CCM Kagera yawafukuza madiwani wake 8

CCM Kagera yawafukuza madiwani wake 8

Naona ikifika wakati wa uchaguzi mdogo kuziba hizo nafasi. Mawaziri wote na wakuu wote wa mikoa na wilaya watahamia huko. Maana kama ccm imefanya maamuzi magumu inabidi ipigane kuhakikisha haiabiki.
 
.....1.Kashai-Amefukuzwa
2. Miembeni-Amefukuzwa
3.Miembe-Amefukuzwa
4.Nyanga-Amefukuzwa
5.Hamugembe-Amefukuzwa
6.Kitendaguro-Amefukuzwa
7.Ijuganyondo-Amefukuzwa
8.(1)Kagondo-Amebaki (CCM) (Meya Amani)
9.(2)Nshambya-Amebaki(CCM)
10.(3)Kahororo-Amebaki(CCM)
11.Bilele-Amebaki(CUF)
12.Kibeta-Amebaki(CHADEMA)
13.Bakoba-Amebaki(CUF)
14.Rwamishenye-Amebaki(CHADEMA)
XXXXXXXXXXXXX

Kujua historia ya chanzo cha yote hapa fungua hapa chini.
Historia ya mgogoro wa kisiasa Bukoba manispaa


Baadaye nitaingiza video.


Nimeipenda hii! Safi sana. Rudieni uchaguzi muipe CHADEMA uongozi wa Halmashauri hiyo! Yaani CCM inafurahisha sana siku hizi! Safi hiyo kwa kuifanyia CHADEMA kampeni! Tena hao madiwani sasa hivi wanachekelea kwani Baraza jipya la madiwani wao watapita, kwani wamefukuzwa kwa KUWATETEA wananchi. Hawakutaka kujinufaisha. Huo ndio msimamo unaotakiwa. Ati mtu ununuliwe kwa Shs. Mil 20? Ili iweje? Mie hata Bilioni moja SINGEPOKEA! Pesa ya Shetani daima humtookea mtu puani, pamoja na damu mbichi!

Tena uchaguzi urudiwe ndani ya mwezi mmoja tu, mwasikia nyie wa Tume ya Uchaguzi? Hizo siku 90 za nini huku watu wanakosa uwakilishi wa kweli? Mkichelewa kuna Bilioni 2.4 ambazo zitawatokea puani wananchi!
 
Mzee wangu Samuel Luangisa aka "ndivyo ninavyowasingada" hata ww umebadirika? Ama kweli ukombozi umekaribia Kagera...Katarahiya Mujuni Joseph rudi uokoe chama Bukoba Mjini
 
safi sana CCM KAGERA, madiwani hao wa CCM waliofukuzwa, kwa pamoja na wale wa CHADEMA na CUF na waandishi uchwara wa TANZANIA DAIMA walihongwa na MBUNGE ili kupinga maendeleo ya BUKOBA liwalo na liwe.
 
Kwenye sakata hili kuna pande mbili kila moja likituhumu lenzake:

1. Upande mmoja ukiongozwa na Kagasheki na hao wabunge waliofukuzwa wakiwa wafuasi wake pamoja na mbunge wa viti maalum Chadema, na baadhi ya madiwani wa kuteuliwa chadema na Cuf

2. Ukiongozwa na Meya Amani akiungwa mkono mkono na madiwani nane wa CHAMA CHA MAPINDUZI, madiwani wawili wa CHADEMA, diwani mmoja wa CUF, wabunge wawili wa viti maalum CHAMA CHA MAPINDUZI, Mkuu wa Mkoa wa Kagera, Viongozi wa juu wa mkoa CHAMA CHA MAPINDUZI na baadhi ya viongozi wa CHAMA CHA MAPINDUZI wilaya!

Who are the real fisadis in this saga? Na kundi lipi liko sahihi?
 
Asipofukuzwa kagasheki ambaye ndie kiongozi wa maasi na kiongozi wa madiwani hawa nane basi haki haijatendeka.

Nitaiheshimu ccm mkoa kwa kufanya maamuzi magumu kama tu kagasheki nae atavuliwa uanachama. Period

Kagasheki amechangia sana kudumaza maendeleo ya huko, na hao madiwani bila aibu wakashiriki kum-support kwa kutoshiriki vikao vya maamuzi ya maendeleo kwa ujira wanaoujua wao. Acha wavuliwe uanachama tu, hawakuwa na msaada kwa Kagera.
 
Magamba na ufisadi ni kama pete na kidole.Wapinga ufisadi wafukuzwa ufisadi wakumbatiwa.
 
Hivi hiyo katiba ya CMM inampa mamlaka Katibu wa Wilaya kuwafukuza uanachama viongozi wake kama hao madiwani? Au kuna taratibu nyingine?

Kama kuna mtu mwenye soft copy ya Katiba ya CCM ailete hapa tuione na tuichambue.

Ajabu, ati mtu anafukuzwa kwa ajili ya KUWAJIBIKA kwa wananchi? Wananchi si ndio mtaji wa chama chochote kile cha siasa? Sasa tushuhudie uhamaji wa nguvu wa madiwani hao kwenda CCM (watapokewa kwa kuwa waliwajibika wakafukuzwa...) pamoja na wanachama lukuki. 2015 HAIKO MBALI! CCM endeleeni kujiharibia wenyewe kwani sikio la kufa huwa halisikii dawa!
 
Mkuu adolay wameanza kufukuzana baada ya uwindaji wa tembo kuwa mgumu?
Mtu wao juzi kakatika na meno ya tembo kibao analindwa na kinana ndio pesa yao kubwa ya uchaguzi wanategemea itoke kwa wanyama wetu.shame on them.
 
Tunaenda tena kwenye Uchaguzi wa Udiwani wa kata 8.
Huu mgogoro nilishausahau, ulikuwa kama Episode au Tamthilia.

Katibu wa CCM mkoa wa Kagera Bw Avelin Mushi amemaliza Press Conf hivi punde na kufafanua kuwa kikao cha Halmasahuri Kuu ya mkoa wa Kagera imemaliza kikao chake hivi punde na kuamua madiwani 8 wa Manispaa ya Bukoba kufukuzwa katika chama na kufutiwa nyadhifa za udiwani kutoka na mgogoro uliokuwa ukiendelea.

Waliofukuzwa ni:

1. Richard Gaspar (Miembeni )

2. Murungi Kichwabuta (viti maalum)

3. Alexander Ngalinda ambaye pia ni Naibu Meya (Buhembe)

4. Yusuf Ngaiza ambaye pia ni Mwenyekiti wa CCM wa wilaya (Kashai)

5. Deusdedit Mutakyahwa (Nyanga)

6. Robert Katunzi (Hamugembe)

7. Samwel Ruhangisa (Kitendaguro) na

8. Dauda Kalumuna (Ijuganyondo).

Katibu huyo ameongeza kuwa madiwani hao wanaweza kukata rufaa kwa ngazi za juu za chama wakiona hawakutendea haki na kuwa ngazi ya mkoa ina mamlaka ya kufanya hivyo kwa madiwani wa ngazi hizo.

Aidha amesema kwa Bw Yusuph ngaiza amabye ni mwenyekiti wa CCM bukoba,nafasi yake hiyo inasubiriwa ngazi za juu amabazo ndizo zenye mamlaka juu yake(kwa cheo hicho)

Manispaa ya Bukoba ina kata 14 na kati ya hizo kata 4 zinaongozwa na CDM(2) na CUF(2) hivyo kwa Bukoba mjini CCM imebakiza madiwani 3 TU wa kuchaguliwa .kama ifuatavyo
1.Kashai-Amefukuzwa
2. Miembeni-Amefukuzwa
3.Miembe-Amefukuzwa
4.Nyanga-Amefukuzwa
5.Hamugembe-Amefukuzwa
6.Kitendaguro-Amefukuzwa
7.Ijuganyondo-Amefukuzwa
8.(1)Kagondo-Amebaki (CCM) (Meya Amani)
9.(2)Nshambya-Amebaki(CCM)
10.(3)Kahororo-Amebaki(CCM)
11.Bilele-Amebaki(CUF)
12.Kibeta-Amebaki(CHADEMA)
13.Bakoba-Amebaki(CUF)
14.Rwamishenye-Amebaki(CHADEMA)
XXXXXXXXXXXXX

Kujua historia ya chanzo cha yote hapa fungua hapa chini.
Historia ya mgogoro wa kisiasa Bukoba manispaa


Baadaye nitaingiza video.
 
Waitu congratulation wote aambao mumeona kuwa inchi inaenda kubaya mwakora muno kasinge waitu.wacha nikapete karubisi kangu kure kikomera!nasubiri taarifa baaadaye!
 
CCM YAFUKUZA MADIWANI: Chama cha Mapinduzi kimewatimua madiwani wake nane huko mkoani Kagera na kuwavua nyadhifa zao zote kwa madai ya kuhujumu chama.

Kumbe na CCM nao wanapata uchungu wa kuhujumiwa.Wanapo wahujumu wenzao wao wanafikiri wenzao hawapati uchungu.Hawajui kwamba usilo litaka kutendewa usimutendee na mwenzako pia.
 
Back
Top Bottom