Narudisha shukrani zangu za dhati kwa Mwenyezi Mungu baada ya kumuona Makamu wa Rais Dkt. Philip Mpango akiwa mzima wa afya njema

TAJIRI MKUU WA MATAJIRI

JF-Expert Member
Dec 1, 2010
5,720
10,220
Mwenyezi Mungu asifiwe sana. Hakika anastahili sifa, utukufu, heshima na adhama kwa matendo yake makuu.

Leo ninefarijishwa sana baada ya kumuona Makamu wa Rais Dr. Phillip Mpango akiwa ni mzima wa afya njema na akiwa na furaha tele machoni pake.

Kwa kipindi cha zaidi ya mwezi mmoja mheshimiwa Makamu wa Rais hakuonekana popote na wala hakusikika, hali ambayo iliketa taharuki na sintofahamu miongoni mwa Watanzania wengi, sio mijini tu bali hata vijijini.

Ukimya huo ulitoa nafasi ya Watanzania wengi kuanza kuhoji na kuuliza alipo mpendwa wao, asiye na makuu wala baya na mtu, mnyenyekevu na mwenye hekima na busara ya kipekee asiye na kifani ndani ya serikali na chamani kwa ujumla wake.

Waswahili wanasema kwenye wengi pana mengi. Yaliongelewa mengi na mengine ya kutisha na kuogopesha, ndiposa tukaona kuna haja ya kumuombea ulinzi wa Kimungu mpendwa wetu Makamu wa Rais.

Hakika leo tarehe 10 Dec 2023 Mungu amejibu maombi yetu baada ya kumleta mpendwa wetu hadharani na tumemuona kwa macho yetu halisi.

Jambo hili pia lina funzo kubwa sana kwa serikali yetu tukufu. Viongozi wetu wa nchi sio watawala wetu na wala sio miungu watu (labda itokee wakawa wanajiona hivyo). Viongozi wetu ni watumishi wetu.

Kwa kuwa sisi ndio maboss wao tuliowapa hizo nafasi walizozikalia, basi wakiwa wanaenda nje ya nchi kwa ajili ya shughuli mbalimbali wawe wanatuaga, kwani hata hizo ziara zao hugharamiwa na fedha zetu wananchi.

Pia kuna haja ya kurudisha zama za ukweli, uwazi na uwajibikaji. Kuna baadhi ya Viongozi wa juu walishawahi kudanganya huko nyuma, na hawaaminiki kabisa kwa wananchi. Viongozi hao wasitumike kutoa majibu kipindi cha maswali magumu kwasababu hawaaminiki kabisa.


ZAB 95

Mwito wa Kuabudu na Kutii


1. Njoni, tumwimbie BWANA,
Tumfanyie shangwe mwamba wa wokovu wetu.

2. Tuje mbele zake kwa shukrani,
Tumfanyie shangwe kwa zaburi.

3. Kwa kuwa BWANA ni Mungu mkuu,
Na Mfalme mkuu juu ya miungu yote.

4. Mkononi mwake zimo bonde za dunia,
Hata vilele vya milima ni vyake.

5. Bahari ni yake, ndiye aliyeifanya,
Na mikono yake iliumba nchi kavu.

6. Njoni, tuabudu, tusujudu,
Tupige magoti mbele za BWANA aliyetuumba.

7. Kwa maana ndiye Mungu wetu,
Na sisi tu watu wa malisho yake,
Na kondoo za mkono wake.
Ingekuwa heri leo msikie sauti yake.

NB:
JamiiForums huu uzi usiunganishwe na uzi mwingine kwani uzi huu ni wa kipekee kimaudhui ukiwa na lengo moja tu kumrudishia Mungu sifa, heshima, utuku pamoja na kumshukuru kwa ajili ya afya ya mpendwa weyu mheshimiwa Makamu wa Rais Dr. Phillip Mpango
 
Serikali ijifunze kuwaheshimu wananchi, wakiulizia walipo viongozi wao wajibiwe na watu credible sio mijitu yenye historia ya kudanganya danganya
 
Back
Top Bottom