Kaka mkubwa kuliko pesa zetu kutumika kununua makahaba Dodoma ni bora zitumike kukuza demokrasia...hizo ndizo gharama na changamoto zenyewe za demokrasiaMadiwani 8 ni mtaji tosha!!!
Lakini tuache utani kufukuza madiwani 8 si jambo dogo!! Kwa mara nyingine siasa zinaenda kutuingiza katika gharama za kijinga kabisa!!
Mmeshikwa pabaya jibuni hoja iliyopo kwanza baadae tutahamia kwenye hiyo nyumba mnayodhani ni issue.kuitetea ccm ni lazima uwe na akili za maiti.Mkuu Ritz, ina sikitisha kuona chama kikuu cha upinzani nchini (CHADEMA) kuwa na makao makuu kwenye nyumba ya kupanga ila viongozi wake kutembelea mashangingi (VX V8) kwa pesa ya chama.
ah ah kwa raha, na ninavowajua wahaya huwa hawatikisi masikio na watafanya kweli kwa kuikataa ccm hadharani
Hapo kata 8 zinaenda CHADEMA
Kwenye sakata hili kuna pande mbili kila moja likituhumu lenzake:
1. Upande mmoja ukiongozwa na Kagasheki na hao wabunge waliofukuzwa wakiwa wafuasi wake pamoja na mbunge wa viti maalum Chadema, na baadhi ya madiwani wa kuteuliwa chadema na Cuf
2. Ukiongozwa na Meya Amani akiungwa mkono mkono na madiwani nane wa CHAMA CHA MAPINDUZI, madiwani wawili wa CHADEMA, diwani mmoja wa CUF, wabunge wawili wa viti maalum CHAMA CHA MAPINDUZI, Mkuu wa Mkoa wa Kagera, Viongozi wa juu wa mkoa CHAMA CHA MAPINDUZI na baadhi ya viongozi wa CHAMA CHA MAPINDUZI wilaya!
Who are the real fisadis in this saga? Na kundi lipi liko sahihi?
Kwa kweli CCM inabidi waishukuru sana CHADEMA, ndio wamewafundisha mambo haya ya kufukuzia mbali wanachama ambao hawana tija kwa chama hata wakiwa viongozi. Anyway, ninawapongeza CCM kwa ukomavu na uthubutu huu, you are growing now!
Khamis Kagasheki kama hakufukuzwa basi wafuasi wake wameonewa na mzizi wa fitina haujakatwa.
Tunaenda tena kwenye Uchaguzi wa Udiwani wa kata 8.
Huu mgogoro nilishausahau, ulikuwa kama Episode au Tamthilia.
Hapo kata 8 zinaenda CHADEMA
- Habari yako mkuu haiko sawa, CCM Mkoa wa Bukoba kwa katiba ya CCM Taifa haina Mamlaka ya Kumfukuza Diwani ni Kamati Kuu ya CCM tu ndiyo yenye huo uwezo, Mkoa unaweza kuwasimamisha tu na kusubiri maamuzi ya Kamati Kuu ya CCM kama kusimamisha huko ni kwa halali su sio halali, lakini kufukuza ni Kamati Kuu tu ndio yenye huo uwezo, so hii habari haiko sawa.
- Madiwani hao 8 tayari wameshaandika kwa CCM Taifa kuiomba itengue uamuzi huo ambao umefanywa na Viongozi walio upande mmoja wa Vita kubwa ya kisiasa ambayo imekuwa ikiendelea katika Manispaa na jimbo la Ubunge la Bukoba Mjini.
- My Take ni CCM Mkoa wamekurupuka na kujidhalilisha sana na this ishu, kwa sababu bado Madiwani wanaweza kwenda Mahakamani na kubaki na Udiwani wao, uwezekano wa Madiwani hao kufukuzwa na Kamati Kuuu sidhani hata kama upo, kwa kuzingatia sababu za msingi zilizowapeleka CCM Mkoa kuwasimamisha, ni aibu sana kwa Viongozi wa Mkoa wa CCM, tena mmoja Katibu Mkuu wa Mkoa akiwa ni rafiki yangu wa karibu sana, ameniskitisha sana na this!!
Le Mutuz