CCM Kagera yawafukuza madiwani wake 8

CCM Kagera yawafukuza madiwani wake 8

Katibu wa CCM mkoa wa Kagera Bw Avelin Mushi amemaliza Press Conf hivi punde na kufafanua kuwa kikao cha Halmasahuri Kuu ya mkoa wa Kagera imemaliza kikao chake hivi punde na kuamua madiwani 8 wa Manispaa ya Bukoba kufukuzwa katika chama na kufutiwa nyadhifa za udiwani kutoka na mgogoro uliokuwa ukiendelea.

Waliofukuzwa ni:

1. Richard Gaspar (Miembeni )

2. Murungi Kichwabuta (viti maalum)

3. Alexander Ngalinda ambaye pia ni Naibu Meya (Buhembe)

4. Yusuf Ngaiza ambaye pia ni Mwenyekiti wa CCM wa wilaya (Kashai)

5. Deusdedit Mutakyahwa (Nyanga)

6. Robert Katunzi (Hamugembe)

7. Samwel Ruhangisa (Kitendaguro) na

8. Dauda Kalumuna (Ijuganyondo).

Katibu huyo ameongeza kuwa madiwani hao wanaweza kukata rufaa kwa ngazi za juu za chama wakiona hawakutendea haki na kuwa ngazi ya mkoa ina mamlaka ya kufanya hivyo kwa madiwani wa ngazi hizo.

Aidha amesema kwa Bw Yusuph ngaiza amabye ni mwenyekiti wa CCM bukoba,nafasi yake hiyo inasubiriwa ngazi za juu amabazo ndizo zenye mamlaka juu yake(kwa cheo hicho)


Baadaye nitaingiza video.

Inakuwaje leo Nape ? Chadema walipo wafukuza madiwani wa Arusha uanachama mlichonga sana sasa kwenu inakuwaje ? Haya wacha tuone marudio ya uchaguzi itakuwaje tena .
 
Madiwani 8 ni mtaji tosha!!!

Lakini tuache utani kufukuza madiwani 8 si jambo dogo!! Kwa mara nyingine siasa zinaenda kutuingiza katika gharama za kijinga kabisa!!
ahaaaaa!!ukombozi ni gharama hasa ukombozi wa kifikra.
 


Kupitia ITV Nimesikia taarifa ya kisaliti juu ya CCM kuwafukuza madiwani wake.Nimepitia kwa kina taarifa zinazohusiana na msimamo wa madiwani hawa na kile wanachokipigania.


Nawapongeza madiwani hao 8 wa Kagera kwa msimamo thabiti walioonyesha kukabiliana na ufisadi ndani ya chama chao,halmashauri na mkoa wa Kagera kama wawakilishi wa wananchi wanaouchukia ufisadi.Kwa kuwa wamegutuka na kugundua ufisadi ni nguzo kuu ya kiitikadi ndani ya chama chao na kwa kuwa dhamira iliwasuta na kuamua kusimama ili kuirudisha CCM katika misingi iliyoasisiwa na Mwl.Nyerere,sina budi kuwapongeza kwa hatua hii ya kijasiri.Naomba kila mmoja anayechukia ufisadi aungane na madiwani hawa walioamua kupambana ndani ya chama chao kwa kutumia platform sahihi bila kuvunja katiba.

Chama ambacho kinaona kwamba ni kosa la jinai kupinga ufisadi hakifai kuongoza serikali na wawakilishi wa wananchi wanatakiwa kuwa mfano bora kama walivyofanya madiwani hawa

1. Richard Gaspar (Miembeni )

2. Murungi Kichwabuta (viti maalum)

3. Alexander Ngalinda ambaye pia ni Naibu Meya (Buhembe)

4. Yusuf Ngaiza ambaye pia ni Mwenyekiti wa CCM wa wilaya (Kashai)

5. Deusdedit Mutakyahwa (Nyanga)

6. Robert Katunzi (Hamugembe)

7. Samwel Ruhangisa (Kitendaguro) na

8. Dauda Kalumuna (Ijuganyondo).


Hatuwezi kuwa na taifa adilifu ikiwa hatutashinikiza uadilifu katika ngazi za halmashauri na ngazi nyingine.

Safi sana Ben ccm Ufisadi ni jadi yao na ndio maana hawana ubavu wa kuwafukuza mafisadi lakini wapo tayari kuwatoa kafara watu wachache wanao pambana na ufisadi ndani ya chama hiki,hata makada wao walio wengi wamekuwa wakikalilishwa bila hata kujihoji nini wanaambiwa na viongozi wao kwa mfano mgogoro huu tangu umeanza viongozi wao wakuu wamekwenda Kagera na wamedaganya na kubakia kutoa matamko ya kuwa meya na Kaghasheki watafute suluhu kwa kumaliza mgogoro wao,wakati tatizo ni ufisadi hiki chama ni janga kwa nchi hii,hongera sana madiwani hao kwa kusimamia haki na ukweli,hakika haki itawalinda daima.
 
SANY0104.JPG


UFIPA PROJECT MANYANYA TEAM.

CC; @HAMY-D, @scramble, @Lizaboni, chama,

Mkuu Ritz, ina sikitisha kuona chama kikuu cha upinzani nchini (CHADEMA) kuwa na makao makuu kwenye nyumba ya kupanga ila viongozi wake kutembelea mashangingi (VX V8) kwa pesa ya chama.
 
Last edited by a moderator:
Serikali hii inaendeshwa na ''matukio''ya kutengeneza..
Lengo ni kuwaondoa watu kwenye ishu ya ponda! Hao watarudishwa tu...
 
hawa jamaa ni mashujaa ! msimamo mkali! wasiwababaishe hao mafisadi,karibuni kwa wazalendo(CDM).
 
CCM tangu ilipoanzishwa haijawahi kufanya maamuzi yenye utata wala wasiwasi ninakiunga mkono chama changu katika maamuzi haya.
 
Ccm wajanja sana wanawaondoa kwenye ishu ya ponda na madawa ya kulevya...tred ya madawa na ponda itadoda!
 
Maweee,yooöh bojoo! Ccm kwisha bk. Chadema imewaingiza choo cha kike. Kagasheki kafukuzwa?naye alisaini barua ya kutaka meya afukuze. Mkuru hawezi kumgusa. Kagasheki noterwaa!
 
Wanaiga CHADEMA? Ni bora sasa watuachie kata zetu hizo.Cha moto watakiona!
Yaani hapa hatoki mtu,sipati picha mtanange utakavyokuwa wanajidanganya wakidhani watatwaa kata zote nane kama ilivyofanya CDM arusha weeee!! lazima tutawavua nguo tu,kuanzia sasa hadi 2015 ni miaka ya kumuaibisha shetani.
 
Mkuu
Ritz, ina sikitisha kuona chama kikuu cha
upinzani nchini (CHADEMA) kuwa na makao makuu kwenye nyumba ya kupanga
ila viongozi wake kutembelea mashangingi (VX V8).

mkuu eti tumefukuza wangapi vile!
 
Last edited by a moderator:
MMmmh naona kama trailer ya movie vile. Ngoja nisubiri movie kamili...still loading!!!
 
Back
Top Bottom