Chelsea FC (The Blues) | Special Thread

Chelsea FC (The Blues) | Special Thread

Schuller alishauzwa kwa Wolfsburg ya Germany.Mourinho kama kawaida yake haonagi mbali, ni kocha wa kudonoadonoa na kubahatisha. Dogo Schuller ni mbaya ila Mourinho hakuwa anampa nafasi sababu sio defensive minded mpira anaochezesha Mourinho

Schurle kumbe kauzwaaa!!!!!?????? Dah, kweli majanga, yule jamaa akiingiaga anajua kuji-position vibaya sana na huwa ni mwepesi ktk ufungaji akiingia kipind cha pili.
 
Hata mimi nimefurahi sana Chelsie kutolewa,Arsenal na Man city nao wanafuata safi sana
 
Aaaaah Mourinho can you ni jinsi nilivo na furaha kwa chelsea kutoka?
Game ya jama acha kabisa bhanaa, Chelsea walivyo wajinga hata mashambulizi hawakuwa wakifanya.

Hahahahahahaaa, si huwa ukikutana nao hawa wanakusumbua na star man wenu hajawahi ona lango la chelsea, au uongo?
 
Tatizo jingine linalotukabili ni kutokuwa na spirit ya kumaliza mchezo (hili hata Fabregas alilisemea)

Mara nyingi sana tunapopata goli tunapunguza kasi ya kushambulia, ingawa jana tulijaribu kuendelea kushambulia lakini si kwa kiwango kinachotakiwa.

Tulikuwa na uwezo wa kufunga magoli hata manne (4) kama tungetumia nafasi vizuri, tuliingia mara nyingi sana kwenye eneo lao lakini hatukuweza kufunga, sikuona jitihada kubwa za kutaka kufunga isipokuwa kwa Hazard pekee.

Huyu Costa ndio nimekuwa simuelewi kabisa, sijui kapatwa na nini. Nadhani tunahitaji mshambuliaji zaidi ya Costa.

Jana kama tungekuwa na safu nzuri ya ushambuliaji tungepata magoli mengi maana uwezekano huo ulikuwepo.

Kwa jinsi tulivyocheza, kutolewa UEFA ni sawa tu maana hatukuwa wazuri kiasi cha kuweza kuvuka round hii, ukizingatia timu tuliyokutana nayo, maana hata kwao yale matokeo yalikuwa ni bahati kwetu.

Matatizo yetu ni mawili tu yaliyotugharimu, na huwa yanatugharimu sana tu, na yataendelea kutugharimu kama yasipofanyiwa kazi.

1. Udhaifu katika kudefence mipira ya kutenga

2. Safu ya ushambuliaji kutokuwa na uchu wa kufunga magoli mengi. Huwa tunabweteka.

Mimi binafsi naamini jana tulitolewa si kwa sababu PSG walikuwa wazuri sana bali ni ujinga wetu wenyewe, aliyetazama mpira vizuri ataniunga mkono.

#FOREVER BLUE
 
Ni kweli, kama timu zote za Uingereza zitatolewa nafasi yake ya kuingiza timu nne CL na nafasi hiyo itachukuliwa na Ufaransa. Nchi tatu tu ndo uingiza club nne CL na mara nyingi nchi za Uingereza, Hispania na Italy ndo waliokuwa na hiyo chance kwa sababu timu zake kufanya vizuri kila msimu. Lakini kuanzia 2011 nafasi ya Italy ilichukuliwa na Ujerumani baada ya timu zake kuanza kuboronga kwenye michuano hii. Kwahyo timu Asernal na Man U kaeni chonjo maana mtaanza kugombania big 3 na sio big 4 tena😛

hii sheria unatunga chumbani kwako ?
uwe unauliza basi ili ueleweshwe
 
Root mkuu pita hapa,,
1. Tatizo la kipa lipi hasa!? Unasema tukishaongoza goli moja tunakua tunashambuliwa sana, Je hill ni tatizo la Thibout!? Ninavoona Mimi kipa ANATUBEBA SANA TENA SANA ila yy kama yy anatema sana mipira, ila tatizo kubwa sana lipo kwa mabeki hawa WASHAKAJI ZETU wanatuangusha sana hawafanyi marking za kueleweka iwe ni Zonal au man2man.. Mfano goli la 2 PSG poor marking ile tena sana.. Pale kwenye mwamba palitakiwa kuwa na mtu pale...

2. Mabeki sijui wamechoka au ni mini? JT ule ni uzee inabidi apate mbadala wake, cahil kasi imepungua kidogo hapa karibuni, JT ni mzoefu lakn kumuachia akabe kwenye gemu kama ya Jana tungeabika zaidi kama cadabra asingetolewa.. Ivanovic ni iron man anatubeba, full back ya kushoto si vibaya wakipokezana na fillipe sasa...

3. Midfield, hawa wanatubeba sana ila Jana matic na fabregas WALIPOTEA HASA FAB.. OSCAR HUyu dogo mrembo bado has a gemu kubwa William inabid awe anaanza tu bwana, Hazard safi...

Costaaaaaah... Hahahahahah hapa ndo utajua tofauti ya EPL NA LA LIGA, jamaa kachoka kama anakula kiepe na kutrain kwa nusu SAA.. EPL ngumu wazee ina mabeki wakatili sana,, REMY MWENYEWE BADO Labda coz ya bench... Tunahitaji mshambuliaji halisi pale mbele.. Afu pia kucheza 4-2-3-1 kwa Costa hapana tutaaibika sana... ROHO INANIUMA SANA
 
Mourinho siku hizi ni mfanyabiashara mzuri kuliko hata Wenger,Schurle hakupaswa kuuzwa alikuwa mfungaji mzuri hasa akitokea sub,hakukuwa na sababu ya kumuingiza Drogba mwenye miaka karibia 40 kwenye game ngumu kama ile.Hana ile kasi na nguvu za miaka ya nyuma

Hana akili ya kibiashara kama Wenger. Anajaribu kuiga.
 
Hapana mkuu
Diego Costa inabidi sasa awe benched maana hizi ndiyo mechi anazo stahili abebe team lkn yy huwa anapotea

Hajafunga mechi ya ngapi sasa?
Toka mid January.. Maana lile dhidi ya Tottenham sio lake ni OG
 
Hata mie nikipewa karatasi ya kupiga kura nitaandika mara mia tisa aondoke huyu jamaa maana mbinu zake ni za kipuuzi sana. Uzuri boss alikuwepo kaona kilichotokea. Kaumia so mwisho wa msimu tutajua kitachotokea. Mou maneno mengi hakuna vitendo kabisa
Abramovich haujui mpira yule.. Anafurahi kuona timu inashinda na kupiga vipasi tu lakini mambo ya ufundi hana anachojua
 
Umesahau the Gunners. Anajua hauamini...!!
Kama hiyo ni timu yako, subiri wafaulu mtihani wa Monaco.
Sikuisahau, Arsenal haina kikosi cha kuchukua ubingwa wa CL. Si timu iliyo serious, haitabiriki na haina kiongozi uwanjani.
Arsenal inacheza mpira wa kupendeza wakati zingine, (chenga twawala), ina wachezaji mmoja mmoja walio wazuri lakini haijajijenga kama timu imara, timu kisiki.
Hata hivyo Arsenal, Man City, Liverpool wanaweza kutwaa EPL la msimu huu.
 
Mourinho


Unajua mkuu Matic aliumia siku ya fainal pale walipokua wanashangilia....aliumia enka...na mpk jana kulikua na hatihati asicheze na ndio maana Mou ktk mechi na WestHam Utd aliendelea kumpanga Zouma ktk nafasi ya kiungo mkabaji na jana Matic aliumia ndio sababu ya yeye kutolewa na kuingia Zouma na wakati huo ukumbuke na Obi na yeye ni majeruhi. Sasa ktk hali km hiyo kwanini asimuingize Zouma ktk hiyo nafasi?

Wengi kitendo cha kuingia Zouma wanona km Mou alikosea lkn hawajua km Matic na Obi ni majeruhi....
 
Last edited by a moderator:
successor

Hapa mimi nataka kumzungumzia Costa peke yake, Kabla ya mpira jana Laurent Blanc alinukuliwa na vyombo vya habri akisema kua amewambia wachezaji wake kua wawe makini na Costa na wasimunigie mwilini au kumgusa hovyo kwamba wakifanya hvyo wanaweza pata matatizo, lkn kwa jana km uliangalia mpira hii kauli ya LB inaweza kua kweli?

Jana PSG hasa mabeki na kina Motta walikua wakimfanyia Costa vituko na michezo mibaya makusudi mpk anatoka Ibra, Huyu Costa alikua ameshapigwa viwiko mara mbili bila mwamuzi kuamua chochote. alafu bado hawa PSG walikua wakiendelea kumchezea hovyo tu yote hii ni kumfanya Costa asicheze mpra na haya ni maagizo kutoka kwa LB na unatakiwa ufahamu kwamba ukimtoa basi adui yako anakua kafaulu mpango wake.

Mpira jan ulikua ni mbovu tu kowa timu zote.
 
Last edited by a moderator:
Mkuu Ntuzu umeiona hii!?


After Chelsea's players were described as "babies" by PSG striker Zlatan Ibrahimovic, several memes depicting John Terry and his team-mates as young children have been shared across social media.

_81613409_chelsea.jpg

One of the images created after Ibrahimovic's description of Chelsea players
 
Last edited by a moderator:
Wacha1 ni sawa na kumcheka mfungwa anaye nyongwa leo wakati ww pia unanyongwa kesho

Kibaya zaidi akina Ntuzu wametolewa na team nzuri lkn Arsenal wanatolewa na Monaco

Very shame
 
Last edited by a moderator:
Hapa mimi nataka kumzungumzia Costa peke yake, Kabla ya mpira jana Laurent Blanc alinukuliwa na vyombo vya habri akisema kua amewambia wachezaji wake kua wawe makini na Costa na wasimunigie mwilini au kumgusa hovyo kwamba wakifanya hvyo wanaweza pata matatizo, lkn kwa jana km uliangalia mpira hii kauli ya LB inaweza kua kweli? Jana PSG hasa mabeki na kina Motta walikua wakimfanyia Costa vituko na michezo mibaya makusudi mpk anatoka Ibra, Huyu Costa alikua ameshapigwa viwiko mara mbili bila mwamuzi kuamua chochote. alafu bado hawa PSG walikua wakiendelea kumchezea hovyo tu yote hii ni kumfanya Costa asicheze mpra na haya ni maagizo kutoka kwa LB na unatakiwa ufahamu kwamba ukimtoa basi adui yako anakua kafaulu mpango wake. Mpira jan ulikua ni mbovu tu kowa timu zote.

Acha kutokwa povu,mmeishiwa.
 
BAK;


Mkuu BAK nimeiona hiyo na nimemsikia Ibra akisema hivo ktk mahojiano lkn hii imedhihirisha na kuthibitisha kauli ya Mou ktk madai yake kua hawa jamaa ni Aggressive.

Kwa kifupi Ibra kakosea sn maana ameonyesha dharau sn na kutoa kauli za maudhi............
 
Last edited by a moderator:
  • Thanks
Reactions: BAK
Schuller alishauzwa kwa Wolfsburg ya Germany.Mourinho kama kawaida yake haonagi mbali, ni kocha wa kudonoadonoa na kubahatisha. Dogo Schuller ni mbaya ila Mourinho hakuwa anampa nafasi sababu sio defensive minded mpira anaochezesha Mourinho

Na shurle anawasaidia sana wolfsuburg hawashkiki sasa hv.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom