CCJ kuanza Charm offensive! - Ask your questions!

CCJ kuanza Charm offensive! - Ask your questions!

Ha ha, idont even know yu n so she mght think i ma nuts to try n hook her up 2 someone i dont even no......ntajaribu kumsendia hiyo avatar pic yako,do you have eni sisters?And i know you also got a couple of em chicks in here
I miss Mwafrika wa Kike for real tho..... ha ha!

Just hook me up and the rest we'll sort it out along the way...au hutaki niwe shemeji 'ako bana.....wee mangi vipi
 
Kwa wale ambao wangependa kutoa mawazo ya kiitikadi, mfumo au mwelekeo wa CCJ unaweza kuwasiliana nami. Kumbukeni kama nilivyodokeza mapema mwaka huu, mabadiliko siyo tunayoyangojea, bali tunayojiletea!
 
Hizo Itikadi kaeni nazo mkuu tunataka kuona mnafanya mavitu. Sii mara ya kwanza nimesema hivi, kwani niliwahi kuwa nyuma ya Chadema kwa Itikadi yao mara wakageuka na kuchukua mrengo wa kushoto..
Hivyo maadam Itikadi zilizopo ni mfumo uliopangwa na wazungu kulingana na mazingira yao, kwetu sisi bado kabisa...Ni asilimia 10 ya population wanafahamu maana ya Itikadi inavyojenga mrengo, waliobakia ni maskini wenye njaa akili zao zimefunga kufikiria ama kutambua. Kuwavuta watu kama hawa unatakiwa kuwa na bakuli la Ubwabwa ambalo CCM wamelibeba..
Kazi ni moja tu kuliputa bakuli hilo na sidhani kama Ubavu mnao...Hapa ndipo umuhimu wa kutafuta nguvu mpya toka wanachama wengine kujenga jeshi la kupambana na CCM. Msitegemee sympathy, kwani historia inatuonyesha wazi kwamba Wadanganyika kwa asili yetu ni woga na wanafiki..Ni matunda ya Utumwa mabyo CCJ hamuwezi kuepuka kwa hizi ibada za Kiitikadi..
 
mimi ni mjumbe wa CCJ,kwakifupi tutapata usajiri wa kudumu ingawa tendwa alitaka kutumika na CCM hapo kutunyima ila imeshindikana kwa kuwa kigogo mmoja ambae atahamiahivi karibuni nae anatisha katika taifa hili kamwogopa...nchi tunaichukua 2015

Mambo kama haya ndo wengine humu wanayajua tayari na ndio maana nshangazwa sana na confidence yao,at the same time,hawataki kukubali kuwa majority ya wananchi wanapenda itikadi za ccj lakini watu kama hao ie aliyesaidia Tendwa kufuta mawazo ya kukisajili ccj,basi ndo hao tunawasubiria provided thy aren't in fisadis lists.
 
No staki,naonwa una washwa washwa,sasa Ngabu ni watu wa wapi?Ama nyani?

Nawashwa nini tena na wewe bana? Mimi nimekwanbia nipigie krosi dada 'ako kama vipi we mwambie tu ajiunge hapa halafu mimi ntatema sumu mwenyewe.

Ngabu ni watu wa Congo kwa Kabila
 
Una haki kufanya hivyo, hawa jamaa wanaweza kuipunguzia CHADEMA kura na matokeo yake idadi ya viti maalum ikapungua na hapa ndio chuki inapoingia, noma sana.

Sio kweli..Mkuu mimi nagombea jimbo....lakini kubwa ambalo ni consern yangu ni kujaza vivyama kibao
wakati wote tunadhamira moja ya kumkomboa mwananchi...Ni ukweli kuwa CCJ na CHADEMA ni vyama vinavyofanana kwsana kimtazamo na kifikra..believe me tunapoteza muda kujaza vivyama tunazidi kukipa nguvu chama tawala..Sote tu wahanga si CHADEMA wala CCJ..Hatuigopi CCJ kwa kiwango unachodhani mpaka sasa tunamajimbo amabay
o tunauhakika nayo wa kuyapata hata iweje..ni ukweli siopinga with or without CCJ,CHADEMA itaongeza wabunge mwka huu kama ilivyo kawaida yetu...
 
Citizen ya leo, wamripoti Msajili kasema ofisi yake haina fedha za kuhakiki wanachama wa CCJ.
Lengo la kauli hiyo ya Msajili ni kupima msuli wa wana CCJ, who's is reall behind and can come forward to help out uhakiki.
Lakini pia huu ni wakati wa kupress Ofisi ya Msajili wa Vyama iwe na Mkataba wa Huduma kwa Wateja, (Clients Service Charter) utakao mlazimisha msajili lazima awe ametoa usajili wa kudumu kwa vyama vilivyotimiza taratibu ndani ya kipindi kadhaa tangu kuwasilishwa kwa hati.

Hali ilivyo sasa, hakuna taratibu, sheria wala kanuni inayomguide msajili kutoa usajili wa kudumu, ama lini afanya uhakiki wa wanachama wa chama kipya, all rests upon his own discration.
 
Pasco, msajili wa vyama vya siasa anathibitisha tu kuwa zile chembe zilizoko kwenye ubongo wake hazifanyi kazi sawa sawa. NInasema hivyo kwa sababu msajili wa vyama vya siasa asiposajli vyama vya siasa anaweza vipi kuwa msajili wa vyama vya siasa?
 
wakuu nimekuwa nasoma hoja zenu hapo juu with a gleaming smile on my face.
Naamini kuwa CCJ imekuja kwa nia thabiti ya kutukwamua tulipo ili tusonge mbele.
Mimi nilijiunga kwa njia ya ujumbe mfupi wa mkononi yaani SMS. na sijajutia kufanya hivyo.
Nia yangu ni Tanzania njema kwa kila mtanzania.

ninaamini kuwa tendwa atajifanya kama msaidizi wa ziraili ktk usjaili wa hii kitu yetu. Ila inabidi tuanzishe vuguvugu la ofisi huru ya msajili wa vyama vya siasa. kuna kila dalili hii ofisi si kwa manufaa ya UMMA.
 
Pasco, msajili wa vyama vya siasa anathibitisha tu kuwa zile chembe zilizoko kwenye ubongo wake hazifanyi kazi sawa sawa. NInasema hivyo kwa sababu msajili wa vyama vya siasa asiposajli vyama vya siasa anaweza vipi kuwa msajili wa vyama vya siasa?
.
Yes ni Msajili, ila atatoa usajili anapojisikia, tangu siku ile alipotoa usajili wa muda kwa CCJ, alisema wazi, hakiwezi kushiriki uchaguzi wa mwaka huu kwa sababu, amekipa miezi 6 ya kutafuta wanachama, ila pia alisema mwaka huu wote ofisi yake itaskuwa bize na mambo mengine, hivyo hatakuwa na muda wa kufanya uhakiki. Sasa leo ndio nimemsoma kumbe hana hela za kuhakiki!.

Kisheria hajafanya kosa lolote, hata akiwa na fedha, na akapanga uhakiki wa CCJ kuanza August baada ta NEC kukamilisha mchakato wa wagombea, there is nothing anybody can do, to pressure him.
CCJ Mtafanyaje?, ila a serious note, kama issue ni fedha, it is not!, zipo tele!.
 
Yeye anaitwa Msajili wa Vyama vya Siasa! Kama hafanyi usajili au kuwezesha usajili kufanyika kwa harak ainavyowezekana anafanya mambo gani mengine?

Kisheria hajafanya kosa lolote, hata akiwa na fedha, na akapanga uhakiki wa CCJ kuanza August baada ta NEC kukamilisha mchakato wa wagombea, there is nothing anybody can do, to pressure him.

Nadhani kisheria atafanya makosa kwa sababu sheria inamtaka kutoa usajili wa kudumu kwa chama kilichotimiza masharti sasa hivi inaonekana toka mwanzo ana contempt ya CCJ kwa kauli zake hizo. Lakini they picked the wrong party this time! Believe me they have.

CCJ Mtafanyaje?, ila a serious note, kama issue ni fedha, it is not!, zipo tele!.

Tutafanya kile ambacho kimeshinda vyama vingine kufanya wanapodhulumiwa au kuonewa na watawala.
 
Yeye anaitwa Msajili wa Vyama vya Siasa! Kama hafanyi usajili au kuwezesha usajili kufanyika kwa harak a inavyowezekana anafanya mambo gani mengine?
Anapita huku na kule kuelimisha sheria mpya ya uchaguzi ili isivunjwe na vyama vya siasa (ambavyo hataki kuvisajili !)
 
Kuna mtu anaitwa Abasi Mtemvu, naombeni mnipe list ya vyama alivyozunguka mkianzia na CCM.
 
1. Tatizo la CCJ ni kwamba Wale wapiganaji wa ufisadi wamefyata Mkia. Ndo kusema wameogopa Kumuunga mkono Ndugu yao Mpendazoe. Hivyo kwa Upande wangu ninakuwa na Mashaka nao. Tumaini langu linabaki kwa Chadema yenye wapiganaji mahiri kama Freeman Mbowe na Dr Slaa. Laiti Mpendazoe angekuja chadema Kuongeza nguvu!. Kwa hiyo wadau wangu mnaosubiri CCJ ambayo Msajili vyama anaihofia na kuiwekea kauzibe. Tumaini lenu wekeni kwa Chadema.
2. Hivi huyu ni MSAJILI VYAMA au MSAJILI NYAMA!. Mimi nashaka kama watu hawakukosea wakampa cheo MSAJILI NYAMA badala ya MSAJILI VYAMA.
 
Tutafanya kile ambacho kimeshinda vyama vingine kufanya wanapodhulumiwa au kuonewa na watawala.
Acha wengine wetu kina siye tushudie kwa macho, na kusikia kwa masikio yetu hicho ambacho CCJ watafanya baada ya kudhulumiwa na kuonewa kwa kunyimwa usajili, na hapo ndipo uthibitisho wa Jee kweli CCJ ni chama kidume au..
 
Mbona namba ya cm haipatikani/Ikipatikana haipokelewi?
Co mambo ya ujanja ujanja haya?.......
 
Hizo Itikadi kaeni nazo mkuu tunataka kuona mnafanya mavitu. Sii mara ya kwanza nimesema hivi, kwani niliwahi kuwa nyuma ya Chadema kwa Itikadi yao mara wakageuka na kuchukua mrengo wa kushoto..
Hivyo maadam Itikadi zilizopo ni mfumo uliopangwa na wazungu kulingana na mazingira yao, kwetu sisi bado kabisa...Ni asilimia 10 ya population wanafahamu maana ya Itikadi inavyojenga mrengo, waliobakia ni maskini wenye njaa akili zao zimefunga kufikiria ama kutambua. Kuwavuta watu kama hawa unatakiwa kuwa na bakuli la Ubwabwa ambalo CCM wamelibeba..
Kazi ni moja tu kuliputa bakuli hilo na sidhani kama Ubavu mnao...Hapa ndipo umuhimu wa kutafuta nguvu mpya toka wanachama wengine kujenga jeshi la kupambana na CCM. Msitegemee sympathy, kwani historia inatuonyesha wazi kwamba Wadanganyika kwa asili yetu ni woga na wanafiki..Ni matunda ya Utumwa mabyo CCJ hamuwezi kuepuka kwa hizi ibada za Kiitikadi..

Mkuu Mkandara, bado sijakuelewa bakuli la kitu gani, fedha za takrima? Hapana. Ni kweli wapo Watanzania wengi mno wenye njaa na si kwamba kwa ajili hiyo akili zao zimefunga kufikiria ama kutambua. Wanajua sana kinachoendelea na watakuwa tayari pale tu ambapo hisia zao zitaamshwa ipasavyo. Kwa historia hii hii ya nchi yetu unayoizungumzia wananchi wale ambao walikuwa hawajui kusoma wala kuandika waliweza kuhamasika na kumng'oa mkoloni. Leo watawezaje kushindwa kuking'oa CCM endapo watapata Chama kitakachoweza kuwahamasisha kwa umahiri unaotakikana?
 
bado mnafikiria in terms of CCM na upinzani.. you need to widen the spectrum of possibilities..
Majibu rahisi kwa maswali magumu kama afanyavyo JK! Vyombo vya dola ndivyo vimevifikisha vyama vingine vya upinzani hapo vilipo. CCJ msidhani tayari mmesimama, hata kukaa ili mtambae bado.
 
Mheshimiwa Mwanakijiji mimi ni kati ya watu ambao tulikuwa hatuna uhakika sana na uthabiti na ukweli wa CCJ wakati wanaanza harakati. Nimekuwa nikifuatilia kwa karibu makala zako kuhusu CCJ na mara zote umeonesha mwelekeo wa kukiamini na kukiunga mkono kwa dhati. Lakini muda wote huo niliamua kusubiri kwanza kuona kama ni chama chenye mwelekeo wa upinzani wa kweli kwa Chama Tawala.

Lakini kufuatia kauli na maamuzi ya hii ofisi ya Tendwa ya kuzuia usajili wa kudumu wa CCJ nimeamini kuwa hiki ni chama thabiti na kinaweza kuwa chama cha upinzani wa kweli kwa serikali kuliko hivi vyama pandikizi vya upinzani. Huu inathibitisha pia kuwa serikali ya chama tawala inaogopa ujio wa CCJ.

Ninasubiri kwa hamu hii charm offensive ili nipate kuwafahamu zaidi na kujua kujua kwa kina falsafa yao na vision yao kwa taifa letu lenye ugonjwa mkubwa wa kansa ya uongozi. Nadhani ninaweza kuwa kati ya wanachama wa hiki chama kipya na hii itakuwa mara ya kwanza kuwa mwanachama wa chama cha siasa.
 
Back
Top Bottom