CCM Kagera yawafukuza madiwani wake 8

CCM Kagera yawafukuza madiwani wake 8

Naona unataka kamati kuu ya CCM itengue maamuzi ya mkoa.Shhhhh taratibu mkuu
Ben Saanane,

Vipi hii....

Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kimechukua uamuzi mgumu wa
kuwafukuza uanachama madiwani wa Arusha walio kaidi maelekezo ya
kamati kuu waliyopewa baada ya kuingia muafaka na CCM.
Madiwani hao ambao walikaidi maagizo ya kamati kuu na hivyo
kunyang'anywa uanachama watapoteza sifa ya kuwa madiwani na uchaguzi
utaitishwa upya. Majina yao ni:-
1. Estomih Mallya
2. Charles Mpanda
3. Rehema Mohamedi
4. John Bayo na
5. Ruben Ngowi.
 
Last edited by a moderator:
Nimeangalia taarifa ya habari kutoka kituo cha itv usiku huu,nimesikitishwa na kushangazwa sana na taarifa ya kufuzwa kwa madiwani 8 huko Bukoba.kinachoonekana ni kwa kwamba kila anayechukizwa na wizi wa pesa za inchi hii ni adui mkubwa wa CCM,wametetea kuliwa kwa mamilioni ya pesa za wananchi badala ya kuungwa mkono na kusaidiwa wanaishia kufukuzwa?hii ni aibu kubwa kwa chama hiki.hakina huruma hata kidogo na watanzania,hii ni ishara ya wazi kuwa CCM ni wezi,ni majambazi wa mali za umma.Nawasihi wa TZ wenzangu tusikubali kufanywa wajinga na CCM tuikatae katakata,ujinga si ugonjwa hauhitaji dawa yoyote wala kwenda hosp,ni jambo la maamuzi tu.huitaji degree kutetea rasilimali za inchi hii.
 
Mbunge si naye alikuwa katika kundi hilo la kumpinga Meya, mbona yeye hayumo katika orodha?

Hawawezi kufikiria kumvua mbunge wao uanachama maana wanafahamu fika wakifanya hivyo tu jimbo limeondoka na kuacha bad precedence!
 
Wamejipaka matope,watu wanaopinga ufisadi ndio wanaofukuzwa...ama kweli akili ndogo haiwezi kutawala akili kubwa.Kwa upande wetu CHADEMA huo ni ushindi wa kata zote 8,CCM mtakufa bila kujijua

Hapo kidogo inachanganya, maana inasemekana kwamba hawa madiwani wlikuwa wanaungwa mkono na Kagasheki, hao hao inasemekana walikuwa wanapinga ufisadi. Swali, kama wanaungwa mkono na Kagashaki, je Kagasheki naye ni mpinga mafisadi?
 
Katiba mpya ifute huu ujinga pesa iliyotumika kwenye uchaguzi wa hawa madiwani ni nyingi sana pesa itakayotumika kufanya uchaguzi mdogo ni mara tatu ya gharama kufanya uchaguzi wa kawaida tuweke utaratibu chama kikiwafukuza madiwani inatakiwa wafukuzwe uanachama peke yake ila nafasi ya udiwani waendelee hadi uchaguzi mkuu utakapofanyika
 
Kawaponza Kagasheki hawa. Jamaa alikuwa anawatumia na kuwalipa kwa manufaa yake mwenyewe na wao wakingia mkenge. Haya ndio malipo kwao. Mwenzao ka save. Lakini nashangaa kile kikao kwa nini hakikumchukulia hatua na yeye huku wakijua dhahili kwamba yeye ndiye muasisi na mpigaji wa debe wa jambo hili?
Alafu kafukuzwa mwenyekiti wa wilaya uanachama kisha mnasema mnaviachia vyombo vya juu kuamua? Kuamua nini wakati yeye si mwanachama? Hivi anaweza kuitisha vikao vya wilaya kama kiongozi wa chama?
Too much contradictions?
Fukuza na Kagasheki bila hivyo shida itaendelea kuwepo manispaa ya Bukoba.
 
Katiba mpya ifute huu ujinga pesa iliyotumika kwenye uchaguzi wa hawa madiwani ni nyingi sana pesa itakayotumika kufanya uchaguzi mdogo ni mara tatu ya gharama kufanya uchaguzi wa kawaida tuweke utaratibu chama kikiwafukuza madiwani inatakiwa wafukuzwe uanachama peke yake ila nafasi ya udiwani waendelee hadi uchaguzi mkuu utakapofanyika

Waendelee wakati walowaweka wamewakataa?
Mawazo bora ni chama kuchagua mtu mwingine wa kuchukua nafasi yake!
 
nimeipenda, ila nina waswas kama uchaguz utafanyika mapema... CCM inaiga CDM.. hapa kaz sasa!
 
Back
Top Bottom