CCM Kagera yawafukuza madiwani wake 8

CCM Kagera yawafukuza madiwani wake 8

Maigizo haya yataigarimu CCM na faida ni kwa CDM!
CC ya CCM itakubali kutoa hiyo sandakalawe amina mwenye kupata apate na mwenye kukosa akose????huu utakuwa ni muda mwafaka wa CDM kuiaibisha ccm.
 
It is very very interesting kwamba kwa CCM wanaopinga ufisadi ndio hufukuzwa katika chama lakini yale mafisadi, majambazi, majangili, na mauza unga yaliyokubuhu ndio kwanza yanaachwa na hata kupewa nafasi za juu za uongozi katika chama, serikalini, na bungeni.

Hili linashangaza sana! Hivi CCM wanaweza kuwaeleza wananchi sababu ya msingi na inayoingia akili ya kuwafukuza hao madiwani zaidi ya bla bla za kisiasa za akina Nape?

Hilo nadhani halihitaji ufafanuzi wowote. Ukikumbuka Richmond na tume yake, halafu maamuzi ya serikali ya CCM, ukakumbushia lile sakata la "kujivua gamba" tena kwa mkwara wa mwenyekiti wake JK na utekelezaji wake, utakuwa na jibu sahihi CCM ina msimamo gani kuhusu ufisadi na kukosa uadilifu. Pamoja na kuwa haisemwi hadharani ni vema ikakumbukwa kuwa hata mwenyekiti wake anatuhumiwa kusababisha ufisadi katika wizara aliyokuwa anaisimamia kabla ya kuwa Mwenyekiti wa CCM taifa. Na ni huyohuyo mwenyekiti ambaye kwa wadhifa wake kiserikali aliridhia kina Daniel Yona na Bazil Mramba wafikishwe mahakamani kujibu tuhuma za ufisadi na kisha bila haya akaenda kumpigia kampeni mtuhumiwa na kuwaambia wananchi kuwa Mramba ni kiongozi safi na mchapa kazi hivyo apewe kura! halafu utashangaa watu wanangojea matokeo ya kesi wakati zilishahukumiwa!

Bado kuna haja ya wananchi kuambiwa lolote hapo? Ni wazi kuwa uamuzi huo umelenga kumpa nafasi meya anayetuhumiwa kwa ufisadi. Na ninashawishika kuwa uamuzi huo haujachukuliwa bila kupata baraka za juu kwa wenye chama. Kumbuka pia kauli za Mwenyekiti wao alipokuwa kwenye ziara Kagera. Kama kuna anayekumbuka kauli yake Mwenyekiti wao aliwaonya waache "malumbano yasiyo na msingi!".... Wakati madiwani wana hoja ya kuzuia ufisadi wa meya, mwenyekiti aliona ni malumbano yasiyo na msingi!

Naamini wananchi wa Kagera wanapaswa kuona haja ya kufanya mabadiliko kwenye sanduku la kura ili kuondokana na mzigo wa Kongwa bovu la CCM. Wito huu pia ni kwa nchi nzima. Tusipochukua hatua sahihi tutaendelea kuumia.
 
Ni uamuzi mzuri maana utakuza demokrasia ya vyama vingi Tanzania, nashauri hawo waliokuwa madiwani kwa tiketi ya CCM wasihangaike na kukata rufaa, maana huo uamuzi wa kufukuzwa ulikwisha vuja siku nyingi na walilijua hilo na walikuwa tayari kuupokea. Hivyo basi jambo la msingi ni kuiomba wizara husika nadhani ni TAMISEMI na Tume ya uchaguzi NEC watangaze hizo nafasi kuwa wazi kwa mjibu wa sheria ya uchaguzi na uchaguzi ufanyike kwa wakati ili wananchi wa hizo kata zilizo wazi wapate wawakilishi wapya. Hii itakuwa nafasi adhimu ya CCM kujipima na vyama vingine kama wanaweza kufanya kama walivyofanya Chadema katika jiji la Arusha, aidha ni nafasi mjarabu kwa vyama vya upinzani hasa CHADEMA kuendelea kuionesha CCM kuwa mwisho wake wa kutawala umekwisha ikibidi kwa kushinda hizo kata kwa zaidi ya viti vine.

Nawatakia kila la heri vyama vya upinzani hasa CDM kama uchaguzi huo utaitishwa mapema iwezekanavyo.
 
naona ccm wanapave way to comrade lwakatare.
 
tayari hizo kata ni zetu kilainiiiii,M4C piga kambi huko mapema,ila hao madiwani ni wazalendo nashauri wajigeuze waje wavalishwe magwanda wagombee kwa tiketi ya chama chetu cdm,mnaonaje wadau?

Hapana nitapinga! Tuna watu walio competent kuliko hizo takataka ambazo baadaye zinaweza kurudi kwao. Hatuhitaji wanachama kwa sababu ya kugombea vyeo tu. wakitaka kombati wavae na wakae miaka angalau 5 wakaiangaliwa mienendo yao kichama. Hatutaki wakina Shibuda wengine!
 
Usikute ni mradi wa Josephine Mushumbuzi yule mama ni mjasiriamali mzuri sana na anajua kuzitumia rasilimali za chama
Hivi hiyo nyumba wamepanga upande kwa kiasi gani?
 
Wanaiga CHADEMA? Ni bora sasa watuachie kata zetu hizo.Cha moto watakiona!

Mkuu Bukoba inashangaza. Nimefika huko nimeishi zaidi ya miezi mitatu. Sio rahisi hicho ulichokisema. Muleba labda, kwakuwa hadi sasa Ansbert Ngurumo anewashiwa taa ya kijani na wananchi wake...
 
Inakuwaje leo Nape ? Chadema walipo wafukuza madiwani wa Arusha uanachama mlichonga sana sasa kwenu inakuwaje ? Haya wacha tuone marudio ya uchaguzi itakuwaje tena .
kwa ufupi CCM ndo imepoteza kabisa hivyo viti vya udiwani.
 
CDM mwaka huu Mung anatupenda sana kata 8 ukiongeza 10 za awali ni 18 na ccm 16 tutakuwa tumewapiga bao la kisigino.
Hiki chama ndio kimetufikisha hapa tulipo'' stand still''wamelaniwa na kukataliwa na Mwenyezi Mungu.Nchi ni kama haina Mwenyewe.
 
CCM YAFUKUZA MADIWANI: Chama cha Mapinduzi kimewatimua madiwani wake nane huko mkoani Kagera na kuwavua nyadhifa zao zote kwa madai ya kuhujumu chama.
 
CCM wanalifahamu hilo mkuu, na hapa wanazuga tu madiwani wao baadae watawarudisha kupitia vikao vya juu!!!

Vikao vya juu lazima viwarudishe sio rahisi kujua kuwa watapoteza makapi haya!
 
Wakati nikiwa mwangalizi wa Uchaguzi jimboni mwaka 2010, kata za Kashai, Ijuganyondo, Hamugembe, na Buhembe CCM walipita kwa mbinde!Lakini kumfumuza Ruhangisa ni kujiua zaidi mkoani Kagera maana yeye ni mzee wa kuchaguliwa bila kuwepo!

Hivi mahamuzi haya yalipata baraka za CCM makao makuu kweli au ni mahamuzi ya kutaka kuwakingia kifua marafiki zao wenye ajenda za siri kuhusu manispaa. Tuwe wakweli hapa, binafsi naona maslahi binafsi ndio yalikaa kwenye drive's seat katika mahamuzi haya ambayo yata-cost chama tawala an arm and leg!! Busara hisipo tumika na badala yake viongozi walio pewa dhamana ya kuongoza Mkoa na chama tawala Mkoani wakaendekeza mambo ya kukomoana kwa kujaribu kuwalinda marafiki zao at all cost basi kosa hilo litakigharimu chama tawala dearly.

Sakata zima hili ni kuendekeza urafiki tu, hakuna cha kusema wamefikia uhamuzu huo eti kukinusuru Chama tawala au nini sijui - hapa wanataka kumunusuru MEYA sio chama, nashangaa kwa nini Mzee Mang'ula na mzalendo Mh.Kinana hawalioni hilo.Sioni kama uhamuzi huo una manufaa yoyote ya kuendeleza manispaa ya BUKOBA na mkoa wenyewe, wahusika wakuu wote wako radhi CCM ipoteze Ubunge 2015 kutokana na ukosefu wao wa busara wa kuto ona mbali - chama kisiruhusu watu wachache kutumia madaraka yao vibaya kwa kuendekeza mambo ya urafiki kwenye maslahi yanayo gusa maendeleo ya kweli ya manispaa na mkoa wa Kagera kwa jumla.

Wala sishangazwi kilicho tokea! mtu usitegemee Mchina Xu Wang akampinga Mchina mwenzake Chen Tsing at the end of the day watakubaliana kwa kila kitu hata ambacho hakina tija kwa chama TAWALA.
 
Karibuni CHADEMA bhandugu. Nadhani Kesho watakabidhiwa kadi za CHADEMA rasmi. Magamba wanaiga ilivyokuwa Arusha wakidhani watazirudisha kata hzo kwao baada ya uchaguzi wakati ndo inakula kwao direct. Wapi Mwigulu Nchemba bin Nape Nnauye?
 
Back
Top Bottom