KwetuKwanza
Member
- Mar 13, 2023
- 34
- 82
BARUA KWA WAZIRI WA AFYA
09/10/2023
YAH: - KUOMBA KUJUA UAMUZI WA WIZARA YA AFYA DHIDI YA MALALAMIKO YA MADAKTARI WATARAJALI.
Kwako Ummy A. Mwalimu, Waziri wa Afya.
Tunakusalimu kwa jina la Jamhuri.
Kwanza tuanze kwa kukupongeza kwa juhudi zako mbalimbali za kuliwajibikia Taifa ili lipate kuwa na afya njema itakayowezesha kuijenga Tanzania yetu.
Waziri, tunatambua una majukumu mengi sana kwa ajili ya ujenzi wa Taifa letu, hata hivyo tunaendelea kukupongeza kwa kutambua sehemu muhimu ya jukumu lako hata ukaamua kuunda Kamati ya Uchunguzi kwa ajili ya kufuatilia malalamiko yetu dhidi ya Baraza la Madaktari Tanganyika (MCT) na dosari zilizopo kwenye mtihani wa Pre na Post Internship kupitia barua yako ya tarehe 14/08/2023.
Waziri, tunatambua kuwa zoezi la uchunguzi liliendeshwa na Kamati kama ulivyoagiza na ni matumaini yetu kuwa zoezi hilo lilikamilika kwa wakati.
Mheshimiwa Waziri, leo tumeamua kukuandika barua ili tupate kusikia neno kutoka kwako kwa kuwa tulihitaji msaada kutoka kwako na kwa Serikali yetu Tukufu ili tupate kuwa na mtihani usiokuwa na dosari nyingi.
Bahati mbaya, sisi Madaktari Watarajali hatukuwa na mwakilishi ndani ya Kamati uliyokuwa umeiunda na hivyo hatujui chochote au hatujui hatua iliyofikia Kamati au Wizara katika kutafuta ufumbuzi wa malalamiko yetu.
Waziri, kwa kutambua umuhimu wako na sisi jitihada zetu kugonga mwamba kutaka kujua hatua iliyopo katika kuyafumbua malalamiko yetu, kwa kuwa kumekuwa na ukimya mkubwa na sasa ni takribani inakaribia miezi miwili hatujui chochote kinachoendelea dhidi ya malalamiko yetu na msaada tunaoutazamia kutoka kwa wizara.
Tumeamua kuchukua hatua hii ili kukuomba utuweke wazi juu ya uamuzi wa Wizara yako kwa namna ya kutusaidia ili tuweze kuondoka na kipindi kigumu cha maisha na kusumbuliwa na msongo mkubwa wa mawazo unatukabili sisi Madaktari Watarajali.
Waziri, hata hivyo hatutakoma kukuomba msaada wako uzingatie pia barua yetu iliyoainisha dosari, maoni na maombi yetu ili walau tusaidike kupitia ‘panel assessment’ kwa kuwa si hospitali zote zilikuwa na ‘logbook’.
Ahsante na tunakutakia majukumu mema.
Madaktari Watarajali