CCM Kagera yawafukuza madiwani wake 8

CCM Kagera yawafukuza madiwani wake 8

Katibu wa CCM mkoa wa Kagera Bw Avelin Mushi amemaliza Press Conf hivi punde na kufafanua kuwa kikao cha Halmasahuri Kuu ya mkoa wa Kagera imemaliza kikao chake hivi punde na kuamua madiwani 8 wa Manispaa ya Bukoba kufukuzwa katika chama na kufutiwa nyadhifa za udiwani kutoka na mgogoro uliokuwa ukiendelea.

...


Mkuu Ritz na genge lenu hapo Lumumba; tunaomba maelezo hapo kwenye red versus shutuma za Nape Nnauye. Nilidhani chama chenu hakina hao watu kumbe hadi mavyeo makubwa makubwa wanayo! Acheni upuuzi wenu, mnakolipeleka taifa letu siko.
 
Last edited by a moderator:
SANY0104.JPG


UFIPA PROJECT MANYANYA TEAM.

CC; HAMY-D, scramble, Lizaboni, chama,
Mbona mpya kila siku jana nyara za taifa, leo mnafukuzana.Mwezi mugumu kwa magamba, ngumu kumeza bali jitahidi utazoea
 
Jamani eehhh hawa waliofukuzwa hawakuwa wapinga ufisadi wowote. Hawa waliingia mkenge kwa kuingilia ugomvi wa mbunge Kagasheki na Meya. Na Kagasheki mwenyewe akawa akiwalipa ili wamuondoe Meya. Tuhuma hizo hata mwenyekiti wao taifa kajaribu kuingilia hivi karibuni na kasikiliza na kuona ni baseless. Sasa hawa pamoja na rais kusema tofauti ziishe kwa kutimiza ilani ya chama chao wao wameendelea kupinga na si hivyo tu mbele ya mwenyekiti wao walikataa kupeana mikono kama dalili za kumaliza mgogoro. Sasa hivi hakuna kitu maendeleo jimbo la Bukoba mjini tokana na mgogoro huu.
Nitakubali kwamba wanapinga ufisadi kama watasema ilani ya chama chao ni ya kifisadi na watazua swali toka kwangu kwa nini waliinadi hadi wapate ushindi? Huo nao ulikuwa ufisadi. Kutaka madaraka kupitia ulaghai?
Kinachoumiza ni kwamba mgogoro huu uliwagawa hata wapinzani. Madiwani wa Chadema waligawanyika na wale wa Cuf pia waligawanyika na kusababisha migogoro kati yao. Bora wafukuzwe.
 
CCM tangu ilipoanzishwa haijawahi kufanya maamuzi yenye utata wala wasiwasi ninakiunga mkono chama changu katika maamuzi haya.


Ha ha ha! Kufukuza wanaopinga ufisadi na kuwaacha mafisadi sio uamuzi wenye utata! Endelea kuota.
 
Hapo ndipo mjue ujinga wa CCM ukowapi, kama wanaweza kufukuza madiwani wanaolilia maslahi ya wananchi na wakaacha wanofanya deal za wizi wazi wazi.

Sasa huko ndo kutekeleza agizo la rais kuhusu viwanja na Soko?

Kiukweli CCM imefutika Bukoba, inajilinda yenyewe? Hooooooh!!!!!!!!!!!
 
Nadhani kabla hata press Conf, haijafikia nusu ulishaanza kuandika post yako hii. Nadhani kuna upungufu wa uelewa..
tulia la ukweli lisimame na ingekuwa kweli...Nitakuambia siku nyingine
 
Vita ya panzi....
Wagombanapo tembo.......
Iga.......
Usiige kunya kwa.......
Kufa...kufaana
Mwenzako akinyolewa....
Ukimnyoshea mwenzako kidole kimoja....
 
Ben kwa wale tunaojua vizuri kiini cha tatizo la mgogoro huu si kweli kwamba hawa ni wapiga ufisadi. Hakuna ukweli wowote. Hawa walikuwa tu wanatumiwa na Kagasheki kwa manufaa yake. Ni story ndefu sana. Ukiisikiliza juu juu unaweza kukubaliana nao ukijua ukweli kwa ndani utagundua hujuma na uongo/propaganda zinavyotumika kuhalalisha walichokuwa wanafanya hawa madiwani. Mimi ni royal to CHADEMA lakini sikubaliani nao kabisa.
 
Mkuu Ritz, ina sikitisha kuona chama kikuu cha upinzani nchini (CHADEMA) kuwa na makao makuu kwenye nyumba ya kupanga ila viongozi wake kutembelea mashangingi (VX V8) kwa pesa ya chama.
Hilo bango hapo wanauza vocha na luku? Huo mradi sijui wa nani.
 
Last edited by a moderator:
tayari hizo kata ni zetu kilainiiiii,M4C piga kambi huko mapema,ila hao madiwani ni wazalendo nashauri wajigeuze waje wavalishwe magwanda wagombee kwa tiketi ya chama chetu cdm,mnaonaje wadau?
 
Hilo bango hapo wanauza vocha na luku? Huo mradi sijui wa nani.
Usikute ni mradi wa Josephine Mushumbuzi yule mama ni mjasiriamali mzuri sana na anajua kuzitumia rasilimali za chama
 
tayari hizo kata ni zetu kilainiiiii,M4C piga kambi huko mapema,ila hao madiwani ni wazalendo nashauri wajigeuze waje wavalishwe magwanda wagombee kwa tiketi ya chama chetu cdm,mnaonaje wadau?
Hampati kata wala mtungi
 
Bila shaka huo ni mweleka kwa CCM, wakae chini wajitafakari vinginevyo tutasikia madiwani hao wamebambikiwa kesi au kufukuzwa nchini wakidai ni wahamiaji haramu tena Wanyarwanda!
 
Mkuu Ritz, ina sikitisha kuona chama kikuu cha upinzani nchini (CHADEMA) kuwa na makao makuu kwenye nyumba ya kupanga ila viongozi wake kutembelea mashangingi (VX V8) kwa pesa ya chama.

Hii ina uhusiano gani na hoja inayojadiliwa hapa?
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom