CHADEMA wahaha kusaka mgombea urais 2015

Wadau, ni dhahiri kuwa CHADEMA sasa hakijiwei tena na kimechoka hadi huruma.

Kwa ujumla ni kwamba, CHADEMA hawana mtu mwenye sifa, uwezo wala hadhi kuweza kukiwezesha chama kupata angalau asilimia 10 ya kura za Rais. Tegemeo lao hapo awali lilikuwa kwa Dr Slaa. Hata hivyo, imedhihirika kuwa kwa sasa Dr Slaa hana mvuto tena na kama chadema wataamua kiubishi ubishi kumsimamisha kugombea, hakika wataangukia pua kabisa. Hadhi ya Dr Slaa kwa sasa imeshuka sana na wataalam wa masuala ya kisiasa wanasema kuwa asipojiangalia mwisho wake utakuwa mbaya zaidi. Kushuka kwa hadhi kwa Dr Slaa pamoja na mambo mengine kumeelezwa kuwa kumetokana na kitendo chake cha kupanga, kuratibu na kusimamia mpango wa kumng'oa Zitto Kabwe kwenye chama hicho. Wachambuzi wa masuala ya kisiasa wanasema kuwa uwepo wa wanasiasa nguli kama Zitto Kabwe na wasomi mahiri kama Dr Kitila Mkumbo na wapanga mikakati kama Samson Mwigamba kulikiwezesha chama hicho kuaminiwa na wananchi wengi. hata hivyo, baada ya maamuzi ya kuwafukuza akina Zitto, imeelezwa kuwa wafuasi wengi wa chama hicho wameamua kurejea CCM huku wengine wakijiunga chama kipya cha ACT Tanzania. Freeman Mbowe anayo tamaa ya kugombea urais. Hata hivyo tatizo kwake ni Elimu. Mbowe hana elimu ya Shahada inayohitajika kwa mtu kuteuliwa kuwa mgombea Urais.

Blan B ya CHADEMA katika kupata mgombea mwenye sifa ni kuangalia ndani ya mahasimu wao wakubwa kisiasa, Chama cha Mapinduzi ambacho kimesheheni wanasiasa nguli vijana kwa wazee ambao ni Presidential Materials. Target yao kubwa ni wanasiasa wanaotoka mikoa ya Kaskazini na kanda ya Ziwa. Hapa CHADEMA wamekuwa kama fisi ambaye anangojea mkono wa binadau udondoke ili auokote. Lakini wapiiii! CHADEMA nao wanafuata matendo ya fisi. Wanasubiri CCM wateleze hasa katika mchakato wao wa kumpata mgombea urais. Inadaiwa kuwa CHADEMA wanamuangalia sana Edward Lowasa. Kwao wanamuona kuwa Lowasa ni mtu ambaye atakisaidia chama chao kushinda urais wa 2015. Wao wanaamini kuwa LOWASA atatemwa na chama chake kwenye kinyang'anyiro cha urais kitendo ambacho kitasababisha EL ahame chama chake na kujiunga na CDM. Inadaiwa kuwa tayari CHADEMA wamewasilisha mpango wao kwa EL. Hata hivyo, taarifa za ndani zinasema kuwa Lowasa amewaambia live kwamba ikiwa ataamua kugombea urais, basi itakuwa ni kwa tiketi ya CCM kauli ambayo imewakatisha tamaa sana. Baada ya kugonga mwamba kwa Lowasa, inaelezwa kuwa Sumaye na Mama Anna Kajumulo Tibaijuka ni miongoni mwa wanaopendekezwa na Mzee wa Tengeru katika nafasi ya Urais.

Plan C ya CHADEMA ni kuanzisha muungano fake na vyama vingine vya siasa. Kwa kuanzia wameunda umoja ujulikanao kama UKAWA. Ingawa umoja huo lengo kuu ni kupigania Rasimu ya Katiba ya Jaji Warioba, inaelezwa kuwa lengo kuu ni kuwahadaa wanasiasa mahiri wa vyama vingine kama akina Prof Ibrahim Lipumba na James Mbatia. Hapa CHADEMA wanajifanya sitaki nataka. Kwamba, CHADEMA wametoa matamko kuwa UKAWA itasimamisha mgombea mmoja tu katika ngazi ya Rais. Mapendekezo ya awali ni kumsimamisha Mchungaji Christopher Mtikila. Hata hivyo, inadaiwa kuwa James Mbatia, Ibrahim Lipumba na wahafidhina wa CHADEMA wamekataa mapendekezo hayo. Lipumba anadai kuwa ndani ya UKAWA, yeye ndiye Msomi na mkongwe kwenye siasa kuliko wote. Hivyo amewapa masharti kwamba ikiwa UKAWA wataamua kusimamisha Mgombea Urais mmoja, basi wamteue yeye kuwa mgombea. Hata hivyo mzee wa Tengeru amekataa pendekezo hilo la Lipumba kwa sababu zinazojulikana.

Kwa hali hiyo, mipango yote ya CHADEMA Yaani Plan A, B na C imekwama. Wamebaki kutapatapa tu na washauri wao akina Saed Kubenea wanaonekana kukosa kabisa mbinu za kukinusuru chama.

Nawasilisha.
Hizi ni assumptions tu ili uweze kuwachokonoa wahusika na kujuwa plani zao!Ni maswali unayojiuliza kuhusu mikakati yao, huna majibu na sasa unayatafuta.Goodluck on that!

Eti "mzee wa Tengeru alimkatalia Lipumba kwasababu zinazojulikana", as If propaganda dhidi ya chadema ni mpya ama hazijulikani?
 
ukiona mtu anakosa usingizi na kuhangaika na ya jirani yake, ujue huyo hana mapungufu, bali yeye mwenyewe ni pungufu

very weak and poor state of mind LIZABONI
Wao jamaa umempa za usso kila siku,mara chadema imekufa,mara chadema haina mgombea,ni sawa na jamaa anamwambia binti huyo jamaa hana kazi, analala chini na mgonjwa! ,Lizaboni acha siasa za chumbani lete hoja
 
Hizi ni assumptions tu ili uweze kuwachokonoa wahusika na kujuwa plani zao!Ni maswali unayojiuliza kuhusu mikakati yao, huna majibu na sasa unayatafuta.Goodluck on that!

Eti "mzee wa Tengeru alimkatalia Lipumba kwasababu zinazojulikana", as If propaganda dhidi ya chadema ni mpya ama hazijulikani?

Cheupe upo??

Sasa hizo kandambii zako nikuwekee vigozi au nusikuwekee??

Nin sasa??eeeeh.

Yale macho yangu ya kungu umeyapeleka wapi sasa.

Cheupe bana.
 
Kumbe Muungano ukiwa wa CDM na vyama vingine unakuwa Feki siyo.
Je ule wa CUF na CCM Zenji vipi sio Feki?
Umeshachukua chako? . Mjini shule jitahidi kuenendelea kufanya kazi nzuri Lumumba wasikusahau.

Mkuu, ule wa CCM na CUF si umetokana baaya ya kubadilisha katiba ya Zanzibar? Kwa maana nyingine ule unatambulika kikatiba. Sasa tujiulize huu muungano wa UKAWA umetokana na nini? Je katiba za vyama husika zimebadilishwa kuaccomodate muungano huo? Nakubaliana na Lizaboni
 
Cheupe upo??

Sasa hizo kandambii zako nikuwekee vigozi au nusikuwekee??

Nin sasa??eeeeh.

Yale macho yangu ya kungu umeyapeleka wapi sasa.

Cheupe bana.
We kitimoto bana, weupe uko wapi hapo? Teh teh teh! Pambaaf kabisa!
 
Mke wangu hujambo??

Unanitusi eeeh??

Tutakutana usiku unajua nini ninachokufanya.

Wewe si unatamba mchana tuuu.
We akili tope kabisa! Kubwa jinga si kubwa, mtoto si mtoto!Unaita kivuli mke wako? Pambaaf kabisa! Halafu labda wewe ni lijitu lenye nyadhifa unajificha nyuma ya avatar ya kikubwa jinga na mabandiko ya ki.pumbavu kabisa yanayoendana na avatar!
 
Akili ndogo!

Eti CCM imesheheni watu Wa uwezo wa kuwa rais; labda kuwa mafisadi! Just imagine Mwigulu awe rais, Au kinana awe rais, Au January awe rais, Au ridhiwani awe rais, Au Chenge awe rais, Au etc, etc, duh!
Watu wazuri Kama kina Sita ndio hamuwataki!

Chadema Ina wagombea potential wengi tu; Na sasa hivi ndani ya ukawa ndio mtatapatapa Na majungu Kama kawaida yenu
 
Nilisikia Rose Kamili atapewa nafasi ya kugombea urais kupitia CDM. Au mzee wa tengeru kamkataa EX- WA KATIBU MKUU???
Prof Safari ni reject
ndani ya CHADEMA kwa vile Mzee wa Tengeru hamtaki kutokana na sababu
zinazojulikana. Lissu ndo kabisaa. Hafai kabisa kugombea urais
 
Wadau, ni dhahiri kuwa CHADEMA sasa hakijiwezi tena na kimechoka hadi huruma.

Kwa ujumla ni kwamba, CHADEMA hawana mtu mwenye sifa, uwezo wala hadhi kuweza kukiwezesha chama kupata angalau asilimia 10 ya kura za Rais. Tegemeo lao hapo awali lilikuwa kwa Dr Slaa. Hata hivyo, imedhihirika kuwa kwa sasa Dr Slaa hana mvuto tena na kama chadema wataamua kiubishi ubishi kumsimamisha kugombea, hakika wataangukia pua kabisa. Hadhi ya Dr Slaa kwa sasa imeshuka sana na wataalam wa masuala ya kisiasa wanasema kuwa asipojiangalia mwisho wake utakuwa mbaya zaidi. Kushuka kwa hadhi kwa Dr Slaa pamoja na mambo mengine kumeelezwa kuwa kumetokana na kitendo chake cha kupanga, kuratibu na kusimamia mpango wa kumng'oa Zitto Kabwe kwenye chama hicho. Wachambuzi wa masuala ya kisiasa wanasema kuwa uwepo wa wanasiasa nguli kama Zitto Kabwe na wasomi mahiri kama Dr Kitila Mkumbo na wapanga mikakati kama Samson Mwigamba kulikiwezesha chama hicho kuaminiwa na wananchi wengi. hata hivyo, baada ya maamuzi ya kuwafukuza akina Zitto, imeelezwa kuwa wafuasi wengi wa chama hicho wameamua kurejea CCM huku wengine wakijiunga chama kipya cha ACT Tanzania. Freeman Mbowe anayo tamaa ya kugombea urais. Hata hivyo tatizo kwake ni Elimu. Mbowe hana elimu ya Shahada inayohitajika kwa mtu kuteuliwa kuwa mgombea Urais.

Blan B ya CHADEMA katika kupata mgombea mwenye sifa ni kuangalia ndani ya mahasimu wao wakubwa kisiasa, Chama cha Mapinduzi ambacho kimesheheni wanasiasa nguli vijana kwa wazee ambao ni Presidential Materials. Target yao kubwa ni wanasiasa wanaotoka mikoa ya Kaskazini na kanda ya Ziwa. Hapa CHADEMA wamekuwa kama fisi ambaye anangojea mkono wa binadau udondoke ili auokote. Lakini wapiiii! CHADEMA nao wanafuata matendo ya fisi. Wanasubiri CCM wateleze hasa katika mchakato wao wa kumpata mgombea urais. Inadaiwa kuwa CHADEMA wanamuangalia sana Edward Lowasa. Kwao wanamuona kuwa Lowasa ni mtu ambaye atakisaidia chama chao kushinda urais wa 2015. Wao wanaamini kuwa LOWASA atatemwa na chama chake kwenye kinyang'anyiro cha urais kitendo ambacho kitasababisha EL ahame chama chake na kujiunga na CDM. Inadaiwa kuwa tayari CHADEMA wamewasilisha mpango wao kwa EL. Hata hivyo, taarifa za ndani zinasema kuwa Lowasa amewaambia live kwamba ikiwa ataamua kugombea urais, basi itakuwa ni kwa tiketi ya CCM kauli ambayo imewakatisha tamaa sana. Baada ya kugonga mwamba kwa Lowasa, inaelezwa kuwa Sumaye na Mama Anna Kajumulo Tibaijuka ni miongoni mwa wanaopendekezwa na Mzee wa Tengeru katika nafasi ya Urais.

Plan C ya CHADEMA ni kuanzisha muungano fake na vyama vingine vya siasa. Kwa kuanzia wameunda umoja ujulikanao kama UKAWA. Ingawa umoja huo lengo kuu ni kupigania Rasimu ya Katiba ya Jaji Warioba, inaelezwa kuwa lengo kuu ni kuwahadaa wanasiasa mahiri wa vyama vingine kama akina Prof Ibrahim Lipumba na James Mbatia. Hapa CHADEMA wanajifanya sitaki nataka. Kwamba, CHADEMA wametoa matamko kuwa UKAWA itasimamisha mgombea mmoja tu katika ngazi ya Rais. Mapendekezo ya awali ni kumsimamisha Mchungaji Christopher Mtikila. Hata hivyo, inadaiwa kuwa James Mbatia, Ibrahim Lipumba na wahafidhina wa CHADEMA wamekataa mapendekezo hayo. Lipumba anadai kuwa ndani ya UKAWA, yeye ndiye Msomi na mkongwe kwenye siasa kuliko wote. Hivyo amewapa masharti kwamba ikiwa UKAWA wataamua kusimamisha Mgombea Urais mmoja, basi wamteue yeye kuwa mgombea. Hata hivyo mzee wa Tengeru amekataa pendekezo hilo la Lipumba kwa sababu zinazojulikana.

Kwa hali hiyo, mipango yote ya CHADEMA Yaani Plan A, B na C imekwama. Wamebaki kutapatapa tu na washauri wao akina Saed Kubenea wanaonekana kukosa kabisa mbinu za kukinusuru chama.

Nawasilisha.

Lizaboni na WanaJF,

Kwanza,Naomba Mleta Mada atuwekee Document ya Maandishi,audio au Video ya Lipumba akijadili na kutoa masharti hayo.Tusipende kulifanya jukwaa hili lionekane la Ovyo .Tumeshiriki sana kulijenga Jukwaa hili

Pili,CHADEMA kilishaweka wazi Msimamo wake.Hakitachukua mgombea kutoka CCM .Tunajitosheleza,tuna hazina kubwa ya Viongozi na tunaandaa viongozi.Bunge lililoisha Dr.Slaa alikua mbunge bora kabisa kwa mujibu wa ripoti za utafiti na vyombo vya habari viliandika

Ameendelea kuwa Mwanasiasa bora kabisa wa kiwango cha juu katika historia ya siasa za upinzani nchini

Ni kutokana na uzoefu na umaahiri huo wa kiutendaji,katika Bunge hili amekiwezesha chama kupata wabunge Bora kabisa kwa mujibu wa Ripoti ya Juzi.Wabunge wa CHADEMA ndio walioshika nafasi za juu kwa Ubora katika Bunge hili

Tatu,Siasa za kijinga na ushabiki uliopindukia na propaganda za kizamani kabisa zisitutoe katika Mstari

Hapa tunaambiwa Zitto na Kitila walikua nguzo na muhimili wa CHADEMA.

Sasa mleta Mada na kundi lake la propaganda kutoka Lumumba na vibaraka wao watuambie.Ni lini Zitto na Kitila walishiriki kujenga na kutekeleza programu ya CHADEMA NI MSINGI?

Hivi lini Zitto, Mwigamba, Kitila wamejenga Chadema!

Katika Uchaguzi wa Chadema unaoendelea nchi nzima toka ngazi ya Misingi kwa mara ya kwanza Chadema sasa ina misingi takriban 15,000 kati ya 18000 iliyopangwa. Ina Misingi takriban 193,000 kati ya 250,000.

Hivi Mchango wa Zitto,Kitila na Mwigamba hapa ni Upi?Tunaomba mje na data badala ya upuuzi huu

Naomba Watanzania,Vijana,wapenzi na wapenda Mabadiliko mpuuze propaganda yao hii ya kipuuzi kwa kiwango kinachostahili

Nne,Saed Kubenea hajawahi kuwa mshauri wa CHADEMA na hakuna cheo hicho kikatiba.

Aidha CHADEMA kama chama cha siasa,kinachojiandaa kuunda serikali kinaamini na kutambua fursa na nafasi yake kama taasisi yenye wajibu na jukumu la kimsingi kabisa hasa la kupokea ushauri na maoni kutoka kila kona ya nchi,kwa watanzania wote ndani na nchi wenye mapenzi mema na Chama na Taifa letu kwa ujumla.Uhuru wa maoni umehifadhiwa kikatiba na kuheshimiwa.wanachama wanawakilishwa pia na vyombo vya maamuzi walivyovichagua kidemokrasia kama vile Sekretarieti,Kamati Kuu,Baraza kuu kwa ngazi ya chama kitaifa ambapo mojawapo ya majukumu ya vyombo hivi ni kukishauri chama chetu

Mathalani,Ni lazima tukumbuke kuwa UKAWA ni Umoja wa Katiba ya Wananchi na lengo ni kulinda na kusimamia maoni ya wananchi katika mchakato huu wa katiba na si Vinginevyo.Umoja huu umehusisha vyama vya siasa vyenye nia ya kusimamia maoni ya wananchi na pia taasisi na makundi mbalimbali yaliyokua na uwakilishi na yasiyokua na uwakilishi kwenye Bunge la Katiba.Tutasimama na wananchi kwa maslahi yao na taifa kwa ujumla hadi tone la Mwisho.

Asanteni sana.Tulinde heshima ya JF kwa Data za uhakika ili tuendane na kauli mbiu ya "Jf-Home of Great Thinkers".Tupuuze propaganda zozote za kijinga.

CC: Paw, invisble, PainKiller
 
Last edited by a moderator:

Similar Discussions

Back
Top Bottom