Mkandara, Kwanini hadi hivi sasa (kabla ya ujio wa CCJ) vyama vya upinzani havijaweza kuungana na kupata huo ushindi?
Mkuu wangu labda nikwambie kwamba limeisha kata tamaa ya ushindi kwa mwaka huu 2010. Nadhani unakumbuka vizuri kwamba hii kazi ya kuomba au kutaka muungano sikuianza jana na kamasikosei tulikuwa sote kabla ya uchaguzi wa mwaka 2005. Nimeendelea kusema hili hata baada ya uchaguzi kwa malengo ya uchaguzi huu na wala sintabadilisha imani yangu ktk Hili. Chadema,CUF,TLP na NCCR kama vyama vya Upinzani wanatakiwa kuungana ili kupata Ushindi. Na nimesikia wameshindwa kufanya hivyo kutokana na Mapandikizi ya CCM ndani ya vyama hivyo. Haya ni madai ya baadhi viongozi niliowahi kuzungumza nao na tatizo hili limezua makundi ndani ya vyama vyote ikiwa ni pamoja na chama tawala.
Kwa hiyo nimepoteza matumaini yangu toka siku nyingi lakini niliweka mlango wazi kwa tumaini jipya. sasa maadam CCJ wamekuja na wanataka kufanya vitu, basi halahala la kwanza kufanya ni kuunganisha watu. Tukumbuke tu chama ni WATU sio Viongozi wanaokijenga chama... Kupata nguvu na support kubwa ya wafuasi wa vyama vya Upinzani inaanza na hatua hii ya Kuungana. Kunyoosha mikono na kuomba kuungana ni Strategic move ya kisiasa ambayo inakupa wewe sauti kubwa kwa wananchi. Watu watajua malengo yenu sii kutawala ila kuwaondoa wananchi ktk adha waliyopo.. Na Umoja wao ndio pekee utawawezesha Ushindi. Nakumbuka Chadema walijaribu hili lakini nao pia kuna ushindani ndani ya chama, kuna makundi na kwa bahati mbaya zaidi wametengwa zaidi na vyama vingine kwa sababu ya hofu ya hao incumbents.
CCJ haina sababu wala haja ya kuogopa Mapandikizi, ni chama kipya ambacho kinatakiwa kuwa na lengo moja tu..Kuing'oa CCM Madarakani, hizi habari za Itikadi ziwekeni kando kwa sasa. Nguvu yenu iwe KUASI (Upinzani) dhidi ya chama CCM kama ilivyotokea kuundwa kwa CCJ. Hivyo itakuwa rahisi kwenu kuwasoma Mapandikizi wanaoingia kama waasi..Na sii rahisi kwa Mapandikizi kuingia chama kinachopingana na CCM kwa kuasi Uongozi..
Hili neno WAASI litumike kwa faida zaidi badala ya kupiga vita kuitwa hivyo. Na moja ya move kubwa mnayotakiwa kuifanya ni kuwavuta wote wanaotaka KUASI (Upinzani) kujiunga nanyi ili kumshinda CCM.. Amini maneno yangu, mtapata wafuasi red shirts kibao kuliko mnavyofikiria kwani wananchi wamechoka na siasa. Wananchi wanataka kuona chama chenye kufanya kweli na hatua ya kwanza ni kutafuta support ya wananchi mkianza na jumuiya zao. Huko ndiko walikoweka imani zao, na any approach yenye malengo ya kumwondoa CCM itapokelewa kwa nguvu zote isipokuwa kama kuna kiongozi atajaribu kuzuia muungano huu wa Mapinduzi itakuwa amejitenga mwenyewe.
Kwa hiyo mkuu wangu, nachojaribu mimi kufanya ni kutoa ushauri dhidi ya CCM..Nimewahi kusema wazi kwamba JK atapita 2010 kirahisi kutokana na upinzani uliopo lakini sijachoka kupigia debe upinzani na kushauri, inapofikia swala la rais nimependekeza Dr.Slaa kugombea ili kuweka ushindani ktk kiti cha rais. Ushindani ambao utampa mtihani mkubwa kiasi kwamba atumie muda wake mkubwa kutafuta ushindi wake, maadam rais au niseme JK ndiye aliwabeba wabunge wengi mwaka 2005, lengo la mtihani huu ni kutompa nafasi ya kutupiga chenga za Messi.
Mwisho, nimekuwa nikifikiria, kusoma na kuuchosha ubongo wangu kutafuta undani wa kila hatua inayochukuliwa na JK au chama CCM..Kwa mfano kulikuwa na dalili kubwa sna ya wabunge wa CCM waliopo sasa hivi kutorudi mwaka 2010, tena kwa hesabu kubwa lakini maamuzi ya huu uchaguzi wa ndani CCM kupitia wanachama ni mfumo bora kwao kuwaondoshaa viongozi wasiopendwa na wananchi (wasiouzika). Kwa hiyo CCM itaonekana imenza kujisafisha toka ndani (changa la macho) hivyo, kwa hatuua hii wajinga wengi wataipokea na najua haitakuwa ushindani rahisi dhidi ya CCM pasipo nguvu ya umoja wa vyama pinzani..
Bila Umoja nakuhakikishia JK atashinda kwa kishondo tena, na CCM watashinda hakuna cha CCJ, Chadema,CUF,TLP, NCCR wala mjomba wake. niliyasema haya mwaka 2005 na narudia tena kusema hatuwezi kuishinda CCM kwa makundi makundi hali jeshi lake ni kubwa kuliko makundi haya..Tunapoteza muda wetu zaidi kuunda vyama, unless hizi nguvu zote za vyama vya Upinzani ni kutafuta KULA (ruzuku).