Uchaguzi 2020 CASE STUDY - Jimbo la Hai - Walitumia teknolojia gani kupata matokeo sahihi ya kila kituo ndani ya saa 8?

Waulize maana watapewa tu.

Simply ni neno la kilatini, meaning; "a place to stand", yaani malalamiko yako mahakamani yana "base" kwenye nini.
Me Naelewaaa Mkuu... Mara nyingi kwenye kila kesi huwa tunaangalia je parties wana locus stand au wamedandia tu gari kwa mbele
 
Hatua nyingi Sanaa Mkuu.....
-Kwenda jumuiyaa za kimataifa..
-Maandamano ya Aman.. tena yangefanikiwa maan watu walikuwa na morale kubwa sanaa
-kufungua pingamizi mahakaman n.k
Maandamano ya amani katika kipindi kipi ?

Kwenda kwenye jumuiya za kimataifa kufanya nini ?
 
Hatua nyingi Sanaa Mkuu.....
-Kwenda jumuiyaa za kimataifa..
-Maandamano ya Aman.. tena yangefanikiwa maan watu walikuwa na morale kubwa sanaa
-kufungua pingamizi mahakaman n.k
Kufungua pingamizi mahakamani dhidi ya nini mkuu ?
 
Maandamano ya amani katika kipindi kipi ?

Kwenda kwenye jumuiya za kimataifa kufanya nini ?
Maandamano ya Aman kushinikiza tume huru kabla ya uchaguzi Mkuu.....
Kuomba jumuiya za kimataifa kushinikiza kuwepo kwa tume huru
 
kutokuwa na iman na tume....
Mahakamani huwa hatuendi kwa hisia tunaenda kwa facts.

Kukumbusha tu mahakamani tumepeleka kesi mbili moja ni kupinga wakurugenzi wa wilaya kuwa wasimamizi wa uchaguzi mahakama kuu ilikubali ombi letu ila mahakama ya rufaa ikaruhusu wakurugenzi kusimamia uchaguzi.

Mpaka hapo mlango wa mahakama tulishapita na tukagonga mwamba.
 
Maandamano ya Aman kushinikiza tume huru kabla ya uchaguzi Mkuu.....
Kuomba jumuiya za kimataifa kushinikiza kuwepo kwa tume huru
Mkuu maandamano huwezi kuyaamsha tu there must be a cause.

Platform ya uchaguzi huu imetupatia hiyo cause kwa uwazi kwa kila mtu.

Kuhusu jumuiya za kimataifa Uchaguzi ni internal affairs ndiyo maana mashinikizo yoyote hayawezi kutolewa zaidi ya matamko ya kibalozi tu.
 
mkuu... ishu ni kwamba hakuna mahakama ya bongo ya kuiamin...
Hapa ni kama Rev mtikila case ya 2011 tunaenda African court tunapeleka pingamizi letu na facts mahakama ya africa itaamua...
Maamuzi yake sawaa sio binding kwa Tanzania ila yatabind karibia commission zote ambazo zitakuja kuangalia uchaguzi....
After Hizo commission za SADC,EAC na Au hawawez kusema uchaguzi ni wa huru na haki kama maamuzi ya african court hayajafatwa....
hii itakua ni hatua moja ya kuelekea demokrasia....
Tanzania italizimika ku domesticate yale maamuzi ili kulinda heshima yake kimataifa
 
Hayo matokeo ya vituoni hayakutumika kwenye majumuisho
Nilikuwa naongea na baba. Yeye alikuwa mwenyekiti wa TANU wa wilaya. Aliniambia mambo ya kutafakarisha sana. Alisema kuwa Magufuli alikuja na CCM mpya. Alipoingia nadarakani hakuwa anatambua Chama. Alikuwa anaita Serikali ya Magufuli badala ya Serikali ya CCM. Mbele kidogo pale tukaona Wazee wa CCM wanatiwa msukosuko. Mzee Yusufu Makamba, mzee Abd. Kinana, Nape, Januari na wengine waliokuwa nguzo za Chama wakatiwa msukosuko. Baadaye tukamsikia akisema kwa wazi kuwa Viongozi waliomtangulia yeye hakuna walichofanya. Tuliona Mzee Mkapa akilipinga hilo kwa nguvu na wazi. Hata mzee Kijwete amelipinga hilo wazi. Lakini jina hili la CCM MPYA limetumika marakwa mara.
Hii ni ccm ya akina Bashiru na kina Polepole. Ni ccm isiyo na maadili wala isiyozingatia itikadi yake ya awali. Si ya kijamaa wala ya kibepari. Ni ccm inayotumia nguvu badala ya hoja. Hata hekima ya kawaida tu ccm hii mpya haina. Magufuli anasema, "Wewe mkurugenzi, ukiwa msimamizi wa uchaguzi siwezi kuwa nakupa mshahara, gari , nyumba na narupurupu mengine alafu umtangaze mpinzani eti kashinda uchaguzi!" Maneno haya usingesikia yakitoka kwa Wazee wale wa namna ya Makamba wala Kinana. Walikuwa viongozi wa chama chenye hekima na maarifa. Bashiru alisema wazi kuwa ccm itatumia vyombo vya dola kubaki madarakani. Loh! Hiyo ndoyo hekima ya ccm hii mpya.
Mara tukaona utamaduni mpya wa ccm hii mpya kwenye uchaguzi wa viongozi wa serikali za mitaa mwaka jana. Mzengwe ulifanywa na wagombea wa upinzani wakaenguliwa wote. Tulikuwa hatujui kwa kumbe huo ndio utamaduni wa ccm mpya. Imedhihirika kwenye uchaguzi mkuu huu kuwa ccm hii inataka kushinda kwa mabavu, hila, na unyanganyi. Tuliona watia nia wa upinzani wakitekwa na kunyanganywa fomu ili wasirudishe. Tuliona wengine wakitiwa ndani kwa kutumia polisi na hata takukuru ilitumika. Tuliona uenguaji wa kimkakati wa wagombea wa upinzani kwa kutumia NEC ambapo kila mwenye macho yanayoona aliona mkakati wa ccm mpya wa kushinda uchaguzi nje ya sanduku la kura. Kampeni zilidhihirisha nia hii ya ccm mpya. Hakuna kwa wapinzani kutumia vyombo vya habari vya umma wala vya binafsi. Hakuna wapinzani kubandika mabango ya wagombea uraisi popote. Wagombea wa upinzani walipewa adhabu ya kutokufanya kampeni kwa makosa ambayo wale wa ccm mpya walifanya na wao hawakuguswa.
Lakini uchaguzi kama huu haujaonekana miaka ya nyuma. Makaratasi ya kura zilizopigwa yalikamatwa kwa maelfu sehemu mbalimbali. Mwisho hata Kanuni ya majumuisho haikufuatwa. Ilikuwa ni kujaza idadi ya kufikirika na kutangaza mshindi kwa kuwa mawakala wa upinzani walifukuzwa.
Mwisho mzee yule alisema kuwa kama hali hii itaachwa kuendelea, yaani kama hakuna hatua yoyote itakayochukuliwa kwa heri ama kwa shari kukomesha utamaduni wa kundi hili wa kushinda kwa kupora kura, huu utakuwa mwanzo wa mwisho wa taifa zuri la Tanzania tuliyoipenda. Utakuwa mwisho wa demokrasia kwa nchi yetu.
 
Ndio tumesha mchinja kwa hooks na kelele zako hazita saidia
 
Maoni yangu nazani umeyaona kuhusiana na hili swala la mahakama na jumuiya za kimataifa....
 
Hivi unajua kuwa waangalizi wa uchaguzi EAC wamesema ulikuwa huru na wa haki ?

Hivi unajua SADC pia wamesema uchaguzi ulikuwa huru na wa haki ?

Hivi unajua Tanzania pamoja na kesi ya Mtikila kuamuriwa kuwa Tanzania iruhusu mgombea binafsi mpaka sasa Tanzania haijatekeleza uamuzi huo ?

Hivi unajua Tanzania mpaka imeshajitoa law taasisi binafsi na mtu mmoja mmoja kupeleka kesi mahakama ya Africa ya haki za binadamu?

Hivi unajua sasa hivi Tanzania imetunga sheria inayozuia mtu kufungua shauri la katiba katika mahakama za ndani hapa nchini ?
 
Huyu hajui mkoa Kilimanjaro ni mkoa mdogo sana baada ya dar
Hai ni jimbo dogo sana ukiangalia maeneo ambayo kuna makazi ya watu, kijiografia vituo vipo karibu karibu, kuwahi kutangazwa kwa matokeo sio ushahidi.
 
Wakikosaga hoja wanaanzaga vioja ndio maana wanaita wenzao misukule!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…