Chelsea FC (The Blues) | Special Thread

Chelsea FC (The Blues) | Special Thread

Asante Mkuu, poleni wazee wa namba SITA, Kocha Mourinho kaishiwa mbinu, kila siku anagombana na kuwavunja moyo wachezaji, mtapata shida sana na huyo kocha
Japo kaishiwa mbinu ila naamini bado msimu ujao watakuwa vizuri zaidi ya msimu huu. Kikubwa ambacho nadhani Mourinho anakosea ni hawezi kutengeneza mahusiano mazuri na wachezaji
 
[Colour=blue]Kwa kweli sifa zimuendee Conte kuingia kwenye ligi na kubeba ndoo siyo mchezo aisee Amefanya kazi kubwa SANA kurudisha kiwango cha Pedro Kiukweli huyu ni yule Pedro wa Barca wa mwanzo kabisa, kwa upande mwingine niwape sifa zinazostahili HAWA wachezaji watano(5)..

1=DAVID LUIZ huyu amefanya kazi kubwa akiwaongoza wenzake ktk safu yote ya Ulinzi Hongera sana..

2=MARCOS ALONSO Huyu Tangu Conte alivyobadili mfumo na kutumia 3-5-2 and 3-6-1Huyu Amekuwa nguzo kubwa sana kati ya nafas ya ulinzi na kiungo...

3=KANTE huyu mnyama sina mengi ya kumuongelea hadi FA wenyewe walimuona na kumpatia tunzo ya mchezaji Bora Amefanya kazi kubwa akiwa na thaman ndogo ukimlingananisha na yule PogHairstyle na thaman yake kubwa ya mabilion Alichokifanya Kante Kilitarajiwa kifanywe na pogba hii Imedhihirisha wakati mwingine Kuwa na pesa nyingi cyo kupata mafanikio na Dunia haijawahi kuwa sawa siku zote...

4=VICTOR MOSSES Huyu MTU amekuwa Lulu Nadhani anaeumia sana ni mourinho alimdharau na kumuona hafai na kumtoa kwa mkopo hadi anaondoka darajani Lakini Conte kafanya kazi kubwa sana Huyu MTU kwa msimu huu amekuwa mwiba mkali upande wa kupandisha team na mambo mengine siku alizokosekana kulionekana kupwaya sana upande huo Hongera kwa huyu mnyama Kafanya kazi kubwa sana.

5=HAZARD Huyu MTU kwa msimu huu kawa mpya amezitesa sana safu za ulinzi za team Pinzani kwangu Mimi kwa kazi aliyoifanya simudai kabisa licha ya kwamba mwakani Tunamhitaji ktk kutengeneza team ya ushindani ktk UCL lakini hata Akiondoka kwenda Madrid au kwingine kwangu Mimi simudai kabisa na nitamtakia kila Lakheri Hongereni sana Mashabiki wenzangu wa Chelsea Ubingwa wetu wa 2015 tuliowaazima Leicester mwaka Jana, Leo Umerudi Ahsante sana Conte[/color]
Big up the bluus
Ila inaonekana darasa la rangi bado hujalielewa vizur
 
762e3f6fc723e4c5fb76996ebced653e.jpg
 
Ferguson alisemaga Chelsea hata top four hanusi, aibu yake sasa!
Jana baanda ya chelsea kutawazwa mabigwa. Pole sir Alex Ferguson bora ungebaki kimya bila kutoa utabiri wako kama kina ya malafyale. Naamini popote ulipo unaugulia maumivu makali sana. Ndo mpira. Ahsante wachezaji wote wa chelsea, kocha na washabiki kwa ujumla pamoja na kubezwa na kutopendwa kila kona ya dunia mmeonesha kuwa chelsea siyo timu ya kubezwa.
dfc28e7e4812fdf3c4e182e6eb301637.jpg
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom