Chelsea FC (The Blues) | Special Thread

Chelsea FC (The Blues) | Special Thread

Fainali zote za uefa tulikuwa na wachezaji tegemezi karibia kila sekta na zote tulifanya vizuri
Goalkeeper Peter Cech
Beki John Terry
Kiungo super Frank
Forward Drogba

Leo mchezaji tegemezi ni ngolo kante pekee. Hao waliobaki labda muujiza utokee. Tena wakifanya ujinga kama ile gemu ya Leicester tutapigwa hata goli tano.

De bruyne ni mwiba,kwakweli leo nimejiandaa kupokea kipigo heavy




Sent from my SM-J701F using JamiiForums mobile app
2012 Terry alikuwa nje ya squad
Walicheza wachezaji wa kawaida sana
  1. Petr Cech;
  2. Ashley Cole,
  3. David Luiz,
  4. Gary Cahill,
  5. Jose Bosingwa;
  6. Frank Lampard,
  7. John Obi Mikel;
  8. Ryan Bertrand,
  9. Juan Mata,
  10. Salomon Kalou;
  11. Didier Drogba.
Substitutes from:
  1. Ross
  2. Turnbull,
  3. Michael Essien,
  4. Paulo Ferreira,
  5. Oriol Romeu,
  6. Florent Malouda,
  7. Daniel Sturridge,
  8. Fernando Torres.
Ukimuondoa Petr Cech, Ashley Cole, David Luiz, Frank Lampard na Drogba wengine ni kawaida mfano Mikel alisugua benchi hadi alipohama, ndie alikuwa kiungo chetu, Hiyo mechi tulikuwa real un derdogs hata Bayern hawakuamini baada ya ile penalti ya Drogba, walilia uwanja mzima na mashabiki wao
 
Waungwana mfahamu kuwa Mchezo wa leo ni fainali sio ligi na mchezo unachezwa mara moja tu kwa dakika tisini. Timu zote mbili Chelsea na Man City, wachezaji wote wa timu mbili yaani wachezaji wa Chelsea na Man City na makocha wote wawili Pep na TT wote hili kombe wanalihitaji sana. Niwambie tu timu zote mbili leo zitacheza kwa nidhamu kubwa mno, pia tusitalajie mchezo mzuri bali tutalajie mchezo mgumu sana. Timu zote mbili naona zikiingia kwa mfumo wa kujilinda na kushambulia kwa kushtukiza. Pep tayari ana onyo kutoka kwa TT hivyo hawezi kuja kijinga jinga tu, akija kijinga jinga tena atapokea za uso. TT nae anaelewa uzuri wa Man City na madhaifu ya safu yake ya ushambuliaji hivyo lazima leo atabadilika tu.

Mshindi wa leo atatokana na mbinu tu, na si ubora wa wachezaji. Mchezo wa leo ndio mtajua umuhimu wa kocha ama mwalimu katika mpira. Leo msitishwe na majina ya wachezaji kama KDB, Mahrez, Foden, Gundogan, Dias, Rudiger, Kante, Mount, Pulisic na wengineo wote. Hao wote na wengineo leo mtawakataa na kusema ndio hawa kweli, naam watakuwa wao na wala si wengine. Leo ni vita ya mbinu tu, leo ni ugomvi baina ya TT na Pep hao wachezaji wataingia uwanjani wakiwa kama wajumbe wa kufikisha hizo mbinu za walimu wao.

Msitarajie mechi kuanza kwa kasi, mechi itaanza kwa kila kocha kumsoma mwenzake yuko vipi ama amekuja vipi. Na kipindi cha kwanza kinaweza malizika kwa suluhu ya bila kufungana, kipindi cha pili kitabadilika kidogo tofauti na kipindi cha kwanza. Kama nilivyo sema huko juu leo timu zote mbili zitacheza kwa kujilinda sana, mchezo utabadilika baada ya timu moja kupata angalau goli moja.

Kwa uchache hayo ndio naona leo yakienda kutokea, karibu kwa masahihisho.
PEP kashasema kinachomsumbua anapokutana na Chelsea ni mfumo wanaotumia wa wingbacks na kasi ya Werner inawafanya wajikute wameacha space kubwa kwa wachezaji wengine wa chelsea kushambulia. Kasema alipohojiwa kwenye press conference kuwa kila wakati wachezaji wake inabidi warudi nyuma kujilinda na kumuangalia sana werner
Tutegemee leo Werner atakuwa amekatiwa RB ya Robery na akipumua ni bahati sana. Werner akiwa kwenye form atatusaidia sana kutengeneza space na nafasi za kufunga. Pia Kante akiwa na form kama ile ya Real Madrid tutafurahia ushindi. Ila hao wachezaji muhimu wakiflop, tumepigwa na ndio wasiwasi wangu uko hapo
 
We unaongelea tulitufunga wakat kocha alikua ni yule ndugu yake na Arteta, Lampard. Sahv usifananishe hii timu na utopolo ule w Lampard timu yoyote ilikuaga inajichukulia tu point kwetu kirahisi.
Sawa. Siku hizi tunachukua pia au hatujachukua?
 
We unaongelea tulitufunga wakat kocha alikua ni yule ndugu yake na Arteta, Lampard. Sahv usifananishe hii timu na utopolo ule w Lampard timu yoyote ilikuaga inajichukulia tu point kwetu kirahisi.
Lakini huyohuyo ndugu yake na Lampard (Arteta),kachukua point zake 3 kilaini tu tena mkiwa na huyo kocha wenu mtaalamu. LEICESTER kajipigia mara mbili na hata top four mmeingia kwa hisani ya Tottenham, au unasema team ipi?
 
Eeeh Mungu wa Isaka, Ibrahim na Yakobo tunakuja mbele kwa unyenyekevu tunaliweka chama letu THE BLUES mikononi mwako bwana.

Wachezaji tunawaweka mikononi mwako bwana, kama jemedari wa vita ukawaongoze kushinda hii vita iliyoko mbele yetu dhidi ya CITY, wakapambane kwa akili na moyo mwisho wa filimbi tukabebe hili kombe na kuandika historia nyingine katika ulimwengu wa mpira.

THE BLUES in GOD WE TRUST.

Amen

Tukutane baada ya mechi.View attachment 1801274
Tawire
 
Lakini huyohuyo ndugu yake na Lampard (Arteta),kachukua point zake 3 kilaini tu tena mkiwa na huyo kocha wenu mtaalamu. LEICESTER kajipigia mara mbili na hata top four mmeingia kwa hisani ya Tottenham, au unasema team ipi?
Kama kachukua point 3 Kwa chelsea kashindwa nn kuchukua point 6 mbele ya Burnley....ndo maana tunasema Ndugu yake na lampard
 
Hakika leo man city atapigiwa mpura mwingi Sana na kumbua AGUERO bado hajabeba taji la UEFA anazindia na KANTE ambae yeye ameshika kombe la UEFA
Mpura KANTE kashika UEFA lini chelsea mmejaa wauza ugoro
 
Mkuu angalia mchezo mitatu walizokutana Kati ya man city na chalsea man city kashinda Mara moja chalsea kashinda Mara mbili najua hapo utaenderea kuona tofauti kwa timu mbili zilizoingia fainally kwer nzote ni mbola ila ludi kuchambuachezaji mmoja mmoja bado tuuu Chelsea utawapatia nafasi ya kusonga mbele zaidi ya kuchukua kikombe Cha reo
Una bangi wewe mchezaji mmoja mmoja chelsea imzidi man City umeishia form ngapi?
 
Man city sijui atacheza mbinu gani leo. maana akifunguka anakufa kama madrid.

Akipaki basi sina imani kama atatoboa sababu hana watu wa kupaki basi. Ile match ya pili na psg alipaki basi ila pochetino akawa mdwanzi. We mbappe anaanziaje benchi match kama ile?
Mbappe ambaye hakupiga shuti firt match kweli chelsea mnamidomo kama man United
 
Alichosema PEP juu ya Ugumu wa Chelsea

"Why Chelsea play so good… because they have three central defenders close, the two holding midfielders who move in relation are close, the pockets are close, the striker and the two [others in attack] are so, so close," Guardiola said to BT Sport.

"The distances are so close, and at the same time they are so wide with the wing backs, they are so good with the ball in behind.

"That’s why you cannot be close because they push you [out wide] and they have a lot of good players in the middle. That’s why it’s difficult to face teams who want the ball and want to play with the ball. We’ve tried to do it since day one."

Video yake hii hapa

 
Sikufungua huu uzi kosoma au kuchangia chchote tangia tufungwe Fainal ya FA!

Napenda kuwatakia Heri njema sana Mashabiki wenzangu wa Chelsea katika Final nyingine ya Leo UCL

Sijui kwann Moyoni nina Amani sana tena sana Na Final hii ya Leo, sijawa na hofu kbsa.

Tuipende timu yetuu
 
Nasikia John Terry amewahi nafasi kule Porto kuishuhudia Chelsea ikibeba ndoo kama alivyofanya 2012 tofauti safari hii akiwa sio mchezaji wa Chelsea
1622296111445.png
 
Timo Werner hafungi na anakuwa hatari hivyo je angekuwa anafunga ingekuwaje?

Azpilicueta on Timo Werner

“But Timo’s overall contribution to the team; the runs he made, the penalties he won, and the assists he got, has been massive.

“Of course, as a striker, he would like to score more goals — and it’s important that he has this desire, this ambition.

“It has been his first year at Chelsea and tomorrow [in the Champions League final], he is [going to be] an important player for us.

“He can threaten [Manchester City’s defensive] line and make the difference up front.”

1622296663434.png
 
Eeeh Mungu wa Isaka, Ibrahim na Yakobo tunakuja mbele kwa unyenyekevu tunaliweka chama letu THE BLUES mikononi mwako bwana.

Wachezaji tunawaweka mikononi mwako bwana, kama jemedari wa vita ukawaongoze kushinda hii vita iliyoko mbele yetu dhidi ya CITY, wakapambane kwa akili na moyo mwisho wa filimbi tukabebe hili kombe na kuandika historia nyingine katika ulimwengu wa mpira.

THE BLUES in GOD WE TRUST.

Amen

Tukutane baada ya mechi.View attachment 1801274
Ameni 👏👏
 
Sikufungua huu uzi kosoma au kuchangia chchote tangia tufungwe Fainal ya FA!

Napenda kuwatakia Heri njema sana Mashabiki wenzangu wa Chelsea katika Final nyingine ya Leo UCL

Sijui kwann Moyoni nina Amani sana tena sana Na Final hii ya Leo, sijawa na hofu kbsa.

Tuipende timu yetuu
Upo kama mimi aisee
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom