Mkandara, kwanini CCJ iungane na vyama vingine? Na ni chama gani ambacho kinafaa CCJ kuungana nacho na kwanini?
Thank You!
Nimependa sana mwanzo huu wa kufahamishana badala ya kubishana. Kwanza kabla sijajibu swali lako naomba kusema machache kuhusiana na tumaini jipya la wananchi. Kama nilivyokwisha sema hapo awali Ni muhimu sana kuzingatia vitu viwili WATU na MAZINGIRA ktk kila ubunifu wa suluhisho la la kutatua matatizo yaliyopo. Kwa maelezo yako CCJ imekuja na Itikadi mpya mabyo wao wanaiona inafaa na pinzani ya chama kilichopo madarakani.
Yawezekana uko right kabisa lakini sivyo wananchi wanachoamini. WATU yaani sisi wananchi tunajua kwa uhakika kwamba UONGOZI bora ndio tatizo kubwa la maendeleo yetu. NI kutokana na Uongozi uliopo ndio wamebadilisha dira ya Taifa. Dira ambayo baba wa taifa na waasisi wa chama walituahidi kufika hiyo nchi ya Kufikirika. Uongozi mbaya umeshindwa kufuata Itikadi au wanaweza kuibadilisha.
Sasa maadam fikra za wananchi wengi ni kuwepo kwa viongozi wabaya, viongozi ambao walibadilisha mengi ikiwa ni pamoja na miiko na maadili ya uongozi kwa faida yao wenyewe ndio walioharibu Itikadi nzima ya chama CCM... Na kama unakumbuka JK alipoingia madakani hata yeye na Lowassa walisema kwamba wamerithi mapungufu mengi toka Utawala wa Mkapa na Mkapa kwa Mwinyi ili mradi kila mmoja wao kuepa ukweli kwamba jukumu ni lao kuyaondoa matatizo waliyorithi. Hivyo, watu hawa wapiga kura wanachojua ni kwamba Uongozi wa CCM ni mbaya..Na chama ni watu.
Pili, Katika mazingira tulokuwa nayo leo haiwezekani kupata mapinduzi ya kweli kwa kutumia siasa za miundo ya Kiitikadi. wananchi wapiga kura hawajui kabisa hizi habari za Itikadi kwa sababu ya njaa kali. Akili zao zimefungwa kwa njaa na umaskini hivyo kutengeneza mazingira magumu sana kisiasa hasa kwa vyama vya Upinzani..Katiba na taratibu zote za uchaguzi ni mbaya kiasi kwamba mwanya uliopo ni mdogo sana kwa vyama vingi kuweza kupata Ushindi..
Mkuu wangu wananchi hatutajali kama ni CCJ iliyounganisha nguvu zake na Chadema au CUF..Ujumbe huu ni kwa vyama vyote vya Upinzani kutengeneza mazingira ya ushindi bila kutumia porojo za siasa isipokuwa kutengeneza mazingira ya kisayansi. Na hakuna uwezekano wowote kwa vyama hivi kushinda pasipo kuunganisha nguvu zao. CCJ mkiwa wa kwanza kunyoosha mkono, sii vibaya hata kama Itikadi yenu kisiasa ina tofauti kubwa na wengineo. Mkuu majuzi tu Conservative ya Uingereza imeungana na Demokratic (The far left) kumwangusha Labour (kati kushoto). Hivi vyama vinapingana kiitikadi kuliko Conservatives na labour lakini kwa sababu walitaka kumwondoa Gordon Brown, na wakajua mazingira yanayoweza kuleta mgawanyo wa kura, wakatazama uwezekano wa kisayansi kulingana na mazingira yao ndipo walipoitisha uchaguzi kabla ya kusubiri miaka miwili ijayo, Upepo unaweza kugeuka.
Sisi hapa TZ hatuna maswala ya mseto. JK akishinda uchaguzi he takes all hata kama Bunge mtagawana na CCM. Kwa hali yoyote ile najua fika wabunge wengi wa CCM hawatarudi 2010, lakini CCM sio wajinga hivyo, nao wamejiandaa kuwaondoa wale wasio uzika mapema kwa kuweka kura za wanachama wao. Hivyo Wabunge wasioweza kurudi watachujwa mapema ktk uchaguzi wa mwanzo na ukitazama huko Mikoani CCM bado ndio jina kubwa. Ukimuondoa mtu wasiyempenda ukamweka mwingine tayari CCM itaanzisha Uhai mpya na ushindani utakuwa baina yenu na huyu CCM mpya anayependwa na wanachama mikoani. Kwa Tanzania na mazingira yake ni kazi kubwa kuishinda CCM kama mapungufu sio ya mgombea.
Kwa hiyo mkuu wangu swala kubwa la wananchi...ni kuwaondoa CCM madarakani. haihusiani kabisa na Itikadi, malengo wala katiba yao.. Asilimia 80 ya Watanzania hawajali hizi siasa za Itikadi ikiwa tatizo kubwa nchini ni utekelezaji. Na kazi kubwa ya vyama vya Upinzani inatakiwa kujihusisha zaidi na kubuni mbinu za kuuondoa Uongozi uliopo (CCM) na sio kuvumbua Itikadi mpya ambazo haziwezi kufanya kazi hadi siku wameshika madaraka. Na kibaya zaidi tupo ktk taifa la Wajinga na Malimbukeni wenye njaa kali ambao madai yetu makubwa ni - What have You done for me lately! Hii kiswahili mingi ya itikadi na malengo haiwagusi kabisa..
Hii ndio sababu ya CCJ kuanzisha mwamko mpya wa kutunga Muungano wa vyama vya Upinzani. Mkianza na hatua hii hata kujaribu kuungana na wengine kuunda jeshi kubwa mtakuwa mmeanzisha kitu kipya na hakika mtawajua wale wanaotaka kusimama nanyi ktk mapambano na wale wanaojitenga wakitaka madaraka na ruzuku za bunge kwa maniufaa yao binafsi.. Wewe kama Mwanakijiji utawaanika wote hapa na magazetini ili wananchi tusiwape kura zetu..Tunajua fika CCM ina mapandikizi yake ndani ya vyama vyote vya kisiasa na huu ndio wakati wa kuwanasua na kuwatupa nje..Huu ndio wakati pekee wa kufanya mapinduzi ya haki. Nyoosheni mikono yenu msiwe kama Chadema na CUF tulowambia mwaka 2005 wakashindwa kufanya hivyo kisha kwa ujinga wao wakaja taka kuungana baada ya kushindwa uchaguzi mkuu. It was a stupid move, na rahisi kwa CCM kuwavuruga.