jingalao
JF-Expert Member
- Oct 12, 2011
- 35,053
- 28,245
Wasalaamu wanaJF
Herini ya Krismasi na maandalizi ya funga mwaka 2023.
Leo tena ninarudi jamvini nikija na ushauri kuntu kwa wizara zote zinazohusika na afya pamoja na wadau wa sekta ya afya.
Utambulisho
Nirejee kwa kujitambulisha kuwa kwa miaka kadhaa kama raia, mwanaJF, mdau wa maswala ya siasa, mdau wa maswala yanayolalamikiwa na wananchi, mdau wa Sera mbalimbali za nchi, mdau katika sekta ya afya ,mdau wa bima ya afya kwa wote,mdau wa afya ya msingi kwa wote, mdau korofi wa kuona Tanzania inajitegemea katika maswala ya afya lakini pia mzalendo asiye na simile/smile inapokuja suala la uhuru kamili wa Tanzania bila msaada wa walami.
#MWANZO WA HOJA YANGU#
Wakati tunapata uhuru mwalimu Nyerere alitupa muelekeo wa kupambana na maadui watatu muhimu ikiwemo Ujinga,maradhi na umasikini.
Hadi leo bado kama nchi tunayo dira,mipango na mikakati dhidi ya maadui hawa watatu. Kwa kiasi kikubwa Serikali, viongozi wa siasa na jamii wameshirikiana na wananchi katika kukabiliana na maadui hawa kwa ufanisi mkubwa na KAZI INAENDELEA.
Nikijikita katika adui maradhi ni wazi kuwa kumekuwepo na Mabadiliko muhimu mbalimbali yaliyoashiria utekelezaji wenye matokeo.Zaidi tumejionea utekelezaji mkubwa wa kimatokeo hususani katika kipindi cha miaka 7 ya hivi karibuni japo mabadiliko hayo hayana msingi au egemeo la kisiasa(kisera), nasema hivi kwa kuwa bado tuna sera ya afya ya mwaka 2007 mwezi juni.
Kwa muktadha huu tunaweza kuwa tumepiga hatua kubwa bila kuwa na idhini au baraka za kisera. Aidha natambua kuwa Tuna sheria iliyoanzisha mfuko wa bima ya afya ya Taifa (NHIF) kama sikosei ilianza 1999 na marekebisho yaliyofanyika mara kwa mara. Kama nikirejea sawasawa mojawapo ya majukumu ya chombo hiki (kumbukumbu zangu tu zinaniambia niliwahi kusoma sehemu) ni kusimamia utekelezaji wa bima ya afya kwa wote.
Pia niseme kwa maoni yangu kuwa moja ya jukumu la NHIF la kuikuza bima ya afya kwa wote lilishindwa kutekelezwa hadi tukafikia hatua ya wadau wengine au vyombo vingine kuingilia kati.
Nirejee kuipongeza Serikali chini ya Wizara ya Afya na OR TAMISEMI kufikia hatua kubwa ambayo imepelekea kuwa na Sheria ya bima ya afya kwa wote hivi karibuni ambayo inasubiri kutengenezewa kanuni.
VURUGU ZA NHIF KWA SASA
Wakati wadau, wizara za kisekta na za utekekezaji, wanufaika na wananchi wakisubiri maekelekezo mujarabu ya utekelezaji wa sheria ya bima ya afya kwa wote naona NHIF wakijitoa ufahamu iwe kwa kupangwa au kwa kupotoka au vyovyote vile wakiibua sintofahamu katika jamii. Yaani wameibuka na Price list ya huduma watakazogharamia kwa level mbalimbali za huduma bila kuwashirikisha wadau hususani wa afya na wanaotoa huduma za afya.
Kwangu mimi hii naona ni vurugu na pengine ni hujuma dhidi ya sheria hii iliyopita kwa shida na mashaka mengi.
kuna kipindi niliwalaumu waheshimiwa wabunge walivyokataa kuipitisha ila kwa sasa nawaelewa kwa nini walikuwa na mashaka!pengine walipata hisia chafu ya kutengwa kwa mwananchi wa kawaida katika utekelezwaji wa sheria hii.
MAONI NA USHAURI WANGU KWA NHIF/WIZARA YA KISEKTA
-Kwanza kabisa NHIF ijiondoshe na kujiepusha kimkakati (strategic retreate) katika utekelezaji wa mchakato wa bima ya afya kwa wote.NHIF ijiweke kama mdau anayetakiwa kupangwa na kupangiwa katika utekelezaji wa sheria hii mpya, sio kwa ubaya bali kwa maslahi mapana ya wanufaika wote.
-Utungaji wa kanuni na mchakato wake usimamiwe na wizara ya Afya kwa kushirikisha kikamilifu Ofisi ya Rais Tamisemi, Ofisi ya Waziri Mkuu,Wizara mtambuka, Mikoa na Halmashauri sekta binafsi, bunge na jamii kwa ujumla.
Hapa namaanisha USHIRIKISHAJI KAMILIFU na sio semina za kisanii.
-NHIF isitishe michakato yake ya price list inayotarajiwa kuanza mwezi januari 2024 ambayo inakiuka mikataba waliyoingia na watoa huduma ...hii inaangazia na kuakisi maswala ya kibajeti na kisheria ya taasisi mbalimbali ambazo ziliingia mikataba na NHIF.
-Wadau wote wanaohusika waratibiwe kuandaa mapendekezo (yawe kimaandishi) ili yawasilishwe kwa wizara ya afya ili kuunda kanuni za utekelezaji wa sheria ya bima ya afya.
-Ni vyema na ikibidi wizara ya Afya ipeleke bungeni kanuni hizo kwa maridhiano kamilifu ya utekekezaji.
-Wizara ya Afya itambue kuwa Afya kwa kiasi kikubwa inaanzia ngazi ya jamii,zahanati,vituo vya afya ,hospitali za wilaya halafu ndio hospitali za mikoa, kanda na kitaifa.wadau muhimu wa afya wapo ngazi ya msingi na sio ngazi ya rufaa. Wananchi na wagonjwa zaidi ya 80% wanaanzia au wanafaidika na afya ya msingi na sio vinginevyo.
Heri ya Krismasi na mwaka mpya.
KWA HISANI YA MTU WA TANZANIA!