CCJ kuanza Charm offensive! - Ask your questions!

CCJ kuanza Charm offensive! - Ask your questions!

MKJJ unaweza kutuwekea hizo characteritics za Far right ideology and their compatibility to ujamaa?Is your ujamaa a renewed one?Kama sivyo unaweza kutueleza ni kwavipi siasa hizo za ujamaa zilionekana kuendana zaidi na socialism na si hiyo far right ambayo inahusishwa na magharibi?Ama far right yako ni just conservatism?
Ningeshukuru sana mkuu.
 
conservatism with African flavor! Ukirudi nyuma (kurasa za mwanzo) nimefafanua kwaufupi sifa hizi.
 
Mwanakijiji naona unaongelea mistatili ya duara na miduara ya mraba! Ujamaa na Ukonzevativu kamwe havitangamani! Ujamaa ni Imani!
 
conservatism with African flavor! Ukirudi nyuma (kurasa za mwanzo) nimefafanua kwaufupi sifa hizi.

huyu mpendazoe alikuwa conservative tangia akiwa CCM au ndiyo mmempiga msasa na kumbatiza, sijui mtu ailye conservative anawezaje kukaa CCM hata mwezi mmoja tu labda awe ni mbwabwajaji tu.
 
hiyo kadi ya CCM ulinipa wewe? yaani my validation ilitakiwa itoke Chadema? Nadhani unawapa clout ambayo bado hawaistahili.

Siwo wote wana kadi wengine ni waajiriwa. Kwa hiyo unaweza usiwe na itikadi ya CCM lakini ukawa umeajiriwa na ccm na hii ni tosha kukufanya tukuite ni mmoja wao. Chadema kwa kweli ni smart tu. Dr slaa pamoja kwamba kwenye thread moja ulisema una wasiwasi naye lakini ni kiatu usichoweza kuvaa.
 
conservatism with African flavor! Ukirudi nyuma (kurasa za mwanzo) nimefafanua kwaufupi sifa hizi.
Nimerudi,hata hivyo wiki bado?

Itikadi ni ya mlengo wa kulia, nitafafanua zaidi wiki ijayo: Kwa ufupi:

- Limited but responsible government
- Minimal gvt spending
- promotion of free enterprise
- Self - Reliance
- African Socialism as corrected by the new understanding in economics, social justice
- Rule of law
- Restoration and promotion of founding principles of our nation(among them equality of status, accessibility to wealth and of opportunity, african unity - we are not afraid of Kenyas or Ugandans!, etc)
- Defense of the traditional family
- Absolutely and categorical opposition of all forms of exploitation of man by man!
- Fighting for the rights of workers and peasants of our country to give them opportunity to prosper in the globalized economy.
.. na mengine mengi..
 
wakuu nimekuwa nasoma hoja zenu hapo juu with a gleaming smile on my face.
Naamini kuwa CCJ imekuja kwa nia thabiti ya kutukwamua tulipo ili tusonge mbele.
Mimi nilijiunga kwa njia ya ujumbe mfupi wa mkononi yaani SMS. na sijajutia kufanya hivyo.
Nia yangu ni Tanzania njema kwa kila mtanzania.

ninaamini kuwa tendwa atajifanya kama msaidizi wa ziraili ktk usjaili wa hii kitu yetu. Ila inabidi tuanzishe vuguvugu la ofisi huru ya msajili wa vyama vya siasa. kuna kila dalili hii ofisi si kwa manufaa ya UMMA.

Msanii
Hapa ndio CCJ inatakiwa kuweka nguvu kubwa..... YAANI nguvu kubwa la si hivyo..... itakuwa yale yale... kwa sasa nguvu ni kuhakikisha upuuzi huu haufanyiki kinapata usajili wa kudumu haraka bila kupoteza muda, mimi kama sioni hili likitendeka.....
 
Siwo wote wana kadi wengine ni waajiriwa. Kwa hiyo unaweza usiwe na itikadi ya CCM lakini ukawa umeajiriwa na ccm na hii ni tosha kukufanya tukuite ni mmoja wao. Chadema kwa kweli ni smart tu. Dr slaa pamoja kwamba kwenye thread moja ulisema una wasiwasi naye lakini ni kiatu usichoweza kuvaa.

hiyo ajira ndio ulinipa wewe?
 
Mimi nataka kujua M mwanakijiji, kabla alikuwa chama gani? Pia nasikia CCJ inatarajia kupokea wanachama wengi toka CCM, kama ni kweli, tutarajie uozo maaana hakuna kitakatifu kinachoweza kutoka CCM, wametufanyia ufisadi muda mrefu hivyo leo ndo washtuke wakati wenzao upinzani walishapigana vita vya kutosha. Na hao hao wana CCM walikuwa wanawakejeli kuwa wanawivu wa kushindwa.

Nadhani huwatendei haki wanachama safi wa CCM ambao wamejikuta wanaongozwa wasikokutaka na bila shaka hawajaona Chama kingine makini.
 
Mwanakijiji ni wiki ya tatu ina anza toka may 15 useme utatupatia maelezo zaidi "Wiki ijayo" ,sijaona lolote zaidi ya kukumbatia off topics,sasa nimesubiri wee,lakini naona mnataka mrudi tu kwenye off topic zenu....Wengine tunauliza maswali lakini wapi!
 
hiyo ajira ndio ulinipa wewe?

Usipanick! ivi ile namba yenu ya kujiunga na CCJ ni ngapi vile pia unipe na namba ya kubatizwa kuingia kwenye itikadi yenu maana mimi itikadi yangu ni Ujamaa wa kunyang'anya mali za watu na Big gov yaani kwa kifupi socialism!
 
Mzee Mwanakijiji bado ninatamani CCJ ifanye yale ambayo inaona Upinzani haijayafanya kwa miaka 15, mpaka sasa bado sijaona jipya! Natarajia baadaya ya Ukimya wa Tendwa ( Maana yake kupuuzwa) mtafanya kitu ambacho for 15 years wapinzani wameshindwa kukifanya maana kama ni

1: Matamko Makali TLP, CHADEMA, NCCR-Mageuzi, CUF hata UDP wametoa lakini wakapuuzwa kama nyinyi mlivyopuuzwa
2: Kwenda Mahakamani DP wameenda na wakaibwaga Serikali
3: Maandamano CUF wamefanya sana hata watu wao kumwaga damu

Sasa na nyinyi baada ya Kupuuzwa nasubiri kwa hamu kufanya kama hayo apo juu au Zaidi kama ambavyo mmekwisha kujinasibu, kwa Sasa nashindwa kuwaweka katika kundi lolote
 
Mzee Mwanakijiji,
Mkuu mimi ni Conservative simply because I believe in The founding Principals of our nation. Naamini kabisa waasisi wa Uhuru wetu toka TAA,TANU hadi Muungano walikaa na kuweka sababu za msingi kabisa kwa nini tugombee Uhuru wetu hadi wakafanikiwa. Hivyo ni jukumu langu mimi kama Mtanzania ku protect na ku preserve hizo founding Principals kwani Uhuru sii Uhuru pasipo hizi sababu za Kisiasa na Kiuchumi. laa sivyo itakuwa Ujinga mkubwa kufurahia Uhuru ambao umebadilisha vichwa vya watawala tu toka mzungu/mwarabu kuja mswazi hali bado tukitawaliwa..

Everything was built around that, na itikadi yangu lazima iambatane na imani hiyo - REPUBLICANISM..Na ndio maana nchi yangu inaitwa The United Republic of Tanzania. Niliwahi soma maana ya hili neno republicanism nikajikuta naweka ahadi mwenyewe kuwa nitakuwa mrengo wa Conservative. And for that only, I believe the ideas and principles of the Tanzania founding are worth conserving and renewing...
 
Wewe Mkandara una-conserve nini? Status Quo? Our foundation was revolutionary - not conservationary! Hii ndio maana ya Conservatism kwa mujibu wa THE BLACKWELL DICTIONARY OF TWENTIETH-CENTURY SOCIAL THOUGHT EDITED BY WILLIAM OUTHWAITE AND TOM BOTTOMORE:

Conservatism is a political perspective which is universal in a way that the great modern ideologies of LIBERALISM and SOCIALISM and FASCISM are not. An instictive aversion to change, and a corresponding attachment to things as they are...
 
Usipanick! ivi ile namba yenu ya kujiunga na CCJ ni ngapi vile pia unipe na namba ya kubatizwa kuingia kwenye itikadi yenu maana mimi itikadi yangu ni Ujamaa wa kunyang'anya mali za watu na Big gov yaani kwa kifupi socialism!

Hapa naona waku-panick ni wewe. Ujamaa/socialism gani ya kunyang'anya mali za watu?
 
Wewe Mkandara una-conserve nini? Status Quo? Our foundation was revolutionary - not conservationary! Hii ndio maana ya Conservatism kwa mujibu wa THE BLACKWELL DICTIONARY OF TWENTIETH-CENTURY SOCIAL THOUGHT EDITED BY WILLIAM OUTHWAITE AND TOM BOTTOMORE:

Conservatism is a political perspective which is universal in a way that the great modern ideologies of LIBERALISM and SOCIALISM and FASCISM are not. An instictive aversion to change, and a corresponding attachment to things as they are...

Companero, kwa haraka haraka unaweza kuona kuwa conservatism ni zaidi ya conserve tu.. ni kurudia kwenye misingi. Kwahiyo tunaposema tunataka mabadiliko haina mabadiliko yote ni lazima yawe mbali na misingi bali hata kuirudia misingi ni mabadiliko. Na vile vile kuna mambo ambayo yanasimama daima kama misingi ya jamii yetu ndio maana tunapozungumzia African Socialism.. kuna mambo mawili ambayo yameshikamana sana.. African - has to do with our culture, tradition, relations etc. That as a people we can contribute something in the political make up of our country. We should not shy away from bringing african values katika siasa as if there is nothing good. This is the part of conservatism.. lakini kuna na mambo mengine mengi tu.. I believe tunaweza kabisa kufanya a new modern synthesis ya hii itikadi na tukapata kitu chetu kinachotufaa sisi kama Watanzania. Hatuhitaji kwenda mbali sana na sisi wenyewe kukipata kitu hicho.

Ila kama unaamini kuwa denition "yao" ndio tuikubali well and good. Kama unataka tusingeteneze itikadi kwa jinsi ambavyo tunataka kuielewa sisi hadi tupate approval yao that is fine with me.
 
Unajifanya haujui!- na hii dhambi itaendelea kututafuna

Ninachojua ni kwamba Socialism - Ujamaa ulirejesha kwa wananchi mali ambazo ziliporwa na wanyonyaji wachache kutoka kwa wananchi. Kama mtu alitumia madaraka ama nafasi katika jamii kujinufaisha ama kujitajirisha kwa namna moja ama nyingine kwa njia haramu na 'Socialism' ikaamua kumnyang'anya mali aliyoipata kwa njia hiyo then you have no reason to complain. It was for the best interest of the community as a whole!

Ukiangalia kwenye dictionary maana ya socialism ni: "a theory or system of social organization that advocates the vesting of the ownership and control of the means of production and distribution, of capital, land, etc., in the community as a whole."
 
Companero,
Mkuu hata sijakuelewa kabisa..Ila nitatumia lugha rahisi zaidi kwa wote ili kila mtu anielewe pasipo kutumia dictionary sijui ya nani..
Navyojua mimi hakuna Maamuzi yoyote yasiyokuwa na goals zake iwe ni kutafuta Uhuru toka kwa mkoloni, kumwondoa mtawala raia ambaye ni dikteta na hata kuondoa chama au mfumo wa utawala uliopo.. Hizi zote zitatafsirika kutegemeana na MAZINGIRA yaliyopo wakati mhusika anazungumza. Hivyo ni goals zilizowekwa ndizo huzaa ideology, hata kama iwe Revolutionary in Political ndio foundation bado yale malengo ndiyo yatakayozaa ideology in practice.
Kwa hiyo nachoweza mimi kujiuliza leo ni yapi yalikuwa malengo ya kudai UHURU wetu (GOALS) pasipo kujali posiotion ya waasisi wetu wakati wakigombea Uhuru huo..Bila shaka tulipokuwa tukigombea Uhuru wakoloni walikuwa wakikataa changes kwa sababu wao ni watawala.. bila shaka walikataa changes zozote(conservative) na kina Nyerere wakaitwa Revolutionary...
Lakini baada ya sisi kuchukua Uhuru wetu we stand ktk position tofauti kabisa..a step forward hatupo tena pale pa kutawaliwa. Na hapo a revolutinary anaweza kupinga mabadiliko yoyote ya goals zilizowekwa as founding principals za Mapinduzi yao. Tunajikuta wengine tukiwa katika position kama ya yule mkoloni kukataa changes zozote goals zetu tulizoweka wakati tunautafuta Uhuru bila kujali kama wao huko nyuma walikuwa na mitihani wa revolutionary, reformist au Conservative.

Mkuu kumbuka maneno yangu siku zote kuwa WATU na MAZINGIRA mliyopo that's what count. Marekani walipokuwa wakipigania Uhuru, Waingereza walowezi walikuwepo Conservative, Reformist na pengine wengine Revolutionary chini ya utawala wa Malkia. Lakini Yankees na kina Abraham Lincorn walikuwa Revolutionary period. Baada ya Uhuru, madaraka kuwa mikononi mwa wananchi wenyewe everything changed.. now it's about themselves (Political revolutionaries) kuwa aidha Republican hao kina Abraham waliokuwa revolutionary, wengine kuibukia Demokratic, Fascist, Nationalist, Communist, na mengineyo mengi tu kwa kutazama mfumo wa Utawala ulotokana na Mapinduzi yale..

Kwa hiyo mimi, maadam ni Republican jukumu langu ni kulinda na kutunza goals zilizowekwa na waasisi wangu TANU in practice as a Conservative..Ni kweli sikubaliani na changes zozote zinazohusu kurudisha Ukabila, Udini, Kupotea kwa Lugha ya Kiswahili, Wageni kuja kuiba rasilimali zetu, Unyonyaji, Ukabaila, Ubwanyenye, kuuzwa ardhi, wazawa kuwa second class citizen, kuwa brain washed na corrupted..Hizi ni baadhi tu ya vitu ambavyo siku zote sintakubaliana navyo kisiasa...na kiuchumi siku zote nitaheshimu haki ya kila mtu kuendesha maisha yake kiuchumi kama navyotaka Uhuru wa taifa langu kuheshimika - Political freedom, social freedom, economic freedom = Total freedom.
 
Back
Top Bottom