CHELSEA 4-4 AJAX, Champions League: Post-match reaction, ratings
By Mlanzi
Ngoja nianze na Reece James raia wa England ambae anaupiga kama professional player na nafasi yake uwanjani ni full back. Mwezi December tarehe 8, mwaka 1999 ndio alizaliwa pale London Borough of Redbridge, United Kingdom, na sasa ametimiza umri wa miaka 19. Bao la Reece James ndo bao lililoturejesha kileleni katika ile comeback ya kihistoria dhidi ya Ajax.
Kabla sijasahau, first half Ajax walikuwa 3-1 huku wakiwa na shuti moja tu on target, meaning sisi tulikuwa tumejifunga mabao mawili yani 2 own goals.
Zile red cards mbili kwa Ajax zote zilikuwa sahihi kabisa, Tadic alimchezea leg breaker Tammy Abraham na Veltman alikuwa ameushika mpira ndani ya box kosa linalozaa yellow card na penalty juu. Tunahaki ya kujipongeza kwa hii comeback japo tulikosa umakini katika first half. Marcos Alonso ameniangusha kile kiwango hakikuwa cha UEFA Champions League alionekana kuwa chini sana.
Second half ilikuwa powa sana na kama kawaida yetu tulikutana tena na mkono VAR baada ya bao safi kutoka kwa Cesar Azpilicueta kukataliwa kwa kile kilichodhaniwa kuwa handball kutoka kwa TammyAbraham. Hii ilikuwa moja kati ya zile crazy game.
Ndani ya dakika 90+ mambo mengi sana yalijitokeza. Kwanza own goal kutoka kwa Tammy Abraham ndani ya dakika mbili za mwanzo. Pili, Christian Mate Pulisic kushinda penalty iliyotiwa kambani na Jorginho ndani ya dakika tano za mchezo. Tatu, Tammy Abraham kutupia kutokana na through ball ya Mateo Kovačić na bao kukataliwa kutokana na kuwa offside.
Nne, Ziyech wa Ajax kufunga bao tamu kwa njia ya freekick kutoka upande wa kulia mwa uwanja na Kepa Arrizabalaga kujifunga wakati akiokoa.
Tano, Marcos Alonso kupumzishwa half na Reece James na kumfanya Cesar Azpilicueta kuhamia katika left back.
Sita, Kurt Zouma kufanya Maradona-esque style kwa kukimbia na mpira umbali upatao 70-yard na kukosa kosa kufunga.
Next up tutawakaribisha Crystal Palace pale Stamford Bridge katika Premier League siku ya Juma Mosi
KTBFFH