Heheheh mkuu naona ulikuwa umeegesha gari unasubiria kipenga cha mwisho tuu....Masanilo simu haina 'chaji', Invisible lazima atangaze System Maintenance usiku huu.
Watani poleni kwa kichapo..ndio ukubwa!!
Hodi wenyewe,mpo??,naombeni matokeo TANESCO wamenikatia umeme
ha ha ha ha mkuu matokeo ni 2-1 huku adebayor akifunga magoli ya pande zote mpaka half time.kipindi cha pili kamanda tevez akamaliza kazi huku shujaa wamchezo akitokea kuwa GIVEN baada kudaka penati ya lampard.Hodi wenyewe,mpo??,naombeni matokeo TANESCO wamenikatia umeme
Hatujakimbia jamani, tupo! Mechi kama hii inaangiliwa pub, hivyo ngumu kuwa online hapa JF for some reasons! Anyway,
naona wamekubali jukwaa litekwe ha ha ha.kama namuona masanilo aki -refresh page kwenye simu yake huku akipata bei na kushindwa aandike nini ha ha ha.
Kumbe mnajua kwamba mezhi zaangaliziwa pub eeh,maana sie tukipotea pale Ashburton Grove mara tunapocheza huwa mnachonga sana kwamba ooh tumekimbia tumekimbia...Masanilo uli hale???
Kwi kwi kwi ....kazi ipo! Tupo pamoja mkuu, japo mambo ya weekends ndio kama hivi, usiku unaingia taratibu na watu tunatoka kwa kasi!Lazima waingie mitini maana wao ndio wanaongoza kwa kuwa-nanga wenzao wakifungwa ata kwenye mechi za Carling Cup.
Nimekubali mkuu,m leo tulikuwa hovyo, hasa finishing! Hao jamaa wa Manchester wanakutana nusufaili ya Carling cup.Man City wamecheza mpira mzuri sana leo, sikujua kama hao jamaa huwa wanakipiga kipute kwa nguvu na kasi kiasi hiki.
Bao la Chelsea asingekuwa Adebayor leo ingekuwa 2 - 0. Ukitaka kujua kama timu imeelemewa angalia jinsi wanavyocheza rafu, maana mwanzo Refa alivumilia mwisho akaona imezidi ikabidi mvua za yellow card zianze kunyesha.
Shujaa wa mechi alikuwa Given, maana ile penalty kama ingeingia basi wangetoka ngoma droo. Huyo ndiye aliyewanyenyua Man City wakatoka 2 - 1.
All in all, leo Man City wamenitisha sana na nimewaogopa na kuwaheshimu. Si mshabiki wa Man City wala Chelsea lakini ukweli unabaki pale pale kwamba Chelsea walizidiwa game leo. Hawakufurukuta kabisa.
Fainali ya Carling Cup kama Man U watakutana na Man City, basi kuna kazi ya ziada. Maana ninaona kuna dalili zote za SAF kuanza kufukuzia makombe mengine ili asije akatoka mwaka huu, na hiyo mechi inaweza kuwa ngumu, kali na yenye ushindani wa kutosha. Siku hiyo SAF hataweka wale chekechea wake, itabidi aweke kikosi kamili.
Poleni sana Chelsea, angalau Man City amekuwa speed governor amewapunguza kasi yenu kwa kiasi kikubwa sana.
Masanilo yuko wapi jamani??,I.C.U nini?????????