Troublemaker
JF-Expert Member
- Jun 8, 2015
- 19,882
- 38,512
Newcastle wana kipa mkuu aisee acha mchezo yaani kipa kawasave sana kulikuwa na goal 3 jana pale basi tu.Nilichokiona game yetu ya jana Vs Newcastle.
Hawa jamaa ni wagumu sana kuanzia back line yao kiungo mpaka washambuliaji kiukweli wakati game inaanza nilikua sifikirii kama tutapata clean sheet though nilijua ushindi tutapata. Kiuchezaji kwa kuangalia mfumo wao waliingia na 5-4-1 yan nadhan walijidhatiti kuja kutafuta point darajani kama siyo ushindi basi draw ukizingatia na sisi mfumo tuliotumia 4-3-3 na ndio maana tulimiliki mpira lakini bado ilikua ngumu kuwafunga kwa sababu ya solidness ya back yao.
Upande wetu kwenye backline naona bado kuna mapungufu japo tunazifi kuimarika. Pair anayoitaka Lampard bafo haijapatikana lakini jana Zouma alijitahidi tofauti na siku za nyuma nadhani majeruhi wakipona wanaweza kuwa msaada. Mwisho naomba niwe wa kwanza kusema Barkley auzwe January, CHO anakuja kuwa mchezaji hatari EPL, Pulisic the best is yet to come, wengine wote tunafahamu shughuli yao.