The Palm Tree
JF-Expert Member
- Apr 13, 2013
- 7,951
- 12,535
Jimbo la uchaguzi la HAI liko mkoa wa Kilimanjaro. Ni jimbo ambalo "the most wanted person" na watawala wa CCM, mwenyekiti wa taifa wa chama kikuu cha upinzani Tanzania - CHADEMA ndugu Freeman Aikael Mbowe aligombea ubunge kupitia chama chake hicho.
Ilikuwa kwa vyovyote vile asitangazwe mshindi either by HOOKS or by CROOKS. Hili lilikuwa apizo la Magufuli na wenzake na walilifanya kwa ushamba na ujinga wa viwango vyote vya ujinga duniani.
Kwa waliopoteza kumbukumbu, jimbo la HAI ndilo lilikuwa jimbo la kwanza kutoa matokeo ya uchaguzi takribani masaa yasiyozidi 8 baada ya vituo vya kupigia kura kufungwa ile saa 10:00 jioni ya tarehe 28/10/2020.
Kwa teknolojia ya uhesabuji kura ktk vituo vya kupigia kura, kujaza fomu mbalimbali, compilation ya matokeo ngazi ya kata na jimbo ili kumpata mshindi wa udiwani na mbunge na kwa kuzingatia jiografia ya majimbo yetu ya uchaguzi yote Tanzania mtu anaweza kuona ugumu wa kuikamilisha kazi hiyo ktk interval ya masaa takribani 9 au 10 tu katika ngazi ya jimbo.
Bahati njema mimi nilikuwa mmoja wa maafisa wa uchaguzi huu nikiwa mwajiriwa ndani ya serikali, nikipewa jukumu hili pia.
Katika eneo nililosimamia mimi, kituo cha mwisho kuleta matokeo wilayani (jimboni) ili kufanya majumuisho kumpata mshindi wa ubunge ilikuwa ni saa 2asb kesho yake yani 29/10/2020!
Kwa kawaida, baada ya kituo cha kupigia kura kufungwa saa 10:00 jioni, uwezekano wa mtu wa mwisho kupiga kura inaweza kuwa kati ya saa 1 hadi 1.30 kutegemea na kituo na idadi ya wapiga waliokuwepo kabla ya saa 10 jioni. Hii maana yake mtu wa mwisho alipiga kura saa 11:30jioni kabla ya kuanza kuhesabu.
Kuna vituo vingine zoezi la kuhesabu kura, kubishana na mawakala na kutatua migogoro inayojitokeza na kujaza fomu mbalimbali ikiwemo ya taarifa ya kituo lilikwenda hadi saa 4usiku.
Baada ya hapo kwa kawaida msimamizi wa kituo cha kupigia kura hubeba masanduku ya kura na matokeo hadi makao makuu ya kata ili kufanya majumuisho ili kumpata mshindi wa udiwani na kumtangaza.
Baada ya hapo msimamizi wa kituo cha kupigia kura wakiambatana na msimamizi msaidizi wa uchaguzi ngazi ya kata hubeba masanduku ya kura, matokeo ya kura za ubunge na urais hadi jimboni/wilayani kwenda kufanya majumuisho ya kura za ubunge na Urais..
Likifanyika hili, mshindi wa ubunge hutangazwa na kisha msimamizi wa uchaguzi wa jimbo hutuma NEC matokeo ya kura za urais za jimbo...
Je, haya yalifanyika pale Hai katika interval ya masaa machache vile? How exactly?..
Na pengine tujaribu kujiuliza HAI, Kilimanjaro jiogarafia ya jimbo hilo ikoje? Walitumia teknolojia gani kiasi ambacho ndani ya masaa 8 tu baada ya vituo vya kupigia kura kufungwa wakawa wamepata matokeo sahihi ya kila kituo na kuwatangaza wasindi wa udiwani na ubunge?
Mimi nasema, ni uongo. Haiwezekani abadani unless matokeo yawe yalikuwa yakitumwa kutoka vituo vya kupigia kura kwa njia ya mtandao wa computer!
Matokeo ya kawaida ya majimbo - ubunge japo na yenyewe ni wizi mtupu yalianza kutangazwa kesho yake ya tarehe 29/10/2020 kuanzia ingalau saa 6mch..
Ni wazi bila shaka kulikuwa na matokeo mengine "fake" tofauti na matokeo halisi yaliyotumika kutangaza washindi.