Mbona Waziri Dorothy Gwajima yupo kimya sakata la Pauline Gekul?

GRAMAA

JF-Expert Member
Nov 1, 2014
1,155
3,399
Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum mbona upo kimya sana kuhusu hili sakata la Naibu waziri wa katiba na sheria Pauline Gekul?

Dorothy Gwajima hujawahi kukaa kimya kiasi hiki linapotokea jambo la kuzalilishaji na unyanyasaji wa kijinsia kiasi cha kijana mdogo kuingiziwa chupa sehemu ya haja kubwa na Naibu waziri!

Dorothy Gwajima kama uliweza kujitokeza kwa mbwembwe za hali ya juu na kuwananga na kuwasema walimu eti kisa tu wameruhusu kuucheza wimbo wa Zuchu wa Honey. Mbona hili jambo la Gekul umekaa kimya kama vile hulioni?

Wewe huwa unajinasibu kuwa unapinga sana unyanyasaji wa kijinsia na hupendi kuona raia akifanyiwa kitendo cha kinyanyasaji. Sasa mbona hili la Gekul umekausha kimyaaaaa?

Zile mbwembwe zako za kwenye media hasa linapotokea jambo lolote la unyanyasaji wa kijinsi mbona kwa Gekul hatukuoni!

Mbona hutoi matamko yako ya mbwembwe nyingiiiiiiiiiiiiiiii kama tulivyokuzoea!

Kuna siri gani kati yako na Pauline Gekul mpaka "umeufyanta"?

---
Pauline Gekul ambaye ni Mbunge wa Babati Mjini anatuhumiwa kumfanyia unyanyasaji vijana wawili ambapo inadaiwa akishirikiana na watu wengine waliwadhuru mwili na kumuingiza chupa sehemu ya haja kubwa ili wakiri kutumwa kufanya uhalifu. Zaidi soma Naibu Waziri na Mbunge Pauline Gekul adaiwa kumfanyia Ukatili wa Kimwili Mtoto

Saa chache baada ya habari kusambaa kuwa Pauline Gekul amefanya uhalifu, Rais Samia alitengua uteuzi wake wa Naibu Waziri wa Katiba na Sheria, lakini barua ya Ikulu haikuelezea sababu ya utenguzi wake. Zaidi soma Rais Samia atengua uteuzi wa Pauline Gekul saa chache baada ya kutuhumiwa kufanya unyanyasaji kwa mtoto

Baada ya Pauline Gekul kutenguliwa, wanaJF walisema asiishie hatua hiyo bali anatakiwa kuvuliwa uanachama na kufikishwa mahakamani. Zaidi soma Pauline Gekul anastahili kuvuliwa uanachama na kufikishwa mahakamani haraka sana. Amekichafua na kukipaka matope chama

Habari nyingine soma viunganishi hapa chini
 
Right to presumption of innocence until the court proves otherwise. Ninashangaa Samia ametumia kigezo gani kumtumbua! Sifa za kijinga na mob psychology zinatuharibu Watanzania.
Sifa za kijinga? Ndio mtindo wa kisasa wa viongozi wa CCM: cheap populism. Samia sio wa kwanza, btw.
 
Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum mbona upo kimya sana kuhusu hili sakata la Naibu waziri wa katiba na sheria Pauline Gekul?

Dorothy Gwajima hujawahi kukaa kimya kiasi hiki linapotokea jambo la kuzalilishaji na unyanyasaji wa kijinsia kiasi cha

Kuna siri gani kati yako na Pauline Gekul mpaka "umeufyanta"?
Nasoma comment
 
Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum mbona upo kimya sana kuhusu hili sakata la Naibu waziri wa katiba na sheria Pauline Gekul?

Dorothy Gwajima hujawahi kukaa kimya kiasi hiki linapotokea jambo la kuzalilishaji na unyanyasaji wa kijinsia kiasi cha kijana mdogo kuingiziwa chupa sehemu ya haja kubwa na Naibu waziri!

Dorothy Gwajima kama uliweza kujitokeza kwa mbwembwe za hali ya juu na kuwananga na kuwasema walimu eti kisa tu wameruhusu kuucheza wimbo wa Zuchu wa Honey. Mbona hili jambo la Gekul umekaa kimya kama vile hulioni?

Wewe huwa unajinasibu kuwa unapinga sana unyanyasaji wa kijinsia na hupendi kuona raia akifanyiwa kitendo cha kinyanyasaji. Sasa mbona hili la Gekul umekausha kimyaaaaa?

Zile mbwembwe zako za kwenye media hasa linapotokea jambo lolote la unyanyasaji wa kijinsi mbona kwa Gekul hatukuoni!

Mbona hutoi matamko yako ya mbwembwe nyingiiiiiiiiiiiiiiii kama tulivyokuzoea!

Kuna siri gani kati yako na Pauline Gekul mpaka "umeufyanta"?
Double standard.
Dkt. Gwajima D
Please.
 
Back
Top Bottom