DEMOKRASIA ILOBAGAZWA

DEMOKRASIA ILOBAGAZWA

Mkandara

Platinum Member
Joined
Mar 3, 2006
Posts
16,059
Reaction score
9,556
Kwanza ni muhimu tuelewe maana ya Demokrasia kabla ya kuutaka kujenga mfumo wa utawala ambao unakidhi matumaini yetu badala ya matakwa ya Demokrasia yenyewe.

Kwanza Demokrasia ni nini? Imeelezwa kwa kifupi kama Demokrasia ni mfumo wa Serikali ambapo mamlaka ni ya wananchi, ambao huyatumia moja kwa moja au kupitia wawakilishi waliochaguliwa.

Isitoshe Demokrasia ina misingi yake mikuu minne ambayo ni pamoja na
1. Uchaguzi Huru,
2. Utawala wa Sheria,
3. Usawa na
4. Haki za Binadamu.
Hii ndiyo misingi mikuu katika ujenzi wa Demokrasia halisi na sii vinginevyo.

Hivyo basi pasipo Uchaguzi huru ambao Wananchi wamekabidhiwa mamlaka ya kuchagua viongozi na Wawakilishi wao, dhahiri bila shaka hatuwezi kutegemea Demokrasia itakuwepo katika Serikali iloundwa kwa mfumo wa tamaduni na taratibu za vyama vya Siasa.

Kwa ujumla Tanzania haijawahi kuwa na Demokrasia kabla na baada ya kuwa na vyama vingi kwa sababu kamati za Uongozi wa Chama ndizo huteua wagombea wa nafasi zote za Uwakilishi. Wananchi hupewa nafasi ya kuchagua kile walichopewa hata kama sii mapendekezo yao.

Toka wakati wa Maalimu nadhani wengi watakumbuka kuwa rais mstaafu Jakaya Kikwete ndiye alokuwa chaguo la Wanachama wa CCM kugombea Urais mwaka 1995, lakini CCM iliunda Utamaduni na taratibu zake ili kupata mgombea Urais, Kamati zake ndizo zenye mamlaka ya mwisho kupitisha majina matatu yatakayo pigiwa kura za wazi na wajumbe wa Mkutano kuu.

Kwa utaratibu kama huo, tulishuhudia yalotokea katika vipindi tofauti vya Uchaguzi ndani ya CCM wakati wa Jakaya, Lowassa na hata rais Samia. Upande wa Chadema wakato wa dr.Slaa, Lowassa na Tundu Lissu. NCCR wakati wa.Mrema na Mbatia, CUF ya Maalim Seif na Lipumba (Wateule) majuzi ACT na Mpina!

Matokeo yake vyama vimezaa Makundi ambayo kwa umoja wao hugombea nafasi hizi za Ungozi kwa kupeana badala ya mamlaka hayo kuwa ni ya Wanachama.

Vivyo hivyo kwenye Vyama vingine vyote vya Siasa ngazi ya Udiwani na Ubunge. Uchaguzi wa Madiwani na Wabunge hautokani na Chaguo la Wananchi, bali ni mapendekezo ya viongozi na Kamati za vyama. Sii lazima mgombea anayekubalika au alopata kura nyingi za Wananchi ndiye atasimama kugombea katika Uchaguzi Mkuu.

Kwa hiyo, vyama vyote vya Siasa toka mashinani kwa muda wote wa Uchaguzi wa ndani ama Uchaguzi Mkuu, wamekuwa wakikiuka msingi huu mkuu wa Demokrasia kwa sababu kigezo kikuu ni mapendekezo ya uongozi wa Chama wenye sura ya Kiumla (Chama kina wenyewe)

Hivyo, yanishangaza kuona Wanasiasa, Wanaharakati, Wasomi, wazee na wataalamu wakikaa kujadili tunatokaje hapa kwa kuzingatia wapi tulipoangukia, badala ya wapi tulipojikwaa.

Ni dhahiri, kila tunapo karibia Uchaguzi Mkuu, chaguzi zote ndani ya Vyama vyote vya Siasa toka Udiwani, Ubunge na hata Urais utasikia jina la fulani limekatwa, fulani alishinda kwa kura nyingi za Wanachama lakini amekatwa, amechukuliwa mshindi wa pili au tatu. Utasikia fulani amekatwa kwa sababu hana sifa za Uongozi. Hizo sifa nyingine zinatoka wapi ikiwa katiba imeainisha sifa za mgombea ibarabya 67(1).

Kifupi nimalizie kwa kusema lawama zote tunazoituhumu Tume ya Uchaguzi, ni mambo hayo hayo yanafanyika waziwazi ndani ya Vyama vya Siasa ili kupata wagombea Uchaguzi Mkuu.

Hakuna Chama kinachosimamisha wagombea wake wote kutokana na matokeo ya Uchaguzi wa Wanachama wake. Sasa tunawezaje kudai Demokrasia juu wakati katika huko chini kwenye shina hakuna Demokrasia?

Kama kweli tunataka Utawala wa Demokrasia, basi ni muhimu sasa tuwe na mfumo bora zaidi wa Tume ya Uchaguzi kuhakikisha kila Chama cha Siasa kitasimamisha Mgombea ambaye alipata kura nyingi za Wanachama katika nafasi zote kuanzia Serikali za mitaa, Udiwani, Ubunge hadi Urais.

Hatuwezi kupigania Demokrasia wakati wa Uchaguzi Mkuu pekee wakati rushwa, takrima, kujuana, fitna, majungu vinatumika huko chini kuwapata wagombea na washindi.

Maasalaam.
 
Mkuu Mkandara, Asante kwa hoja hii, mimi sio nimekuwa nikiisema, imegeuka wimbo nina mabandiko humu zaidi ya 100 ya hoja hii ya demokrasia tenge nchini Tanzania.
Naunga mkono hoja
Demokrasia ni
Serikali ya watu,
Iliyochaguliwa na watu,
Inayoongozwa na watu,
Kwa manufaa ya watu.
Of the people
By the people
For the people!.

Kwa Tanzania ni serikali ya chama
Iliyochaguliwa na chama
Inayoongoza na chama
Kwa manufaa ya chama https://www.jamiiforums.com/threads...a-chama-katiba-si-lolote-si-chochote.2468677/

Mzee Pasco
 
Kwanza ni muhimu tuelewe maana ya Demokrasia kabla ya kuutaka kujenga mfumo wa utawala ambao unakidhi matumaini yetu badala ya matakwa ya Demokrasia yenyewe.

Kwanza Demokrasia ni nini? Imeelezwa kwa kifupi kama Demokrasia ni mfumo wa Serikali ambapo mamlaka ni ya wananchi, ambao huyatumia moja kwa moja au kupitia wawakilishi waliochaguliwa.

Isitoshe Demokrasia ina misingi yake mikuu minne ambayo ni pamoja na
1. Uchaguzi Huru,
2. Utawala wa Sheria,
3. Usawa na
4. Haki za Binadamu.
Hii ndiyo misingi mikuu katika ujenzi wa Demokrasia halisi na sii vinginevyo.

Hivyo basi pasipo Uchaguzi huru ambao Wananchi wamekabidhiwa mamlaka ya kuchagua viongozi na Wawakilishi wao, dhahiri bila shaka hatuwezi kutegemea Demokrasia itakuwepo katika Serikali iloundwa kwa mfumo wa tamaduni na taratibu za vyama vya Siasa.

Kwa ujumla Tanzania haijawahi kuwa na Demokrasia kabla na baada ya kuwa na vyama vingi kwa sababu kamati za Uongozi wa Chama ndizo huteua wagombea wa nafasi zote za Uwakilishi. Wananchi hupewa nafasi ya kuchagua kile walichopewa hata kama sii mapendekezo yao.

Toka wakati wa Maalimu nadhani wengi watakumbuka kuwa rais mstaafu Jakaya Kikwete ndiye alokuwa chaguo la Wanachama wa CCM kugombea Urais mwaka 1995, lakini CCM iliunda Utamaduni na taratibu zake ili kupata mgombea Urais, Kamati zake ndizo zenye mamlaka ya mwisho kupitisha majina matatu yatakayo pigiwa kura za wazi na wajumbe wa Mkutano kuu.

Kwa utaratibu kama huo, tulishuhudia yalotokea katika vipindi tofauti vya Uchaguzi ndani ya CCM wakati wa Jakaya, Lowassa na hata rais Samia. Upande wa Chadema wakato wa dr.Slaa, Lowassa na Tundu Lissu. NCCR wakati wa.Mrema na Mbatia, CUF ya Maalim Seif na Lipumba (Wateule) majuzi ACT na Mpina!

Matokeo yake vyama vimezaa Makundi ambayo kwa umoja wao hugombea nafasi hizi za Ungozi kwa kupeana badala ya mamlaka hayo kuwa ni ya Wanachama.

Vivyo hivyo kwenye Vyama vingine vyote vya Siasa ngazi ya Udiwani na Ubunge. Uchaguzi wa Madiwani na Wabunge hautokani na Chaguo la Wananchi, bali ni mapendekezo ya viongozi na Kamati za vyama. Sii lazima mgombea anayekubalika au alopata kura nyingi za Wananchi ndiye atasimama kugombea katika Uchaguzi Mkuu.

Kwa hiyo, vyama vyote vya Siasa toka mashinani kwa muda wote wa Uchaguzi wa ndani ama Uchaguzi Mkuu, wamekuwa wakikiuka msingi huu mkuu wa Demokrasia kwa sababu kigezo kikuu ni mapendekezo ya uongozi wa Chama wenye sura ya Kiumla (Chama kina wenyewe)

Hivyo, yanishangaza kuona Wanasiasa, Wanaharakati, Wasomi, wazee na wataalamu wakikaa kujadili tunatokaje hapa kwa kuzingatia wapi tulipoangukia, badala ya wapi tulipojikwaa.

Ni dhahiri, kila tunapo karibia Uchaguzi Mkuu, chaguzi zote ndani ya Vyama vyote vya Siasa toka Udiwani, Ubunge na hata Urais utasikia jina la fulani limekatwa, fulani alishinda kwa kura nyingi za Wanachama lakini amekatwa, amechukuliwa mshindi wa pili au tatu. Utasikia fulani amekatwa kwa sababu hana sifa za Uongozi. Hizo sifa nyingine zinatoka wapi ikiwa katiba imeainisha sifa za mgombea ibarabya 67(1).

Kifupi nimalizie kwa kusema lawama zote tunazoituhumu Tume ya Uchaguzi, ni mambo hayo hayo yanafanyika waziwazi ndani ya Vyama vya Siasa ili kupata wagombea Uchaguzi Mkuu.

Hakuna Chama kinachosimamisha wagombea wake wote kutokana na matokeo ya Uchaguzi wa Wanachama wake. Sasa tunawezaje kudai Demokrasia juu wakati katika huko chini kwenye shina hakuna Demokrasia?

Kama kweli tunataka Utawala wa Demokrasia, basi ni muhimu sasa tuwe na mfumo bora zaidi wa Tume ya Uchaguzi kuhakikisha kila Chama cha Siasa kitasimamisha Mgombea ambaye alipata kura nyingi za Wanachama katika nafasi zote kuanzia Serikali za mitaa, Udiwani, Ubunge hadi Urais.

Hatuwezi kupigania Demokrasia wakati wa Uchaguzi Mkuu pekee wakati rushwa, takrima, kujuana, fitna, majungu vinatumika huko chini kuwapata wagombea na washindi.

Maasalaam.
nonsense 🐒
 
Mkuu Mkandara , umeliweka jambo hili kwa usahihi wa hali ya juu, na Mzee Pascal Mayalla ameliongezea uzito kwa ulinganisho wake wa kudumu. Naomba niongeze safu moja ya uchambuzi ambayo naamini itaipa hoja yenu msingi wa kikatiba usiopingika.

Umegundua kitu cha msingi: Katiba ya sasa inasimamia uhuru wa uchaguzi mkuu, lakini haigusi kabisa uhalali wa mchakato uliozaa mgombea kabla ya kufika kwenye uchaguzi huo. Ibara ya 67(1) ya katiba ya jamhuri ya muungano wa tanzania ya mwaka 1977 uliyoitaja inaeleza sifa za mgombea, lakini haitoi njia yoyote ya kikatiba kwa mwanachama aliyeshinda kura za ndani kudai haki yake pale Kamati Kuu ikimkata. Pengo hili si dosari ndogo, ni tundu kubwa linaloruhusu kile ulichokiita "demokrasia iliyobagazwa" kubaki likizoeleka kizazi hadi kizazi.

Kwa Maoni Yangu:
Rasimu ya Katiba iliyopo www.katibampya.com imelifunga tundu hili kwa njia ambayo naamini itawavutia nyote wawili. Ibara ya 176(2)(b)(II) inaweka wazi: endapo Kamati Kuu ya chama itamwangusha mgombea wake wa Urais, Ubunge au Udiwani aliye na vielelezo vya wazi vya kupokonywa ushindi wake, mgombea huyo anapata haki ya kuchukua Hati ya Mashtaka kutoka kwa Mwendesha Mashtaka Mkuu na kufungua shauri lake mwenyewe mbele ya Mahakama ya Katiba, akisimama kwa nafsi yake binafsi, bila kuhitaji ridhaa ya chama chake. Akishinda shauri hilo, anaendelea kuwa mgombea halali wa chama husika, na chama hicho hakiwezi kumfukuza kwa kigezo cha shauri hilo.

Hii inageuza kabisa mizani mliyoieleza. Kwa mfumo wa sasa, kama mlivyoonyesha kwa mifano ya Kikwete, na kwa historia ya vyama vingine vyote, mamlaka ya mwisho ya kumtambua mgombea ni ya Kamati Kuu peke yake, na mwanachama aliyeshinda kura hana pa kukimbilia. Kwa muundo huu, uamuzi wa Kamati Kuu hauwi tena wa mwisho, unabaki chini ya uangalizi wa Mahakama ya Katiba, chombo kilicho nje kabisa ya mfumo wa ndani wa chama.
Zaidi ya hilo, rasimu inaenda mbele zaidi ya uponyaji wa mtu binafsi. Ibara ya 104(7) inaanzisha Kamati ya Malezi ya Vyama vya Siasa ndani ya Ofisi ya Haki, Miiko na Udhibiti wa Demokrasia iliyoko chini ya Baraza la Usimamizi wa Taifa, chombo chenye jukumu la kudumu la kuimarisha maadili ya kidemokrasia ndani ya vyama vyote vilivyosajiliwa, bila upendeleo. Kwa maneno mengine, tatizo la demokrasia ya ndani ya vyama halisubiriwi hadi mgombea mmoja aumie na kufungua kesi, linafuatiliwa kwa jicho la kudumu la kikatiba.

Hii ndiyo tofauti ya msingi kati ya Katiba inayosimamia matokeo ya juu ya mfumo, na Katiba inayogusa mzizi wa mfumo wenyewe. Mlichokigundua wote wawili, kwamba lawama tunazomtupia Tume ya Uchaguzi zinafanyika waziwazi ndani ya vyama, ni ushahidi kwamba tatizo la demokrasia si la juu ya mti, ni la mzizi. Muundo wa Mihimili Minne unaopendekezwa, ambapo Bunge, Serikali na Mahakama zinasimamiwa na Baraza la Usimamizi wa Taifa lisilokuwa la kisiasa, ndio jibu linalofika hadi kwenye mzizi huo, kwa kuweka jicho la kudumu na chombo cha kudai haki mahali ambapo Katiba ya sasa haipo kabisa.

Nawaalika ninyi wote wawili, wenye uzoefu mkubwa wa kufuatilia siasa za ndani ya vyama kwa miongo mingi, kusoma Ibara ya 176 na 104 kwa undani na kutupatia tathmini yenu. Rasimu kamili ipo www.katibampya.com.
 
Shukran sana, nitapitia hizo Ibara tajwa za Katiba Pendekezwa kuhusiana na hili, kisha nitachangia mawazo yangu juu yake.
 
Nimezisoma Ibara hizo mbili kwa haraka, binafsi naona kama Katiba Pendekezwa ina mambo mengi sana yakijirudia rudia kama sii MWONGOZO ulonyooka na rahisi mtu kuuelewa.

Ni hivi, mimi ningeshauri kuipa meno Tume ya Uchaguzi iwe Taasisi HURU yenye mamlaka ya juu kabisa na isofungamana na chama wala Utawala ili wahusike wao na chaguzi zote ndani ya Vyama vya Siasa.

Maadam Vyama.vyote vya Siasa vinataka Tume Huru, budi pia tume hiyo iwe na mamlaka ya Uangalizi wa Chaguzi zote za wagombea Udiwani, Ubunge na Uras toka chini huku chini ngazi ya Vyama, na baadae kusimamia Uchaguzi Mkuu badala ya kuunda muhimili mwingine wa Usimamizi.

Hii itawarahisisha kuwa na records zote za chaguzi nchini na hata mgombea akienda mahakamani wao watasimama kama mashahidi wa kile walichoshuhudia katika Uchaguzi hizo. Naamini mikono mingi katika Upishi huharibu mapishi.

Kitu pekee ambacho natamani kukiona ni kuwa na Vyama Vitatu au Vinne tu vya Siasa nchini badala ya Utitiri tulonao. Kwa kumuenzi Mwalimu, kwanza tuwe na Chama cha Ujamaa kutokana na historia yetu, ambacho kitalinda misingi tuloanza nayo hawa watakuwa Wahafidhina (as Conservative).

Halafu Vyama.vingine vitajipanga Kiitikadi dhidi ya Mrengo wa Ujamaa aidha kuwa Liberali ama Chama kinachokiwa kati Kushoto/Kulia n.k. Hapo tutakuwa wanaoamini katika Ubepari wa Kiafrika. Ndio upi? Watajipanga kwa Itikadi na sera zao.

Kwa wale sasa wanaotaka kujiunga na Siasa wajue wanasimamia nini (Mrengo) badala ta kufuata MTU. Ukiwa Mjamaa ndio imani yako.hata kama hukubaliani na Uongozi uliopo hakuna wakufukuzwa Uanachama ila.anaweza poteza nafasi ya mamlaka ndani ya Chama. Utamfukuzaje muumini ili aende wapi? Kuamini Siasa gani nyingine kama njia bora ya kuwapelekea Wananchi Maendeleo? Kama Mtu anaamini latika.Umamaa utamvuaje Imani hiyo kwa sababu amewakosoa viongozi? Hili ni kosa kubwa la Siasa zetu na tumelifumbia macho kwa muda mrefu sana. Turudi kwenye Uhalisia.

Tukiwa na Vyama vitatu au Vinne, Wagombea Urais waloshindwa Uchaguzi Mkuu wao wanaingia moja kwa moja Bungeni kama wawakilishi wananchi upande wa mrengo wao. Hii itaongeza chachu na umakini zaidi kwa Chama tawala kwa sababu Siasa zitahamia Bungeni badala ya majukwaa ya mikutano na Maandamano. Ndivyo wanavyofanya nchi za Magjaribi.

Swala la Maandamano yataruhusiwa tu kwa Wananchi wenyewe pamoja na Taasisi za Kijamii. Chimbuko la Mikutano ya hadhara na Maandamano kiasili ilikuwa na kusherehekea kama vile Yanga au Simba wanavyo andamana kwanUshindi na hupewa Ulinzi. Sii maandamano ambayo mali za watu ndio zinalindwa! Hizi ni vurugu (strike) na hatari kwa Usalama.wa.Wananchi.

Kisiasa maandamano ni migomo (strikes) ya Wananchi wenyewe kudai haki zao sii Vyama.vya Siasa. Iwe madai ya ongezeko la Mishahara, mazingira ya kazi, mashinikizo ya kudai haki ambazo hutokana na mikataba n.k. Hii habari ya Mikutano na maandamano ya Vyama vya Siasa tena baada ya Uchaguzi Mkuu ndio sababu kubwa ya vurugu zote zinazotokea nchini. Siamini katika.majukwa ya Mikutano ya Kisiasa.kama ni kutafuta Wanachama bali kujenga chuki za Kisiasa.

Niishie hapa kwa leo japo nina mengi sana kichwani ambayo nayaona hayaendi sawa kabisa. Tunatala kuiadhibu Katiba nzima ya mwaka 1977 kwa makosa yetu wenyewe.

Hata hizo Biblia na Kuruan kuna watu wanazikiuka, hivyo hatuwezi sema tuandike Biblia au Kuruan Mpya kwa sababu zimepitwa na wakati. Laa hasha sisi ndio wakosa tinahitaji kumrudia Mungu. Vivyo hivyo kwenye Katiba tunahitaji kujipima Uzalendo wetu sisi wenyewe. Katiba hii tunaibomonda na Tumeibagaza kama sii mwongozo bali kitabu cha Hadith.
 
Kwanza ni muhimu tuelewe maana ya Demokrasia kabla ya kuutaka kujenga mfumo wa utawala ambao unakidhi matumaini yetu badala ya matakwa ya Demokrasia yenyewe.

Kwanza Demokrasia ni nini? Imeelezwa kwa kifupi kama Demokrasia ni mfumo wa Serikali ambapo mamlaka ni ya wananchi, ambao huyatumia moja kwa moja au kupitia wawakilishi waliochaguliwa.

Isitoshe Demokrasia ina misingi yake mikuu minne ambayo ni pamoja na
1. Uchaguzi Huru,
2. Utawala wa Sheria,
3. Usawa na
4. Haki za Binadamu.
Hii ndiyo misingi mikuu katika ujenzi wa Demokrasia halisi na sii vinginevyo.

Hivyo basi pasipo Uchaguzi huru ambao Wananchi wamekabidhiwa mamlaka ya kuchagua viongozi na Wawakilishi wao, dhahiri bila shaka hatuwezi kutegemea Demokrasia itakuwepo katika Serikali iloundwa kwa mfumo wa tamaduni na taratibu za vyama vya Siasa.

Kwa ujumla Tanzania haijawahi kuwa na Demokrasia kabla na baada ya kuwa na vyama vingi kwa sababu kamati za Uongozi wa Chama ndizo huteua wagombea wa nafasi zote za Uwakilishi. Wananchi hupewa nafasi ya kuchagua kile walichopewa hata kama sii mapendekezo yao.

Toka wakati wa Maalimu nadhani wengi watakumbuka kuwa rais mstaafu Jakaya Kikwete ndiye alokuwa chaguo la Wanachama wa CCM kugombea Urais mwaka 1995, lakini CCM iliunda Utamaduni na taratibu zake ili kupata mgombea Urais, Kamati zake ndizo zenye mamlaka ya mwisho kupitisha majina matatu yatakayo pigiwa kura za wazi na wajumbe wa Mkutano kuu.

Kwa utaratibu kama huo, tulishuhudia yalotokea katika vipindi tofauti vya Uchaguzi ndani ya CCM wakati wa Jakaya, Lowassa na hata rais Samia. Upande wa Chadema wakato wa dr.Slaa, Lowassa na Tundu Lissu. NCCR wakati wa.Mrema na Mbatia, CUF ya Maalim Seif na Lipumba (Wateule) majuzi ACT na Mpina!

Matokeo yake vyama vimezaa Makundi ambayo kwa umoja wao hugombea nafasi hizi za Ungozi kwa kupeana badala ya mamlaka hayo kuwa ni ya Wanachama.

Vivyo hivyo kwenye Vyama vingine vyote vya Siasa ngazi ya Udiwani na Ubunge. Uchaguzi wa Madiwani na Wabunge hautokani na Chaguo la Wananchi, bali ni mapendekezo ya viongozi na Kamati za vyama. Sii lazima mgombea anayekubalika au alopata kura nyingi za Wananchi ndiye atasimama kugombea katika Uchaguzi Mkuu.

Kwa hiyo, vyama vyote vya Siasa toka mashinani kwa muda wote wa Uchaguzi wa ndani ama Uchaguzi Mkuu, wamekuwa wakikiuka msingi huu mkuu wa Demokrasia kwa sababu kigezo kikuu ni mapendekezo ya uongozi wa Chama wenye sura ya Kiumla (Chama kina wenyewe)

Hivyo, yanishangaza kuona Wanasiasa, Wanaharakati, Wasomi, wazee na wataalamu wakikaa kujadili tunatokaje hapa kwa kuzingatia wapi tulipoangukia, badala ya wapi tulipojikwaa.

Ni dhahiri, kila tunapo karibia Uchaguzi Mkuu, chaguzi zote ndani ya Vyama vyote vya Siasa toka Udiwani, Ubunge na hata Urais utasikia jina la fulani limekatwa, fulani alishinda kwa kura nyingi za Wanachama lakini amekatwa, amechukuliwa mshindi wa pili au tatu. Utasikia fulani amekatwa kwa sababu hana sifa za Uongozi. Hizo sifa nyingine zinatoka wapi ikiwa katiba imeainisha sifa za mgombea ibarabya 67(1).

Kifupi nimalizie kwa kusema lawama zote tunazoituhumu Tume ya Uchaguzi, ni mambo hayo hayo yanafanyika waziwazi ndani ya Vyama vya Siasa ili kupata wagombea Uchaguzi Mkuu.

Hakuna Chama kinachosimamisha wagombea wake wote kutokana na matokeo ya Uchaguzi wa Wanachama wake. Sasa tunawezaje kudai Demokrasia juu wakati katika huko chini kwenye shina hakuna Demokrasia?

Kama kweli tunataka Utawala wa Demokrasia, basi ni muhimu sasa tuwe na mfumo bora zaidi wa Tume ya Uchaguzi kuhakikisha kila Chama cha Siasa kitasimamisha Mgombea ambaye alipata kura nyingi za Wanachama katika nafasi zote kuanzia Serikali za mitaa, Udiwani, Ubunge hadi Urais.

Hatuwezi kupigania Demokrasia wakati wa Uchaguzi Mkuu pekee wakati rushwa, takrima, kujuana, fitna, majungu vinatumika huko chini kuwapata wagombea na washindi.

Maasalaam.
Hio wala si demokrasia bali domogasia kama siyo demockrery kwa kisukuma
 
Mkuu kabla sijachangia mada naomba kuweka historia vizuri
CHADEMA walianza na utaratibu wa kuchagua kuanzia ngazi za chini kisha Kanda. Utaratibu huo ukaigwa na CCM kwa kuita kura za maoni. Kura za maoni ni njia tu ya kutoa mwanya kwa ngazi za juu kufyeka au kuweka watu wao.

Nikirejea bandiko lako umetaja mambo kadhaa kama msingi wa Demokrasia. Kuna moja muhimu umeliacha ambalo ni uhuru wa kuamua, kushiriki au kutenda kwa mujibu wa sheria bila kizuizi.

Hakuna sababu zozote za kuwa na Tume ya Uchaguzi kusimamia chaguzi za vyama, in fact hata msajili wa vyama anapaswa kusajili tu wala si kulea. Kwa maana kwamba vyama viwe huru kutengeneza taratibu zao zitazowawezesha kushiriki chaguzi bila kufungwa na sheria yoyote.

Jibu rahisi la nini kifanyike ni kuruhusu MGOMBEA BINAFSI. Hakuna jibu lingine wala sioni utaratibu mwingine
 
Mkuu, Ukisha sema kwa mujibu wa Sheria, hiyo inaondoka katika misingi kwa sababu misingi ndio Sheria yenyewe. Hivyo Uhuru wa kushiriki unaingia katika hayo manne inategrmea Ushiriki upi unazungumziwa.

Swala la nani alianza kusema kweli mimi sijui ila natazama ni wapi tulipojikwaa tukaanguka kiasi hiki tunapozungumzia Demokrasia. Nikagundua kwamba Demokrasia haikuhi kuwepo Tanzania! Chaguzi zote za Madiwani na Wabunge mara zote walikuwa wateule wa Kiongozi wa juu na sababu rais aliyepo madarakani anawahitaji kushika vyadhifa mbali mbali za Serikali yake. Ndani ya Chama hapakuwa na Uchaguzi bali waliteuliwa kugombea nafasi hizo Uchaguzi Mkuu.

Na hata Ukitazama vyama vya Upinzani nako unakuta Viongozi wajumbe wa Kamati Kuu na kamati nyinginezo hawa ndio Wagombea Ubunge wa Uchaguzi Mkuu. Nani alowachagua wakagombee ubunge katika ambayo sii wakazi wa huko? Kwa hiyo ni kundi la watu walochaguana na kugawana majimbo ya kugombea. That is a fact kwa vyama vyote vya siasa Tanzania.

Kibaya zaidi basi unakuta wagombea wenyewe sii wakazi wa Jimbo hilo kwa hiyo hutokea tu wakati wa kuomba Kura baada ya hapo wanasepa tutaonana mwakani. Hata Bungeni unakuta wanajikita zaidi katika maswala ya Kitaifa badala ya Uwakilishi wa Wananchu katika Majimbo walogombea.

Huo ndio Ukweli wa Demokrasia tunayodai leo, haipo wala haijawahi kuwepo na sii kwa sababu ya Katiba au mfumo wa CCM bali Vyama vyote vimejikita katika Siasa za Kuingia Ikulu by all means necessary badala ya kuwatumikia Wananchi. Pasipo kuhakikisha Wananchi ndio wenye Mamlaka ya Kuchagua Viongozi na wawakilishi wake haijalishi hata tukiwa na Mgombea Huru! Hatuta inuka toka hapa tulipo angukia!

In fact mimi naogopa sana Mgombea Huru kuwa rais wa nchi kwa kuzingatia mila na tamaduni Waafrika.(Maskini). Nafasi zoye za juu ataweka watu wake halafu mtaanza kulia kama navyowasikia Watanganyika leo wakilia na rais Samia. Nikiuliza kisa nini? Naambiwa Positon nyingi za Juu kaweka watu wake au wa huko kwao. Kama ndivyo inakuwaje Leo mnataka Mgombea Huru kweli?
 
Nimezisoma Ibara hizo mbili kwa haraka, binafsi naona kama Katiba Pendekezwa ina mambo mengi sana yakijirudia rudia kama sii MWONGOZO ulonyooka na rahisi mtu kuuelewa.

Ni hivi, mimi ningeshauri kuipa meno Tume ya Uchaguzi iwe Taasisi HURU yenye mamlaka ya juu kabisa na isofungamana na chama wala Utawala ili wahusike wao na chaguzi zote ndani ya Vyama vya Siasa.

Maadam Vyama.vyote vya Siasa vinataka Tume Huru, budi pia tume hiyo iwe na mamlaka ya Uangalizi wa Chaguzi zote za wagombea Udiwani, Ubunge na Uras toka chini huku chini ngazi ya Vyama, na baadae kusimamia Uchaguzi Mkuu badala ya kuunda muhimili mwingine wa Usimamizi.

Hii itawarahisisha kuwa na records zote za chaguzi nchini na hata mgombea akienda mahakamani wao watasimama kama mashahidi wa kile walichoshuhudia katika Uchaguzi hizo. Naamini mikono mingi katika Upishi huharibu mapishi.

Kitu pekee ambacho natamani kukiona ni kuwa na Vyama Vitatu au Vinne tu vya Siasa nchini badala ya Utitiri tulonao. Kwa kumuenzi Mwalimu, kwanza tuwe na Chama cha Ujamaa kutokana na historia yetu, ambacho kitalinda misingi tuloanza nayo hawa watakuwa Wahafidhina (as Conservative).

Halafu Vyama.vingine vitajipanga Kiitikadi dhidi ya Mrengo wa Ujamaa aidha kuwa Liberali ama Chama kinachokiwa kati Kushoto/Kulia n.k. Hapo tutakuwa wanaoamini katika Ubepari wa Kiafrika. Ndio upi? Watajipanga kwa Itikadi na sera zao.

Kwa wale sasa wanaotaka kujiunga na Siasa wajue wanasimamia nini (Mrengo) badala ta kufuata MTU. Ukiwa Mjamaa ndio imani yako.hata kama hukubaliani na Uongozi uliopo hakuna wakufukuzwa Uanachama ila.anaweza poteza nafasi ya mamlaka ndani ya Chama. Utamfukuzaje muumini ili aende wapi? Kuamini Siasa gani nyingine kama njia bora ya kuwapelekea Wananchi Maendeleo? Kama Mtu anaamini latika.Umamaa utamvuaje Imani hiyo kwa sababu amewakosoa viongozi? Hili ni kosa kubwa la Siasa zetu na tumelifumbia macho kwa muda mrefu sana. Turudi kwenye Uhalisia.

Tukiwa na Vyama vitatu au Vinne, Wagombea Urais waloshindwa Uchaguzi Mkuu wao wanaingia moja kwa moja Bungeni kama wawakilishi wananchi upande wa mrengo wao. Hii itaongeza chachu na umakini zaidi kwa Chama tawala kwa sababu Siasa zitahamia Bungeni badala ya majukwaa ya mikutano na Maandamano. Ndivyo wanavyofanya nchi za Magjaribi.

Swala la Maandamano yataruhusiwa tu kwa Wananchi wenyewe pamoja na Taasisi za Kijamii. Chimbuko la Mikutano ya hadhara na Maandamano kiasili ilikuwa na kusherehekea kama vile Yanga au Simba wanavyo andamana kwanUshindi na hupewa Ulinzi. Sii maandamano ambayo mali za watu ndio zinalindwa! Hizi ni vurugu (strike) na hatari kwa Usalama.wa.Wananchi.

Kisiasa maandamano ni migomo (strikes) ya Wananchi wenyewe kudai haki zao sii Vyama.vya Siasa. Iwe madai ya ongezeko la Mishahara, mazingira ya kazi, mashinikizo ya kudai haki ambazo hutokana na mikataba n.k. Hii habari ya Mikutano na maandamano ya Vyama vya Siasa tena baada ya Uchaguzi Mkuu ndio sababu kubwa ya vurugu zote zinazotokea nchini. Siamini katika.majukwa ya Mikutano ya Kisiasa.kama ni kutafuta Wanachama bali kujenga chuki za Kisiasa.

Niishie hapa kwa leo japo nina mengi sana kichwani ambayo nayaona hayaendi sawa kabisa. Tunatala kuiadhibu Katiba nzima ya mwaka 1977 kwa makosa yetu wenyewe.

Hata hizo Biblia na Kuruan kuna watu wanazikiuka, hivyo hatuwezi sema tuandike Biblia au Kuruan Mpya kwa sababu zimepitwa na wakati. Laa hasha sisi ndio wakosa tinahitaji kumrudia Mungu. Vivyo hivyo kwenye Katiba tunahitaji kujipima Uzalendo wetu sisi wenyewe. Katiba hii tunaibomonda na Tumeibagaza kama sii mwongozo bali kitabu cha Hadith.
Mkuu Mkandara, ahsante kwa kuzipitia Ibara hizo na kwa uwazi wa maoni yako. Naomba nikubaliane na wewe kwenye mambo mawili ya msingi kabla sijaeleza kwa nini rasimu imesimama pale ilipo, kisha nijibu pendekezo lako la Tume moja yenye mamlaka yote, kwa mantiki hilo ndilo linalobeba uzito mkubwa zaidi wa kiuundo.

Kwanza, kuhusu urefu na marudio, uko sahihi kabisa. Rasimu hii ina Sura kumi na nne na Ibara mia tatu ishirini na moja, (14/321) na ni ndefu kwa kiwango ambacho hakiwezi kubishaniwa. Marudio unayoyaona si udanganyifu wa uandishi, ni matokeo ya uamuzi wa kimakusudi kwamba kila Ibara imeandikwa iwe na uwezo wa kusomeka na kueleweka bila kumlazimisha msomaji kurudi mara kwa mara kwenye Ibara nyingine ili kuipata maana kamili. Hii ni gharama ya urefu badala ya gharama ya utata. Nakubaliana na wewe kwamba hii inaifanya isiwe rahisi kusomwa mfululizo na mtu wa kawaida, na hilo ni jambo ambalo Muongozo na Uchambuzi tunaouandaa kwa lengo la kuisaidia jamii kuisoma sehemu kwa sehemu unajaribu kulishughulikia, ingawa sikatai kwamba rasimu kamili yenyewe inabaki nzito kwa msomaji wa mara ya kwanza, labda aisome zaidi ya mala moja Ndo utaiona Nyepesi Sana zaidi ya Kuisoma mala moja Tu.

Pili, kuhusu Ujamaa na idadi ya vyama, nako uko sahihi. Rasimu hii haijatamka Ujamaa wala itikadi nyingine yoyote kama msingi wa uchumi au siasa ya Taifa, wala haijaweka ukomo wa idadi ya vyama. Hili si pengo la bahati mbaya, ni uamuzi wa kifalsafa wa makusudi, na naomba nijitetee kwa uwazi kuhusu hilo. Ibara ya 104(6) inatamka waziwazi kwamba hakuna mtu anayeweza kulazimishwa kujiunga na chama fulani au itikadi fulani, wala chama hakiwezi kukataliwa kusajiliwa kwa kigezo cha itikadi yake, Hivyo Basi Kama rasimu ingeweka Ujamaa au itikadi nyingine yoyote kama msingi rasmi wa Taifa, au ingefunga idadi ya vyama view vitatu au vinne, Katiba yenyewe ingekuwa imeshachagua upande mmoja wa mjadala wa kiitikadi kabla mjadala huo haujaanza. Pia Wazo lako la chama cha Ujamaa chenye kumuenzi Mwalimu ni zuri na lina nafasi kamili ndani ya muundo huu, kwa mantiki hakuna kinachokizuia kuanzishwa na kushindana kihalali, Tofauti ni kwamba rasimu haitaki kukilazimisha wala kukikataza, inataka kubaki mahali ambapo kila itikadi, ikiwemo Ujamaa, inaweza kusimama sawa mbele ya wapiga kura.
(Kwa Nyoongeza yangu Rasimu hiyo kwenye Ibara ya 273(5)(a) na (b) Zimetamka Kuhusu Tunu ya Heshima na zimetamka Ofisi mbili za kuwaenzi waasisi wa Taifa, Yaani Karume na JK Nyerere, hii inaweza Kutoa Majibu ya Maswali yako Kuhusu kuwakumbuka waasisi wa Taifa Letu.)

Sasa naomba niende kwenye pendekezo lako zito zaidi, ambalo ni kuipa Tume Huru ya Uchaguzi mamlaka ya juu kabisa juu ya chaguzi zote, kuanzia za ndani ya vyama hadi Uchaguzi Mkuu, badala ya kuunda muhimili mpya wa usimamizi. Hoja yako ina mantiki ya vitendo, kwa mantiki chombo kimoja chenye kumbukumbu zote kingerahisisha ushahidi mahakamani. Lakini hapa ndipo naona hatari ya kimuundo ambayo naomba unipe nafasi ya kuieleza.

Ukiipa Tume moja mamlaka ya kusimamia uendeshaji wa kiufundi wa Uchaguzi Mkuu, wakati huohuo ikawa ndiyo inayosimamia demokrasia ya ndani ya vyama, na ikawa tena ndiyo yenye mamlaka ya juu kabisa isiyofungamana na chombo kingine chochote, umeweka mizigo mitatu tofauti kabisa kimaumbile juu ya bega moja.
1. Usimamizi wa kiufundi wa upigaji kura ni taaluma ya uendeshaji na Utendaji wa Tume huru ya uchaguzi.

2. Uamuzi wa haki kati ya mwanachama na Kamati Kuu ya chama ni taaluma ya kimahakama.

3. Usimamizi wa Misingi ya Demokrasia ni swala la Baraza la Usimamizi wa Taifa. (Naomba nikufafanulie hapa, Baraza la Usimamizi wa Taifa Kazi yake ni Kusimamia Misingi yote ya taifa, Yaani Misingi yote inayolifanya Taifa liwepo, Hivyo Basi miongoni mwa Misingi ya Demokrasia ni Uchaguzi ulio Huru, kweli na Haki na hapa ndipo Baraza linaingia kutoa Tathimini yake, au muongozo lakini alijihusishi wala kuingilia Utendaji wa Kila siku wa Tume. Pia naomba niendelee kufafanua kwamba Baraza linasimamia Misingi ya Demokrasia sio Utendaji wa Tume Huru ya Uchaguzi, lakini pia Haki ya mwanachama wa chama cha Siasa Husika inapatikana Mahakamani hasa Mahakama ya Katiba kama Rasimu yenyewe ilivyowekwa. Kwa kuongezea hapa ni kwamba "Baraza hilo lina kazi zaidi ya moja na kusimamia misingi ya demokrasia ni sehemu ya kazi zake si Kazi pekee iliyowekwa na katiba", )

NAOMBA KUENDELEA KIDOGO HAPA.
Ukiviunganisha vyote vitatu kwenye chombo kimoja, na kikaishiwa kufungamana na mtu yeyote, tatizo halipotei, linahama tu.

Embu jiulize What if.! Tume hiyo moja itatekwa siku moja, na Chama Fulani cha Siasa, kikundi cha Maslahi Binafsi au vyovyote, na hakuna mahali pa kukimbilia, kwa mantiki umeondoa uwiano wa kuangaliana uliokuwepo hapo awali.

Ndiyo maana rasimu imeamua kugawa mizigo hii mitatu kwa vyombo vitatu tofauti vinavyoangaliana.
1. Tume Huru ya Uchaguzi inabaki na jukumu lake la kiufundi la kuendesha Uchaguzi Mkuu.

2. Mahakama ya Katiba, kupitia Ibara ya 176(2)(b)(II), inabaki na jukumu la kuamua haki kati ya mwanachama aliyepokonywa ushindi na Kamati Kuu ya chama chake.

3. Baraza la usimamizi wa taifa kwa kupitia kwa Kamati ya Malezi ya Vyama vya Siasa, iliyoko ndani ya Ofisi ya Haki, Miiko na Udhibiti wa Demokrasia chini ya Baraza, inabaki na jukumu la kufuatilia afya ya kidemokrasia ya vyama kwa muda wote, si wakati wa uchaguzi pekee. Yaani Haki za kidemokrasia, maadili ya taifa, miiko na udhiti hili siasa isitumike kuathili usalama wa taifa au kuchota tamaduni za njee zisizo njema kwa taifa letu.

Kwenye Muundo Huu Kila chombo kina mamlaka finyu (Separation of power), lakini vyote vitatu vinasimama kwenye Mipaka yake na vinakuwa bora, hivyo Basi kutekwa kwa Chombo kimoja hakuvunji mfumo mzima, Bali itasaidia Kutambua Kwa Haraka shida hipo wapi.

Kuhusu mlinganisho wako wa mwisho, kati ya Katiba na vitabu vya dini, naomba nikupe mtazamo mwingine wa kuuangalia.

Vitabu vya dini vinaongoza dhamiri ya mtu binafsi, na uvunjaji wake huwa kati ya mtu na imani yake, Yaani Leo Mimi nikitenda dhambi ya uzinifu ni Mimi na Mungu wangu, na wala Jamii yangu haiwezi kuathilika na dhambi niliyofanya.

Lakini Katiba ina kazi tofauti kabisa, yaani Mwenye Madaraka anapokula Mali ya Umma unaoathilika ni Umma wote sio yeye Binafsi, au Mtu mmoja, hivyo Basi kazi ya Katiba si Tu Kutoa muongozo wa mambo mbali mbali ya Taifa lakini pia kwenye mada hii ni kumfunga mwenye madaraka hata pale asipokuwa na dhamiri njema.

NAOMBA NIKWAMBIA HAYA KWA UZITO MKUBWA KWAMBA.
Mfumo unaotegemea uzalendo wa watu peke yake, bila muundo wa kuwabana wale wenye tabia mbaya, ni bahati nasibu, si mpango wa kudumu.

Mimi Kwa Maoni yangu sikubaliani kwamba tatizo ni sisi wenyewe pekee bila muundo kuhusika, kwa mantiki hata watu wema wanahitaji mfumo unaowazuia Ili wabaki wema wakati wote, na ndipo thamani ya urefu wa Ibara hizi mia tatu ishirini na moja 321 inapoonekana, japo naelewa kabisa unavyoona uzito wake.

OMBI LANGU KWAKO MKUU NI HILI.
Binafsi nimeona wewe si tu msomaji wa kawaida wa Mada hii Bali Unatafuta kitu kilicho bora zaidi, Mimi sitaki kukuaminisha kwamba Rasimu hii ni Bora moja kwa moja Bali ninachoitaji ni kukuongoza sehemu za kusoma Hili kuamua kurudi hapa na kusema kwamba Rasimu hiyo ni Bora Basi usome Kwa Moyo Wako wote, si kukuaminisha kabra ujasoma wewe mwenyewe.

Kwanza kabisa na Kwa ukweli kwamba Rasimu hiyo ni ndefu Sana nakuomba nikupe muongozo wa wapi pa kuanza kusoma Hili Kuisoma mala moja Tu Uweze kuielewa Haraka zaidi.

Anza Ibara ya 286(1) Mwanzo kabisa kuna mambo yaliyowekwa Kuhusu Namna Katiba hiyo ilivyoandikwa, Yaani "Ibara, Ibara ndogo, Aya, kipengere na Aya ndogo. Pia kuna kitu kama vile kikao cha Ufafanuzi maana yake ni nini...? Na kinakaa wapi.? kwenye Rasimu kinaonekana ndani ya maneno yaliyowekewa Kati Kati ya [+......].

Kisha Ibara Hiyo hiyo, Yaani 286(2) kuna muongozo wa Katiba yote, Mipaka ya Jumla na Ufafanuzi wa Jumla wa Katiba.

All in all Ibara ya 286 ni Ibara ya Ufafanuzi wa Katiba yote, Yaani maneno yaliyotumika, na Nyoongeza nyingine kama vile bodi ya Kikatiba n.k

Ukishasoma Ibara Hizo pia soma Ibara ya 98 mbaka 116 Kuhusu Baraza la Usimamizi wa Taifa maana ndicho kitu kigeni zaidi kwenye Katiba hii na Kiukweli Ndio Muhimili wa Nne Wenyewe, hivyo umeelezewa kiundani kabisa kwenye Ibara Hizo Hapo Tajwa.

Baada ya hapo sasa kuanza Mwanzo Ibara ya 1 mbaka ya 321 unapata picha Kamili na kuelewa ubora wa Rasimu Hiyo ya Katiba.

Naomba niendelee kusema kwamba Rasimu hii ni ndefu hasa wingi wa Ibara zake lakini Naona ni muhimu kuwa Hivyo Kwa sababu pia Baraza Ndio Mamlaka ya Kimuungano Kati ya Tanganyika na Zanzibar hivyo Rasimu hiyo imetoa Majibu ya Maswali ya Muundo wa Muungano, Yaani Serikali Moja, mbili au Tatu. Yaani Rasimu hii imeweka Serikali Moja na kuongeza Muhimili wa Nne ambao Ndio unawakutanisha Tanganyika na Zanzibar kusimamia Misingi yote ya Taifa na hapo ndipo Mihimili mingine iliyobaki inakuwa Mihimili ya Jamhuri ya Muungano na Muungano Kati ya Pande Hizo mbili unapewa Mamlaka ya kusimamia Misingi yote.

Hivyo basi Rasimu hiyo ina mihimili minne ya kitaifa, yaani.
1. Baraza l usimamizi wa Taifa.
2. Serikali ya jamhuri ya muungano wa tanzania.
3. Bunge la jamhuri ya muungano wa tanzania.
4. Mahakama ya jamhuri ya muungano wa tanzania.

Mihimili yote minne imetamkwa kwenye SURA YA NNE ya Rasimu hiyo ya katiba kwa kuanzia na Baraza na kuendelea mihimili mingineyo.

Nilisema Misingi yote ya Taifa maana yake ni Misingi yote ya Demokrasia, Misingi ya Muungano wetu, Misingi ya Ukuu wa Katiba, Misingi ya utawala wa Sheria, Misingi ya Maendeleo na Mengineyo mengi, kwaiyo baraza la usimamizi wa misingi ya taifa kazi yake ni kuhakikisha misingi hiyo inaendelea kuwepo na isiweze kudhoofishwa kwa maslahi ya chama cha siasa, kikundi cha maslahi binafsi au mtu mmoja.

Rasimu Kamili ya Katiba Hipo kwenye Tovuti ya www.katibampya.com
 
Kwanza ni muhimu tuelewe maana ya Demokrasia kabla ya kuutaka kujenga mfumo wa utawala ambao unakidhi matumaini yetu badala ya matakwa ya Demokrasia yenyewe.

Kwanza Demokrasia ni nini? Imeelezwa kwa kifupi kama Demokrasia ni mfumo wa Serikali ambapo mamlaka ni ya wananchi, ambao huyatumia moja kwa moja au kupitia wawakilishi waliochaguliwa.

Isitoshe Demokrasia ina misingi yake mikuu minne ambayo ni pamoja na
1. Uchaguzi Huru,
2. Utawala wa Sheria,
3. Usawa na
4. Haki za Binadamu.
Hii ndiyo misingi mikuu katika ujenzi wa Demokrasia halisi na sii vinginevyo.

Hivyo basi pasipo Uchaguzi huru ambao Wananchi wamekabidhiwa mamlaka ya kuchagua viongozi na Wawakilishi wao, dhahiri bila shaka hatuwezi kutegemea Demokrasia itakuwepo katika Serikali iloundwa kwa mfumo wa tamaduni na taratibu za vyama vya Siasa.

Kwa ujumla Tanzania haijawahi kuwa na Demokrasia kabla na baada ya kuwa na vyama vingi kwa sababu kamati za Uongozi wa Chama ndizo huteua wagombea wa nafasi zote za Uwakilishi. Wananchi hupewa nafasi ya kuchagua kile walichopewa hata kama sii mapendekezo yao.

Toka wakati wa Maalimu nadhani wengi watakumbuka kuwa rais mstaafu Jakaya Kikwete ndiye alokuwa chaguo la Wanachama wa CCM kugombea Urais mwaka 1995, lakini CCM iliunda Utamaduni na taratibu zake ili kupata mgombea Urais, Kamati zake ndizo zenye mamlaka ya mwisho kupitisha majina matatu yatakayo pigiwa kura za wazi na wajumbe wa Mkutano kuu.

Kwa utaratibu kama huo, tulishuhudia yalotokea katika vipindi tofauti vya Uchaguzi ndani ya CCM wakati wa Jakaya, Lowassa na hata rais Samia. Upande wa Chadema wakato wa dr.Slaa, Lowassa na Tundu Lissu. NCCR wakati wa.Mrema na Mbatia, CUF ya Maalim Seif na Lipumba (Wateule) majuzi ACT na Mpina!

Matokeo yake vyama vimezaa Makundi ambayo kwa umoja wao hugombea nafasi hizi za Ungozi kwa kupeana badala ya mamlaka hayo kuwa ni ya Wanachama.

Vivyo hivyo kwenye Vyama vingine vyote vya Siasa ngazi ya Udiwani na Ubunge. Uchaguzi wa Madiwani na Wabunge hautokani na Chaguo la Wananchi, bali ni mapendekezo ya viongozi na Kamati za vyama. Sii lazima mgombea anayekubalika au alopata kura nyingi za Wananchi ndiye atasimama kugombea katika Uchaguzi Mkuu.

Kwa hiyo, vyama vyote vya Siasa toka mashinani kwa muda wote wa Uchaguzi wa ndani ama Uchaguzi Mkuu, wamekuwa wakikiuka msingi huu mkuu wa Demokrasia kwa sababu kigezo kikuu ni mapendekezo ya uongozi wa Chama wenye sura ya Kiumla (Chama kina wenyewe)

Hivyo, yanishangaza kuona Wanasiasa, Wanaharakati, Wasomi, wazee na wataalamu wakikaa kujadili tunatokaje hapa kwa kuzingatia wapi tulipoangukia, badala ya wapi tulipojikwaa.

Ni dhahiri, kila tunapo karibia Uchaguzi Mkuu, chaguzi zote ndani ya Vyama vyote vya Siasa toka Udiwani, Ubunge na hata Urais utasikia jina la fulani limekatwa, fulani alishinda kwa kura nyingi za Wanachama lakini amekatwa, amechukuliwa mshindi wa pili au tatu. Utasikia fulani amekatwa kwa sababu hana sifa za Uongozi. Hizo sifa nyingine zinatoka wapi ikiwa katiba imeainisha sifa za mgombea ibarabya 67(1).

Kifupi nimalizie kwa kusema lawama zote tunazoituhumu Tume ya Uchaguzi, ni mambo hayo hayo yanafanyika waziwazi ndani ya Vyama vya Siasa ili kupata wagombea Uchaguzi Mkuu.

Hakuna Chama kinachosimamisha wagombea wake wote kutokana na matokeo ya Uchaguzi wa Wanachama wake. Sasa tunawezaje kudai Demokrasia juu wakati katika huko chini kwenye shina hakuna Demokrasia?

Kama kweli tunataka Utawala wa Demokrasia, basi ni muhimu sasa tuwe na mfumo bora zaidi wa Tume ya Uchaguzi kuhakikisha kila Chama cha Siasa kitasimamisha Mgombea ambaye alipata kura nyingi za Wanachama katika nafasi zote kuanzia Serikali za mitaa, Udiwani, Ubunge hadi Urais.

Hatuwezi kupigania Demokrasia wakati wa Uchaguzi Mkuu pekee wakati rushwa, takrima, kujuana, fitna, majungu vinatumika huko chini kuwapata wagombea na washindi.

Maasalaam.
Essay la maneno 7,0000 yasiyo na maana yoyote zaidi ya kutaguta kuhalaisha UPUMBAVU.

Unajaribu ku-sound upumbavu, utafikiri masuala ya uchaguzi wa viongozi ni masuala miliki ya wanansiasa, na kwasababu wanasiasa kupitia vyama vyao wana shida, basi na wananchi hawatakiwi kuchagua watu wao.

Jinga kabisa.
 
Back
Top Bottom