benzemah
JF-Expert Member
- Nov 19, 2014
- 1,504
- 3,034
Chama cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Manyara kimefanya kikao leo Jumapili Novemba 26, 2023 kujadili sakata la Mbunge wa Babati Mjini, Pauline Gekul anayekabiliwa na tuhuma za ukatili na udhalilishaji, na kesho Novemba 27, 2023 kitatoa tamko lake.
Gekul anatuhumiwa kutoa maelekezo kwa kundi la vijana wake kumwingizia chupa mfanyakazi wake, Hashim Ally au kumpiga risasi kwa madai kwamba alitumwa kimkakati kwenda kwenye hoteli yake ya Paleii Lake View Garden.
Sakata hilo liliibuka baada ya video kusambaa mitandaoni ikimwonyesha Hashim akieleza jinsi alivyofanyiwa ukatili huo na Gekul ambaye hadi jana, alikuwa ni Naibu Waziri wa Katiba na Sheria, kabla ya uteuzi wake kutenguliwa na Rais Samia Suluhu Hassan, jana usiku.
Akizungumzia sakata hilo leo Novemba 26, 2023, mwenyekiti wa CCM mkoa wa Manyara, Peter Toima amesema wako kwenye vikao kwa ajili ya kujadili suala hilo, akiahidi kesho, atafutwe, atakuwa na maelekezo kamili.
Chanzo Mwananchi
====
Zaidi soma:
Naibu Waziri na Mbunge Pauline Gekul adaiwa kumfanyia Ukatili wa Kimwili Mtoto
Breaking News: - Rais Samia Suluhu atengua uteuzi wa Pauline Gekul saa chache baada ya kutuhumiwa kufanya unyanyasaji
Pauline Gekul ajibu tuhuma za kumdhuru na kumdhalilisha kijana
Pauline Gekul anastahili kuvuliwa uanachama na kufikishwa mahakamani haraka sana. Amekichafua na kukipaka matope chama