CCJ kuanza Charm offensive! - Ask your questions!

Mzee Mwanakijiji

Platinum Member
Mar 10, 2006
33,476
39,995
Chama cha mwamko mpya wa ujenzi wa taifa CCJ kinaanza harakati za kukutana na kuzungumza na wananchi katika kujitambulisha zaidi kwa wananchi wakati kinaendelea kusubiri usajili wa kudumu. Hadi hivi sasa maelfu ya Watanzania wameamua kujiunga na chama hiki ambacho hakina "jina kubwa" na ambacho viongozi wake "hawana majina makubwa" katika medani za siasa nchini.

Katika siku chache zijazo CCJ itapita kusalimiana na kukutana (meet and greet tour) wananchi katika sehemu mbalimbali za Tanzania Bara na Visiwani.

Yawezekana una maswali mengi kuhusu CCJ ni yapi hasa na ungependa hasa kujua nini?
 
Are these guys for real or they are just a passing fad? I guess time will tell....

Najua jinsi vyama vingine vilivyotulet down.. this is the best chance we have.. NN kwa muda wote huu umewahi kuniona lini napigia debe chama chochote cha siasa and why this?
 
Najua jinsi vyama vingine vilivyotulet down.. this is the best chance we have.. NN kwa muda wote huu umewahi kuniona lini napigia debe chama chochote cha siasa and why this?

And that's exactly what got me wondering why this one (CCJ)....then some things started running wild in my mind....huko siku za nyuma tumeshawahi kusikia watu wakiunda vyama ili kupata hela za ruzuku n.k....Lakini tusubiri tuone...haitakuwa vyema kuhukumu kabla ya makosa na si busara kuwahukumu hawa kwa makosa ya wengine (vyama vingine)...
 
kumbuka ruzuku haiji hivi hivi tu; haiji kwa kuanzicha chama bali kwa kushinda uchaguzi. Kama CCM wametengeneza mfumo wa ruzuku ambao wao ndio wanufaika wakuu basi mfumo huo huo unaweza kabisa kutumiwa kukiangusha kwa kuanzisha chama ambacho kitashinda uchaguzi, kushika hatamu na kutumia ruzuku hiyo hiyo kujijenga na kuweza kuleta uongozi unaotakiwa kwa taifa. Ruzuku basi ni matokeo tu japo kwa wengine ni lengo.
 
Mzee Mwanakijiji, as others have said, I can't comment anything now. I had a very bad dream about all these games. Definitely time will tell the whole truth. Isije ikawa story zile zile za siku zote. hahahahahahahaha. Lakini kanyaga twende mbele ninalotamani ni Kikwete na sisi m kuanguka si vinginevyo.
 
Najua jinsi vyama vingine vilivyotulet down.. this is the best chance we have.. NN kwa muda wote huu umewahi kuniona lini napigia debe chama chochote cha siasa and why this?

mkuu laizma utakuwa unausika na hiki chama pia manake unakipigia debe sana toka mwanzo.nakutakia kila la kheri na mfanikiwe kila mnachopanga.

mualike mmoja wao haje hapa basi kujibu maswali au mapema sana?
 
Ulizeni tu maswali yoyote ambayo mngependa kupata majibu kuhusu CCJ...
 
Nataka kujiunga na CCJ ila ninaishi nje ya Tanzania; je ni njia ipi rahisi ya kufanikisha azama yangu hiyo?
 
Nataka kujiunga na CCJ ila ninaishi nje ya Tanzania; je ni njia ipi rahisi ya kufanikisha azama yangu hiyo?
Hadi urudi home au tafuta mtu bongo akuchukulie kadi nadhani itakuwa rahisi. Kumbuka kulipa kadi ya mwanachama kila mwaka!
 
Nataka kujiunga na CCJ ila ninaishi nje ya Tanzania; je ni njia ipi rahisi ya kufanikisha azama yangu hiyo?

utaweza kujiunga hata ukiwa nje ya nchi; tayari hadi hivi sasa wameweza kujiunga kuanzia Japan, South Africa, Uingereza na US yenyewe.. lakini kwa sababu sasa hivi ni zaidi katika uanzilishi basi kujiunga kwa kwanza kabisa siyo kadi bali ni itikadi! Hivyo utaona uanachama wa CCJ utakuwa ni tofauti sana na uanachama wa vyama vingine vyote Tanzania, hautategemea kadi bali zaidi itikadi. Huu ndio mtindo uliopo kwenye nchi nyingi za kidemokrasia. Watu wanaposema mimi ni Republican au Democrat haina maana ana kadi rasmi ya chama bali anakubaliana na itikadi za vyama hivyo.

So, endapo baada ya kuona kuwa CCJ inaakisi fikra na mtazamo wako wa kisiasa, consider yourself a member; ni pale tu inapokuja sasa katika kuwezesha CCJ na kutafuta nafasi za uongozi ndipo uanachama wa kadi na wa kuunga mkono unapojitokeza.
 
Back
Top Bottom