Wadau, ni dhahiri kuwa CHADEMA sasa hakijiwezi tena na kimechoka hadi huruma.
Kwa ujumla ni kwamba, CHADEMA hawana mtu mwenye sifa, uwezo wala hadhi kuweza kukiwezesha chama kupata angalau asilimia 10 ya kura za Rais. Tegemeo lao hapo awali lilikuwa kwa Dr Slaa. Hata hivyo, imedhihirika kuwa kwa sasa Dr Slaa hana mvuto tena na kama chadema wataamua kiubishi ubishi kumsimamisha kugombea, hakika wataangukia pua kabisa. Hadhi ya Dr Slaa kwa sasa imeshuka sana na wataalam wa masuala ya kisiasa wanasema kuwa asipojiangalia mwisho wake utakuwa mbaya zaidi. Kushuka kwa hadhi kwa Dr Slaa pamoja na mambo mengine kumeelezwa kuwa kumetokana na kitendo chake cha kupanga, kuratibu na kusimamia mpango wa kumng'oa Zitto Kabwe kwenye chama hicho. Wachambuzi wa masuala ya kisiasa wanasema kuwa uwepo wa wanasiasa nguli kama Zitto Kabwe na wasomi mahiri kama Dr Kitila Mkumbo na wapanga mikakati kama Samson Mwigamba kulikiwezesha chama hicho kuaminiwa na wananchi wengi. hata hivyo, baada ya maamuzi ya kuwafukuza akina Zitto, imeelezwa kuwa wafuasi wengi wa chama hicho wameamua kurejea CCM huku wengine wakijiunga chama kipya cha ACT Tanzania. Freeman Mbowe anayo tamaa ya kugombea urais. Hata hivyo tatizo kwake ni Elimu. Mbowe hana elimu ya Shahada inayohitajika kwa mtu kuteuliwa kuwa mgombea Urais.
Blan B ya CHADEMA katika kupata mgombea mwenye sifa ni kuangalia ndani ya mahasimu wao wakubwa kisiasa, Chama cha Mapinduzi ambacho kimesheheni wanasiasa nguli vijana kwa wazee ambao ni Presidential Materials. Target yao kubwa ni wanasiasa wanaotoka mikoa ya Kaskazini na kanda ya Ziwa. Hapa CHADEMA wamekuwa kama fisi ambaye anangojea mkono wa binadau udondoke ili auokote. Lakini wapiiii! CHADEMA nao wanafuata matendo ya fisi. Wanasubiri CCM wateleze hasa katika mchakato wao wa kumpata mgombea urais. Inadaiwa kuwa CHADEMA wanamuangalia sana Edward Lowasa. Kwao wanamuona kuwa Lowasa ni mtu ambaye atakisaidia chama chao kushinda urais wa 2015. Wao wanaamini kuwa LOWASA atatemwa na chama chake kwenye kinyang'anyiro cha urais kitendo ambacho kitasababisha EL ahame chama chake na kujiunga na CDM. Inadaiwa kuwa tayari CHADEMA wamewasilisha mpango wao kwa EL. Hata hivyo, taarifa za ndani zinasema kuwa Lowasa amewaambia live kwamba ikiwa ataamua kugombea urais, basi itakuwa ni kwa tiketi ya CCM kauli ambayo imewakatisha tamaa sana. Baada ya kugonga mwamba kwa Lowasa, inaelezwa kuwa Sumaye na Mama Anna Kajumulo Tibaijuka ni miongoni mwa wanaopendekezwa na Mzee wa Tengeru katika nafasi ya Urais.
Plan C ya CHADEMA ni kuanzisha muungano fake na vyama vingine vya siasa. Kwa kuanzia wameunda umoja ujulikanao kama UKAWA. Ingawa umoja huo lengo kuu ni kupigania Rasimu ya Katiba ya Jaji Warioba, inaelezwa kuwa lengo kuu ni kuwahadaa wanasiasa mahiri wa vyama vingine kama akina Prof Ibrahim Lipumba na James Mbatia. Hapa CHADEMA wanajifanya sitaki nataka. Kwamba, CHADEMA wametoa matamko kuwa UKAWA itasimamisha mgombea mmoja tu katika ngazi ya Rais. Mapendekezo ya awali ni kumsimamisha Mchungaji Christopher Mtikila. Hata hivyo, inadaiwa kuwa James Mbatia, Ibrahim Lipumba na wahafidhina wa CHADEMA wamekataa mapendekezo hayo. Lipumba anadai kuwa ndani ya UKAWA, yeye ndiye Msomi na mkongwe kwenye siasa kuliko wote. Hivyo amewapa masharti kwamba ikiwa UKAWA wataamua kusimamisha Mgombea Urais mmoja, basi wamteue yeye kuwa mgombea. Hata hivyo mzee wa Tengeru amekataa pendekezo hilo la Lipumba kwa sababu zinazojulikana.
Kwa hali hiyo, mipango yote ya CHADEMA Yaani Plan A, B na C imekwama. Wamebaki kutapatapa tu na washauri wao akina Saed Kubenea wanaonekana kukosa kabisa mbinu za kukinusuru chama.
Nawasilisha.