The Palm Tree
JF-Expert Member
- Apr 13, 2013
- 7,951
- 12,535
It sounds awkward, lakini ndivyo ilivyo. Kwamba iweje ofisi kuchomwa moto iwe ni jambo jema? Iweje msafara wa mgombea Urais Tundu Lissu ushambuliwe mbele ya macho ya polisi liwe jambo jema? Iweje Tundu Lissu ashambuliwe kwa Risasi za kivita za SMG na AK47 iwe ni jambo jema?
Well. Tufutane ili kunielewa.
Mungu aliyetuumba, wakati mwingine huachilia matukio mabaya kutendeka ili ikiwa ni ishara ya kusudi jema la Mungu juu yetu.
Kwa wasomaji wa Biblia naomba warejee hadithi ya Ayubu ktk Biblia. Sio kusudi langu kwenda ndani sana juu ya maisha ya mtu huyu.
Lakini itoshe kusema tu kuwa, ni miongoni mwa watu wachache ktk uumbaji wa Mungu waliopitia nyakati ngumu na za kutisha katika maisha yao.
Katika fikra na mawazo ya wanadamu ni kama vile Mungu alikuwa anamwadhibu Ayubu kwa dhambi zake. Lakini ukweli siyo hivyo. Hali hiyo ya mateso ya Ayubu, iliachiliwa na Mungu mwenyewe ili yeye huyu Mungu kitambo kidogo mbele, apate kujitukuza kupitia shida na mateso ya mtu huyu na kwa hakika ndivyo ilivyokuwa.!
Kwa hiyo, tunaweza kusema hivi. Ndani ya shida na mateso ya Ayubu, alikuwemo Mungu mwenyewe akitenda kazi yake.
Yuko mtu mwingine ndani ya Biblia aitwaye Yakobo ambaye baadaye alibadilishwa jina na kuitwa Israel.
Huyu ndiye baba wa watoto 12 na ambao hawa watoto ndiyo wanaunda kabila 12 za Israel kwa majina yao wakati huo na mpaka sasa. Hawa (not) in chronological order ni Reuben, Simeoni, Lawi Yusufu, Benjamin, Yuda, Zabuloni, Isikari, Dani, Asheri, Gadi na Naftali.
Ilitokea kuwa mmoja wa watoto wa mzee Yakobo aitwaye Yusufu (Joseph) aliyempenda sana, wakiwa ktk kuchunga ng'ombe, mbuzi na kondoo wa baba yao nyikani, nduguze wa kuzaliwa kwa sababu ya wivu wa kutoona ndugu yao akifanikiwa, waliamua kumuuza kwa wafanyabiashara wa watumwa wa Misri ili kujaribu kuizima nyota yake iliyokuwa inang'aa kuliko za nduguze.
Baada ya Yusufu kuishi miaka mingi Misri akiwa mtumwa, hatimaye kukatokea njaa kubwa duniani kote.
Chakula kilikuwa kinapatikana Misri tu. Watu wote walifunga safari kwenda Misri kununua chakula wakiwemo nduguze Yusufu kutoka nchi ya baba yake, Mzee Yakobo.
Yusufu wakati huo licha ya kuishi katika nchi ya utumwa ya Misri Mungu alimuinua na akatokea kukubalika na Mfalme Farao wa Misri hata akampa cheo cha Uwaziri Mkuu na ndiye aliyehusika na utunzaji wa ghala zote za chakula ktk nchi ya Misri yote.
Ni kweli na hakika kuwa, hakuna Majuto katika kumtumaini na kumtegemea Mungu katika maisha.!
Watoto ya Yakobo walifika nchini Misri kununua chakula mara ya kwanza. Wakapokelewa na ndugu yao Yusufu mwenyewe. Yusufu aliwatambua. Wao walishasahau, hawakuweza kumtambua ndugu yao.
Kilichowashangaza, ni kupewa chakula kwa kadiri walivyohitaji na baadaye wakiwa njiani kurudi nyumbani kwao, waligundua kuwa ndani ya magunia yao fedha yao waliolipa kwa ajili ya chakula hicho, iko imefungwa ndani ya magunia.
Walipofika nyumbani walimsimulia baba yao namna "mtu huyo" (bila kujua kuwa ndiye ndugu yao waliyemuuza) alivyowatendea.
Baadaye chakula kiliisha. Ikawalazimu tena kusafiri kwenda Misri kununua chakula. Safari hii wakakumbana na kikwazo kidogo.
Wakaambiwa, kabla ya kuchukua chakula, sharti warudi kwanza nyumbani wakamlete ndugu yao mdogo aitwaye Benjamin.
Bila kusita, walirudi nyumbani na kumweleza tena baba yao yote waliyoambiwa na "yule mtu". Na wakamwambia kuwa, mtu huyo amemtaka Benjamin (Mdogo wao) kwanza ndipo atakapowapa chakula.
Ndipo Mzee Yakobo alipolia kwa sauti akilalamika kwanini hayo yatokee kwake? Alipoteza mtoto wa kwanza Yusufu, na Benjamini tena akapotee? Mzee hakutaka hili litokee.
Ambacho hakutambua Mzee Yakobo, ni hiki:
Ndani ya matukio yote hayo alikuwemo Mungu mwenyewe akiyaratibu kwa ajili ya kusudi lake maalumu kwa familia yote ya Yakobo na ulimwengu leo kwa ajili ya utukufu wake Mungu mwenyewe.
Sio kusudi langu kusimulia hadithi hii ya kweli ya kihistoria. Lengo langu ni kuwapa ujumbe muhimu CHADEMA, kwamba siyo kila tukio ni adhabu kwenu kwa sababu iwayo yoyote. Matukio mengine yenye sura ya ubaya na kuhuzunisha ni kwa ajili uzuri ujao.
Matukio mengine yaanaachiliwa kwa ajili ya kusudi maalumu la Mungu.
Lilianza la ndugu yetu Tundu A. Lissu kushambuliwa mchana kweupe na Risasi nyingi. Mungu alimlinda, yuko hai mpaka sasa.
Jana alhamisi trh 13/8/2020 ofisi za chama chenu Kanda ya Kaskazini huko Arusha imechomwa moto na watu "wasiojulikana".
Leo ijumaa trh 14/8/2020 msafara wa Tundu Lissu umeshambuliwa Hai Kilimanjaro na watu "wasiojulikana".
Naomba niwape hii tip. Kwamba, haya yanatokea siyo kwa sababu mna dhambi ama mmekosea mahali fulani, HAPANA.
Hampaswi kulalamika. Mtukuzeni Mungu kwa sababu kibinadamu ni mabaya, ni uonevu, unyanyasi lakini ndani yake yumo Mungu - Yehova ili kutimiza kusudi lake jema kwenu na taifa hili zuri la Mungu (Tanzania) na watu wake.
Matendo yao mabaya, ndiyo kukosa kwao. Ndiyo kupotea kwao
Mungu awabariki sana.