuwachanganya baadhi ya wachezaji hasa wale wachanga na kushindwa kutekeleza maelekezo hayo na hivyo kusababisha mbinu kushindwa kufanya kazi

Mifumo yenyewe ni:

Possesive Footbal
Kocha anyetumia mfumo huu anaamini kuwa kukaa na mpira sana unatoa mwanya wa ku buy time ili kuforce timu pinzani ifanye makosa, itoe mwanya wa kushambulia na kufunga. PEP ni muumini wa huu mfumo tangu aanze kufundisha soka. Timu kama Barcelona, Napoli wanatumia pia mfumo huu

Direct Football
Hakuna kupoteza muda, Kocha kama Klopp anaamini kuwa kuupeleka mpira kwa haraka kutoka point moja hadi nyingine kwa kwenda mbele inaleta matokeo tarajiwa kwa haraka. Timu inayocheza mfumo huu ikipoteza mpira inafanya jitihada kubwa kuwin second balls na kuendelea kupeleka mashambulizi mbele ili kufunga. Timu zinazotumia mfumo huu consistently ni Liverpool, pia Lampard ni muumini wa huu mfumo

Counter Attack Football
Kocha anayetumia huu mfumo anaamini mpira wa pasi chache hadi golini unatoa fursa ya kuexploit nafasi zinazoachwa wazi kizembe na timu pinzani wakati wanashambulia au wanamiliki mpira kwenye final third. Mfumo huu unahitaji kuwa na washambuliaji clinical kwenye kupasiana na kufunga. Conte, MOU ni waumini wa huu mfumo kwa mfano MOU kautumia akiwa Portal, Chelsea Inter na Real Madrid na ikamletea mafanikio makubwa sana
Kwa sasa timu zinazotumia huu mfumo waziwazi ni Tottenham chini ya Conte na Real Madrid chini ya Anceloti.

Total Football
Huu mfumo unamtaka mchezaji kumiliki nafasi wazi yeyote iliyoachwa wazi hasa wakati wanamiliki mpira kwenda kushambulia. Kwa huu mfumo ni ngumu kujua mchezaji anacheza nafasi ipi. na hivyo kiuwa ngumu kufanya marking. Barcelona na Juventus wanautumia mfumo huu sana

Low Press
Huu mfumo unatumiwa na timu zenye lengo ya kujilinda tu, kupaki mabasi hadi mwisho wa mechi hasa kama hiyo mechi hyaina umuhimu wa kushinda au hawataweza kushinda

Positional au Zone Marking
Mfumo huu unamtaka mchezaji kuhakikisha anabaki kwenye positiuon yake na kuulinda vyema

Mifumo inaweza kuendelea zaidi ya hapa
 
TT is desperate alichelewa kufanya maamuzi sokoni yani uuze Lukaku 26 na Warner 24 ununue Auba 33, sawa wote wana kasoro ila hapo tofauti kubwa ni ipi? Ni sawasawa kuuza filinji na kununua coolerbox
unaposema Lukaku 26, Werner 24 una maanisha nbini?
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom